Siku hizi Ligi za Ulaya hazina watazamaji wengi huku kwenye vibanda umiza

Siku hizi Ligi za Ulaya hazina watazamaji wengi huku kwenye vibanda umiza

Pia matangazo, Azam ikifika mechi ya yanga au simba inatangazwa mno hata kama sio mdau wa mpira utaijua tarehe na saa.

Kwenye bar nyingi wana azam tv na sio dstv kwa sababu za kibiashara.

Na Simba na Yanga kuendelea kujitutumua kimataifa ndo kabisaa wanazidi kuifanya ligi ifuatiliwe sana.

Kipindi tunakua miaka ile ilikua nadra kukuta mtu ana uzi wa simba/yanga badala ya timu za ulaya, ila siku hizi jezi za timu za ndani zinavaliwa mno mtaani.

Tupende vya kwetu.
 
Siku hizi services za kustream ni nyingi. Na unaweza kustream mechi za ligi nyingi za nje hizi timu zetu ili ustream labda icheze michezo ya kimataifa.

So hapo mtu anayeweza kumudu bando hutamuona bandani.

Man City kuigeuza epl nyumbani kwake.

Kuwepo kwa madish cheap (canal +)

Location pia. Mfano kijiji nilipo haijalishi ni mechi gani watu hawajai, haijalishi ni mechi ya nje au ya ndani na hata awe anacheza nani.

Hawa canal + wangepata usajili rasmi Tz hawa dstv wangefunga virago
Canal wamenunua hisa za dstv 42% soon watakuwa wamiliki wapya wa dstv
 
Wote mmeshindwa kubaini kwamba corona ndio imesababisha. Hao wapuuzi walivyopiga lockdown na baadae kucheza bila mashabiki ... Ladha ya ligi hizo ilianza kushuka. Kuanzia wakati huo nimefuatilia na kubaini watu waliacha kwenda ukumbini kutizama mechi za ulaya.

Kuna wakati man u vs araenal zilikuwa zikicheza unakuta vibanda umiza unakosa seat. Goli likiingia ni kelele za kutosha lakini siku hizi aah!!
 
1:technology, watu wanastream mtandaoni
2: tv zipo nyingi tofauti na zamani
3:kushuka kiwango kwa man u , hii ni sababu kubwa sana
4:man city kudorminate epl kwa muda mrefu
 
Wanaofuatilia mpira wa bongo ,80% hawajui mpira ni ile tu sababu azam media imerahisisha access ya kutazama mechi hizo na pia wasipitwe na mabishano yanayoendelea mtaani.
Angalia hao mashabiki wa mpira wa bongo kina mama na wadada shazi hawajui lolote ni ile tu ushabiki wa na mimi nimo.

Mpira wavbongo hapana sijawahi kuwa na mzuka nao kabisa maana ni vichekesho, pasi inapigwa kwasababu mtu yupo mbele na magoli si yakutegenezwa bali sababu tumefika golini basi ww piga tu😂, yaani mpira hauna mbinu kabisa mchezaji anapiga krosi iingie ndani sio kwasababu kamuona mtu ila anapiga tu watu wagombanie tu mpira au shoot unaona linapaa juu anapiga kokote tu yaani ni kubahatisha kulenga goli.

Kuna siku niliona George ambagile anachambua match za bongo sijui ilikua mashujaa na tanzania prison , nikaona kabisa anatupiga fix et sijui mashujaa wakiwa na mpira wanacheza sijui 4 42 wakiwa hawana mpira sijui wanabadilisha mfumo sijui 3 2 3 nini sijui kitu ambacho si kweli , team nyingi za bongo zinacheza mpira ili mradi hakuna mbinu yoyote ile inatumika.

Japo kuna kipindi niliangalia baadhi ya mechi nikashangaa mpira waliocheza ulikus mzuri niliona kama maajabu mpira huo kuchezwa bongo , kuna mwaka simba vs alhaly na hata juzi juzi yanga vs waarabu walishinda 4 ile na baadhi ya mechi chache chache.

Kwa mbaali kidogo yanga anajitahidi hata pasi na possession play unaona kuna mpira anacheza hasa last season .
 
Kabisa mkuu 🤣🤣 mara full back ndio anakuwa winger yani vitu havieleweki
Mpira wa Ulaya umekuwa science sana wachezaji wamekuwa robots
Haya Rodri kabeba balon mbele ya kina Martinez Vini n.k lakini ukiangalia huoni hata uchezaji wa sanaa ya mpira ndani ni aghalabu kusikia mtoto akisema ndoto yake ni kuwa kama Rodri
Ukiangalia ligi kama ya Roshn Saudia Kuna mtu kama Mitrovic husikii akitajwa ila jamaa anafanya mpira uonekane kitu kizuri ila sababu hayuko Ulaya humsikii kwenye tuzo yoyote ya dunia
 
Mpira wa Ulaya umekuwa science sana wachezaji wamekuwa robots
Haya Rodri kabeba balon mbele ya kina Martinez Vini n.k lakini ukiangalia huoni hata uchezaji wa sanaa ya mpira ndani ni aghalabu kusikia mtoto akisema ndoto yake ni kuwa kama Rodri
Ukiangalia ligi kama ya Roshn Saudia Kuna mtu kama Mitrovic husikii akitajwa ila jamaa anafanya mpira uonekane kitu kizuri ila sababu hayuko Ulaya humsikii kwenye tuzo yoyote ya dunia
Umeandika kituko itoshe kusema hujui mpira
 
Ahaa
Umenikumbusha mpira wa zamani kipindi nacheza mpira. Utasikia kauli ya wajita " bhuma imbele" yaani kipa wewe tupia mbele tutajuana hukuhuku🤣🤣
Siku hizi mpira wa aina hiyo haupo tena.
Enzi izo kona ikipigwa tunamwambia mpigaji we idondoshe pale pale kwa kipa, ikidondoshwa watu tunaingia nyavuni na mpira pamoja na kipa refa analeta mpira kati. Sasa hivi sheria kibao mpira umekua soft. Kanuni kibao mpira umekua kama play station.
 
Back
Top Bottom