Siku ikatokea nikawa Rais wa nchi nitahakikisha haya yanatokea. Weka yako pia tuchuane kuipa nchi mawazo chanya

Siku ikatokea nikawa Rais wa nchi nitahakikisha haya yanatokea. Weka yako pia tuchuane kuipa nchi mawazo chanya

winnerian

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
379
Reaction score
603
Pita yote usiachie nusu tafadhali
100. Kutoa motisha kwa vijana kwa kila namna inayowezekana kupenda mambo ya msingi. Hii itawezesha kuwafanya wapende kujihusisha na ubunifu, uzalendo, kujitegemea, kutoa mchango mkubwa kwa taifa lao. Sio kama hali ilivyo sasa wengi wao wanatamani na kujitahidi sana kuwa uchi mtandaoni, wanatumia muda mwingi kubeti na kucheza upatu kama vile biko na kadhalika.

101. Nitaweka sheria kali dhidi ya maadili na utamaduni bora kwa kila rika. Mfano kwasasa watoto wadogo wanapata mimba zisizokusudiwa na wanatelekezwa kinapatika kizazi kisichokuwa na malezi bora na hatimae taifa lenye watu wasiojitambua wala kujua maadili na misingi ya maisha yao kama watanzania. Sheria ya ndoa itaboreshwa na kuwekewa meno makali kiasi kwamba itadumisha utamaduni wa kuwa na famili bora na sio bora familia. Taifa linaanza na familia zenye upendo na amani.

200. Nitafuta sheria zote zinazomkandamiza mtanzania mwenye nia ya kujiinua kiuchumi. kuna sheria nyingi zipo ambazo zinawanyima wazao hususani vijana fursa nyingi na kusababisha mikopo yote tunayopata kutoka kwa wadau wa maendeleo kuchoropokea china.

201. Nitaweka ukomo wa kushika madaraka ya kisiasa kwa kila nyanja kuanzia kitongoji hadi taifa kwa ujumla, sio mtu huyo huyo kuanzai nyerere hadi samia anatuongoza na mawazo yale yale.

300 Nitaanzisha kitengo mahususi na chenye utalaamu wa hali ya juu cha kushauri na kutoa maamuzi ya mwisho kuhusu mustakabali wa maendeleo ya nchi. Sio kama ilivyosasa kundi la watu wengi wasiojua dunia inaelekea wapi wanakusanyika kwenye jengo linaitwa bunge na kuchambana kisha kulipwa na kurudi majumbani mwao. Kitengo hiki kitakuwa na watu wachache na wenye uchungu an uzalendo wa hali ya juu katika kupeleka nchi mbele kimaendelo.

301. Nitahakikisha naipatia nchi mahakama yenye nguvu kuliko mtu binafsi au taasisi yeyote ile kwenye nchi. Haki ni moja ya mambo ya msingi kwenye kupata maendeleo. Nitaweka mfumo ambao hataruhusu kamwe kutokea kwa rushwa kwenye eneo hili. Sheria kali na taasisi za kuchunguza utendaji wa mahakama zetu zitaimarika maradufu hadi watendaji kazi katika mahakama wafikirie mara mbili mbili kula rushwa.

400. Nitaweka mfumo mgumu mnoo wa kuwachuja viongozi wetu. Itampsa mtu yeyote anaetaka kuwa kiongozi awe mtu sahihi na mwenye uzalendo na usafi wa hali ya juu Kuanzia aipoanza maisha yake hapa duniani hadi alipo sasa na hiii sio tu kwamba itakuwa kigezo pekee bali vigezo vingi ili tuwapte viongozi wenye ndoto na uwezo wa kizitimiza ndoto zao.

401. Nitaisuka tume ya uchaguzi ambayo sio tu kwamba itakuwa huru bali itakuwa tume yenye uwazi kwa 100%. Uhuru wa tume hautoshi bali tume yenye uwazi kwa silimia zote ndio tume yenye kutupa viongozi tunawataka.
500. Uchaguzi utafanyika kwa uwazi kuliko hata bidhaa zinazouwa kando ya barabara. Yanani mtu akipita amepita kwa haki na takaekosa atakosa kwa haki.

501. Mwisho kabisa nitaweka uzio na mbwa wakali kwenye suala zima la maadili kama watanzania wenye nia ya kusonga mbele kwa heshima, maadili mazuri, na yenye kuleta tija katika tafia. kwasas maadili mabovu yametawala sana sio tu kwa wanawake hata kwa wanaume. Watanzania kwasasa wanashabikia na kuubariki uhuuni na uzandiki kuliko kushabikia mambo yenye tija kwa uzao waa ujao.
 
1. Nitafuta utawala wa kisiasa.
Hii itaenda sambamba na kuweka mifumo mipya ya kushika dola. Kwa hiyo CCM na vyama vingine vitakuwa kama VIKOBA.

2. Ualimu itakuwa ni kazi ya kukimbiliwa kwani ndio kazi pekee itakayo kuwa na mshahara mkubwa,marupurupu na mikopo yenye riba nafuu <10%.

Hii itaenda sambamba na kuboresha taaluma hii, na pia kupiga marufuku mikopo ya vibanda umiza.

3. Samaki wote wataliwa na kusindikwa hapa hapa nchini. Kukiwa na uhitaji wa kuuza nje tutauza kwa bei ya juu mno.

4. Kukomesha tabia ya uonevu, kuanzia jeshi la polisi mpaka idara ya usalama wa taifa; kwa kuongozwa na dhana kwamba hakuna mwenye hatimiliki ya nchi hii.

5. Kufumua idara ya usalama wa taifa.

Ni pamoja na kuajiri watu wenye IQ kubwa sana. Sio watu wenye IQ za chini, ambao hata ishu ndogondogo zinawashinda.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Mkuu unaweza kuanza na kuwa rais wa Kijiji chako kama ni rahisi hivyo.Talkin is cheap.
 
Mkuu unaweza kuanza na kuwa rais wa Kijiji chako kama ni rahisi hivyo.Talkin is cheap.
Cheap to the one who does not have a vision and mission, brother. Kindly understand that there are people out there who have got a taste of wine and who don't know what it the wine itself.

Sent from my SM-G998B using JamiiForums mobile app
 
Freemasons na Illuminati watakuua au watafanya mapinduzi kwako maana naona umeingilia sera Yao mojawapo.
 
Nchi hii inarasilimali zakutosha kabisa na Mungu ameibaliki vyakutosha.

1. Barabara zote zakata,harimashauli au wilaya zitajengwa kwa Lami..kuwezesha usafirishaji.

2. Mijadara ya kisenge Bungeni nitamulu ikome..mf.mambo ya Vumbi la Kongo upuuzi kabisa lastly mtu anapata laki 4 nakitu per day.

3. Kilimo na Ufugaji ungekua ndo mkombozi wa maisha ya raia wangu.Bei za mazao zingeenda juu eg.korosho,mpunga,pamba ,mahindi etc, mambo ya kufunga mipata visititoke Sela yakimaskini sana na haisaidii wakulima. Mtu analazimika kuuza mpunga gunia 10 kwa shida ya laki 5 wakati angeuza mbili tu kwa bei nzuri.

4. Usalama na Haki kwa raia wangu ndo ingeligeuka misingi ya utawala wangu.Akijichanganya mwehu kutukana serikali ningemnyosha fast pasipo kumuua...lkn panya road,jambazi ningeamuru polisi wakiwa na ushahidi waue.

5. Madini yangenufaisha sana nchi yangu, mikataba yote ningeifumua.Nchi inaexport millions of Gold and Diamond Tazanite tones lkn masikini nisingekubali.

6. Ningepunguza matumizi ya Serikali sana. Mambo ya Naibu PM na wakuu wa wilaya ningefuta nafasi hizo hazina maana,wabunge ningepunguza posho laki per day na mishahara yao.Pia Mimi Rais ningepokea Ml5 tu! Na pasinge kua na mtu serikalini mwenye Zaid ya Ml5.

7. Uwazi na uwajibikaji kwangu na watumishi wote. Rushwa mtu akithibitika ni kunyongwa au jela maisha.

8. Jeshi lingeimalika na kuwana silaha za kisasa,hii ingeenda sambamba na kurecluti wanajeshi wapya wenye Elimu nzuri sio FM 4 failures.

9. Technology, Raia mwenye ubunifu na kipaji chochote angelelewa na kufanywa kukuza kipaji chake kwa manufaa yaan Taifa. Wasomi wengi ningepeleka nje kusoma technology mbalimbali na pia Matibabu.

10. Michezo,Raia wangeishi kwa furaha sana maana Soka lingekua Bora. Kila Mkoa ningejenga Akademi za soka...Hususani Ukanda wa Kaskazini na Kanda yote ya ziwa kutokana na advantage ya maumbo ya watu wa Ukanda huo makubwa wangenifaa kk wenye soka sana...mf Misukuma milefu sana likikaa beki au Forward mbona Drogba kabisa au Halland.

11.Mambo haya ya kuchagua viongozi wale wale au mtoto wa nani ningekomesha. Yaaan Mimi Kijana makini aliyemaliza SAUT/UD Nampa cheo Cha RC pasibo kujali kunamtoto wa Makamba.

12. Utali na Bandari,maeneo haya mhimu sana kiuchumi. Huwa sielewi kabisa kwanini utalii wetu hautunufaishi sana.....kooo ningeutangaza utalii haswaa. Hebu fikilia Rwanda jezi za Arsenal zimeandikwa Visit Rwanda,sisi tunakwama wapi kubuni namna ya kuutangaza utalii wetu. Bandari ingeleta mchangi mkubwa sana kwenye uchumi wetu....kikubwa hapo nisingecheka na kima wizi, Rushwa kukwepa Kodi adhabu yake ingelikua either kifo au jela maisha. Ikiniwia! ngumu ningeweka wanajeshi walinde!

NB: Nchi yangu Mungu kaipendelea sana, mifumo ya kuiongoza ndo mibovu na sera za nchi.Mfano Kila Rais akiingia huanza vipaombele vyake pasipo kujali alietoka alifanikiwa wapi na alishindwa kipi na kifanyike Nini kuifanikisha. Kwa kutambua hili ningetunga Sheria Kali za kuhakikisha ajaye anakamilisha miladi na malengo ya nchi yetu.

Hata hivyo nisingekubali kutoka Madarakani pasipokukamilisha malengo haya kwa Taifa langu, mpaka nifikishe Miaka 80, watu wa democrasia hamtanielewa ila ningefanya kuliokoa Taifa na umaskini.
 
Nitafutilia mbali wale wajinga wajinga, wanaojiita machawa..
 
Kuwa Rais Haina maana kwamba mawazo Yako ndio yataendesha Nchi, ukilazimisha utaishia kuwa Rais diktetea, kuwa Bunge, kuwa Mahakama, kuwa IGP yaanykuwa Kila kitu.

Mpaka hapo umeshafeli, Nchi sio familia.
 

Watanzania wengi hawajaridhika Mkataba wa Bandari, tusahihishe ama tuache kabisa~JB​

 
Kama mtu anakutwa na VAZI linalosemekana ni la Jeshi, ni mahakama pekee, ndio yenye mamlaka kuamua vazi hilo ni la Jeshi au la. JWTZ hawana mamlaka KUTAIFISHA vazi (mali) ya raia pasipo IDHINI ya sheria. Kama mtu amekutwa na vazi ya aina hiyo, sheria inataka utaratibu ufuatwe.

Kama mtu huyo anaaminika kutenda kosa, basi sheria inataka akamatwe, afunguliwe mashtaka kisha mahakama itamke wazi kuwa mtu huyo amekosa au la. Mahakama ndio hutoa adhabu kwa mkosaji au kutoa amri ya KUTAIFISHA mali na si JWTZ ama Jeshi la Polisi.

Angalizo:
Ni jambo gumu mno KUTHIBITISHA mahakamani vazi la Jeshi, hata kama yanafanana vipi na vazi RASMI! Kuna VIELELEZO vinavyotofautisha vazi rasmi kati ya Majeshi ya nchi moja na nchi nyingine. Vielelezo hivyo ni lazima viwepo kwenye vazi lenyewe ili lifanane na vazi la Jeshi.

Lakini, ufanano si wa mwonekano tu! Ukisoma sheria za PENAL CODE, The National Defence Act, 1966 & National Security Act, zote nimeeleza vyema. Kuna "key words" zimetumika kwenye sheria ili kusaidia utambuzi wa mavazi RASMI ya Jeshi.

Sio kwa namna ambavyo wengi wenu mnaaminishwa! Ni vyema sana sheria zikasomwa na KUELEWEKA vizuri. JW kisiwe chombo cha kuleta taharuki kwa raia. Mwisho, mahakama & sheria za nchi hii haziwezi kumkuta mtu na hatia endapo atakutwa na vazi RASMI la Jeshi la nchi nyingine.

Sheria ya Tanzania, inalinda "VAZI RASMI" & "SINAZOFANANA NA VAZI RASMI" tu. Hapa "zinazofanana" ndio imekuwa KIZUNGUMKUTI kueleweka JWTZ au labda wameamua KUPUUZA tu! Hili neno "zinazofanana" lina maana TOFAUTI kabisa na wanachowaambia raia. Sheria zisomwe vyema, zieleweke.

#BabaMwita
20230910_053539.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais unayejikita sana kwenye maadili utafeli asubuhi subuhi. Acha watu wapotoke kimaadili kadri wanavyotaka, wewe wanakuhusu nini?
 
Hii ndiyo ile kauli ya baadhi ya watu wanaosema nikiwa mkubwa Nita save asilimia 50 ya kipato na baada ya miaka 10 anahisi atatoboa.Haya sasa umekuwa mkubwa toa majibu.
 
Back
Top Bottom