Siku hizi waumini tunapenda mahubiri ya kumiliki vitu vya dunia

Siku hizi waumini tunapenda mahubiri ya kumiliki vitu vya dunia

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
πŸ”˜ Siku hizi waumini hatutaki INJILI ya kuambiwa/kuhubiriwa;
βœ“Acha umalaya ni dhambi.
βœ“ Acha kudanga ni dhambi.
βœ“ Acha wizi ni dhambi.
βœ“ Acha uchawi ni dhambi.
βœ“ Acha kutoa mimba ni dhambi.
βœ“ Acha pombe ni dhambi.
βœ“ Acha rushwa ni dhambi.
βœ“ Acha ushoga na usagaji ni dhambi.
βœ“ Acha kubaka watoto.
βœ“ Acha kuchonganisha watu.

πŸ”˜ Bali, huku tukiendelea kutenda dhambi tunataka INJILI ya kuambiwa/kuhubiriwa;
βœ“ Mwaka huu lazima ununue gari.
βœ“ Mwaka huu lazima upande cheo.
βœ“ Mwaka huu lazima upate ajira.
βœ“ Mwaka huu lazima utajenga.
βœ“ Mwaka huu lazima ufunge ndoa.
βœ“ Mwaka huu lazima umalize chuo.
βœ“ Mwaka huu lazima upate watoto.
βœ“ Mwaka huu magonjwa yatakuacha.
βœ“ Lazima biashara yako ifanikiwe.
βœ“ Mwaka huu lazima utafanikiwa.

Right Marker,
Dar es salaam.
 
πŸ”˜ Siku hizi waumini hatutaki INJILI ya kuambiwa/kuhubiriwa;
βœ“
Acha umalaya ni dhambi.

βœ“ Acha kudanga ni dhambi.

βœ“ acha wizi ni dhambi.

βœ“ acha uchawi ni dhambi.

βœ“ acha kutoa mimba ni dhambi.

βœ“ acha pombe ni dhambi.

βœ“ acha rushwa ni dhambi.

βœ“ acha kubaka watoto.

πŸ”˜ Bali, huku tukiendelea kutenda dhambi tunataka INJILI ya kuambiwa/kuhubiriwa;
βœ“Mwaka huu lazima ununue gari.

βœ“ Mwaka huu lazima upande cheo.

βœ“ Mwaka huu lazima upate ajira.

βœ“ Mwaka huu lazima utajenga.

βœ“ Mwaka huu lazima umalize chuo.

βœ“ Mwaka huu lazima upate watoto.

βœ“ Mwaka huu magonjwa yatakuacha.

Right Marker,
Dar es salaam.
Kwa nini unataka vitu vya mbinguni?

Ina maana Mungu anapenda kuona watu wanateseka Duniani?
 
πŸ”˜ Siku hizi waumini hatutaki INJILI ya kuambiwa/kuhubiriwa;
βœ“
Acha umalaya ni dhambi.

βœ“ Acha kudanga ni dhambi.

βœ“ acha wizi ni dhambi.

βœ“ acha uchawi ni dhambi.

βœ“ acha kutoa mimba ni dhambi.

βœ“ acha pombe ni dhambi.

βœ“ acha rushwa ni dhambi.

βœ“ acha kubaka watoto.

πŸ”˜ Bali, huku tukiendelea kutenda dhambi tunataka INJILI ya kuambiwa/kuhubiriwa;
βœ“Mwaka huu lazima ununue gari.

βœ“ Mwaka huu lazima upande cheo.

βœ“ Mwaka huu lazima upate ajira.

βœ“ Mwaka huu lazima utajenga.

βœ“ Mwaka huu lazima umalize chuo.

βœ“ Mwaka huu lazima upate watoto.

βœ“ Mwaka huu magonjwa yatakuacha.

Right Marker,
Dar es salaam.
Kuutafuta ufalme wa mbinguni hakupo tena;baraka zote hupatikana hata kama hujamkiri Kristo kuwa alikufa ili atuokoe na ulimwengu uliojaa maovu yanayomchukiza Mungu.so sad
 
Sasa kama mtumishi anamiliki Grenadier mbiliπŸ˜† hana hata miaka 5 kwenye utumishi ila ana uwezo wa kumnunulia mkewe range rover vogue 2024 model ikiwa ni gari ya billion na point kadhaa pamoja na kodi.

Kwanini waumini wasitamani hayo maisha? Nani hapendi G wagon kati yenu😁?
 
Hayo maisha si mbadala ya ufalme wa Mbinguni.Mungu alikusudia tuishi ndani ya ufalme wake ;kumpenda yeye kwa mioyo yetu ,roho zetu akili zetu na kwa nguvu zetu ,kisha yeye atupe maisha ndani ya ufalme wake.
 
Ni mwendo wa maombi ya utajirisho na mafanikio,
hayo ya utakatifu/usafi wa roho, matendo mema sio muhimu, sio lazima.

Ajabu hawamo na hawatakuja kuwepo wenye kundi la kumiliki mali, majengo, viwanda, maduka, kampuni
 
Back
Top Bottom