Siku hizi ukitangaza Ndoa na una mwelekeo wa maisha, suala la Mahari hawakulazimishi sana

Siku hizi ukitangaza Ndoa na una mwelekeo wa maisha, suala la Mahari hawakulazimishi sana

Rasterman

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
33,894
Reaction score
44,117
Kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele swala la mahari linaonekana kuwa la kizamani. Sijui kama ndio kustaarabika au ni kuachana na mila na desturi zetu.

Kwa upande mwingine hii ni fursa kwa vijana wa kiume waliokuwa wakiogopa mambo ya mahari kwanza. Siku hizi mambo mbwelele.

Siku za nyuma ili uoe lazima mwanaume uwe umejenga nyumba kwanza. Lakini siku siku hizi geto la chumba kimoja tu jiko unabeba. Kwanza utaanza kuona manzi kila anapokutembelea anaacha kitu kimoja kimoja mara kandambili, mkufu siku zingine brauzi.

Vijana msiogope. kuoa kumerahisishwa.

Mimi nawashtua tu.

asubuhi njema.

1624089340464.png
 
Ndugu unaongea kwa uzoefu au umesimuliwa? Juzi tu hapa jamaa yangu mahari pamoja na makorokoro yote imemtoka 3M na kaoa mluguru tu, nenda uchagani utajuta
Jamaa unatushusha kwahiyo umeona waluguru ndio wa bei rahis? Eti ni mluguru tu.🤣🤣
 
Sitakuja nitoe million 1 kwa kiumbe kinachoitwa mwanamke,et mahali... ..

Never ever
 
Huo urahisi unaozungumzia inategemea na jamii, nenda Mara, mikoa yenye jamii ya wasukuma......kurahisishwa pia inategemea na binti unayemuoa uyo wa kujikabidhi kabla ujakabidhiwa na wazazi wake
 
Haya mambo ya mahari ni mambo ya kizamani sanaaa kama unataka kuoa ongea na binti myamalize na mkubaliane hata hiyo mahari muelewane mwisho ni kiasi gani kulingana na uwezo wako binafsi nilimwambia wife awaambie kabisaa wazazi wake siwez toa zaid ya Milioni 1 na ndio niliyotoa japo nilikuwa na uwezo wa kutoa zaid ila sikuona maana
 
Ofcourse lazima muwe na mipango nyinyi kama nyinyi. Wife to be lazima awapange wazazi yeye mwenyewe kama kweli ana nia ya kuolewa.
 
Huo urahisi unaozungumzia inategemea na jamii, nenda Mara, mikoa yenye jamii ya wasukuma......kurahisishwa pia inategemea na binti unayemuoa uyo wa kujikabidhi kabla ujakabidhiwa na wazazi wake
multifactorial sio?
 
Back
Top Bottom