Pita yote usiachie nusu tafadhali.
100. Kutoa motisha kwa vijana kwa kila namna inayowezekana kupenda mambo ya msingi. Hii itawezesha kuwafanya wapende kujihusisha na ubunifu, uzalendo, kujitegemea, kutoa mchango mkubwa kwa taifa lao. Sio kama hali ilivyo sasa wengi wao wanatamani na kujitahidi sana kuwa uchi mtandaoni, wanatumia muda mwingi kubeti na kucheza upatu kama vile biko na kadhalika.
101. Nitaweka sheria kali dhidi ya maadili na utamaduni bora kwa kila rika. Mfano kwasasa watoto wadogo wanapata mimba zisizokusudiwa na wanatelekezwa kinapatika kizazi kisichokuwa na malezi bora na hatimae taifa lenye watu wasiojitambua wala kujua maadili na misingi ya maisha yao kama watanzania. Sheria ya ndoa itaboreshwa na kuwekewa meno makali kiasi kwamba itadumisha utamaduni wa kuwa na famili bora na sio bora familia. Taifa linaanza na familia zenye upendo na amani.
200. Nitafuta sheria zote zinazomkandamiza mtanzania mwenye nia ya kujiinua kiuchumi. kuna sheria nyingi zipo ambazo zinawanyima wazao hususani vijana fursa nyingi na kusababisha mikopo yote tunayopata kutoka kwa wadau wa maendeleo kuchoropokea china.
201. Nitaweka ukomo wa kushika madaraka ya kisiasa kwa kila nyanja kuanzia kitongoji hadi taifa kwa ujumla, sio mtu huyo huyo kuanzai nyerere hadi samia anatuongoza na mawazo yale yale.
300 Nitaanzisha kitengo mahususi na chenye utalaamu wa hali ya juu cha kushauri na kutoa maamuzi ya mwisho kuhusu mustakabali wa maendeleo ya nchi. Sio kama ilivyosasa kundi la watu wengi wasiojua dunia inaelekea wapi wanakusanyika kwenye jengo linaitwa bunge na kuchambana kisha kulipwa na kurudi majumbani mwao. Kitengo hiki kitakuwa na watu wachache na wenye uchungu an uzalendo wa hali ya juu katika kupeleka nchi mbele kimaendelo.
301. Nitahakikisha naipatia nchi mahakama yenye nguvu kuliko mtu binafsi au taasisi yeyote ile kwenye nchi. Haki ni moja ya mambo ya msingi kwenye kupata maendeleo. Nitaweka mfumo ambao hataruhusu kamwe kutokea kwa rushwa kwenye eneo hili. Sheria kali na taasisi za kuchunguza utendaji wa mahakama zetu zitaimarika maradufu hadi watendaji kazi katika mahakama wafikirie mara mbili mbili kula rushwa.
400. Nitaweka mfumo mgumu mnoo wa kuwachuja viongozi wetu. Itampsa mtu yeyote anaetaka kuwa kiongozi awe mtu sahihi na mwenye uzalendo na usafi wa hali ya juu Kuanzia aipoanza maisha yake hapa duniani hadi alipo sasa na hiii sio tu kwamba itakuwa kigezo pekee bali vigezo vingi ili tuwapte viongozi wenye ndoto na uwezo wa kizitimiza ndoto zao.
401. Nitaisuka tume ya uchaguzi ambayo sio tu kwamba itakuwa huru bali itakuwa tume yenye uwazi kwa 100%. Uhuru wa tume hautoshi bali tume yenye uwazi kwa silimia zote ndio tume yenye kutupa viongozi tunawataka.
500. Uchaguzi utafanyika kwa uwazi kuliko hata bidhaa zinazouwa kando ya barabara. Yanani mtu akipita amepita kwa haki na takaekosa atakosa kwa haki.
501. Mwisho kabisa nitaweka uzio na mbwa wakali kwenye suala zima la maadili kama watanzania wenye nia ya kusonga mbele kwa heshima, maadili mazuri, na yenye kuleta tija katika tafia. kwasas maadili mabovu yametawala sana sio tu kwa wanawake hata kwa wanaume. Watanzania kwasasa wanashabikia na kuubariki uhuuni na uzandiki kuliko kushabikia mambo yenye tija kwa uzao waa ujao.