Siku kesi ya Lissu nashauri anaenda mahakama ya Kisutu aende na vitambulisho vya NIDA sababu kesi inahusu mambo ya ndani ya nchi

Shotocan

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2023
Posts
9,938
Reaction score
15,987
Siku kesi ya Lissu ikiletwa mahakama ya Kisutu wahudhuriaji waende na vitambulisho vya taifa vya NIDA sababu hiyo kesi inahusu mambo ya ndani ya nchi. Wahudhuruaji lazima wawe watanzania sio wageni.

Na wahakikiwe kwa madole kwenye mashine kama hivyo vitambulisho vyao

Hiyo itazuia watu wa nje kuhangaika na mambo yetu ya ndani ya nchi

Asiyeenda na kitambulisho cha NIDA asiruhusiwe kuingia getini
 
Siku kesi ya Lisu ikiletwa mahakama ya Kisutu wahudhuriaji waende na vitambulisho vya taifa vya NIDA sababu hiyo kesi inahusu mambo ya ndani ya nchi .Wahudhuruaji lazima wawe watanzania sio wageni.

Kuweka sharti la NIDA pekee kwa wahudhuriaji wa kesi ya Lissu ni kuvuruga misingi ya haki za kikatiba. Mahakama ni taasisi ya umma, si klabu ya watu wenye kadi. Haki ya kushuhudia mashauri ya wazi ni ya kila mtu mwenye sababu halali, iwe ni raia au mgeni aliyeidhinishwa kisheria. NIDA haipaswi kuwa kigezo cha kupima uzalendo wala uhalali wa kuwepo mahakamani.

Zaidi ya Watanzania, kuna mabalozi, waandishi na mashirika ya haki yanayofuata mchakato huu. Kuwazuia kwa hoja ya "masuala ya ndani" ni dalili ya hofu ya ukweli. Kesi safi haifichwi. Taifa imara hujenga imani kwa uwazi, si kwa ukiritimba wa mashine za vidole getini. Haki haipaswi kuchujwa kwa masharti ya vitambulisho.
 
Siku kesi ya Lisu ikiletwa mahakama ya Kisutu wahudhuriaji waende na vitambulisho vya taifa vya NIDA sababu hiyo kesi inahusu mambo ya ndani ya nchi .Wahudhuruaji lazima wawe watanzania sio wageni.

Na wahakikiwe kwa madole kwenye mashine kama hivyo vitambulisho vyao

Hiyo itazuia watu wa nje kuhangaika na mambo yetu ya ndani ya nchi
Asiyeenda na kitambulisho cha NIDA asiruhusiwe kuingia getini
Tusubili siku ukipata changamoto wakili wako awe mchina, kikikiki

Swali fikirishi je watu wote wana vitambulisho vya NIDA?
 
Ujinga ni mwingi sana kwenye mifumo yetu sheria.

Mihimili inaelekezwa nini cha kufanya, kufuata na hata kuamua.
 
wageni halali wapatiwe utaratibu mbadala wa utambulisho kama pasipoti na kibali maalum kutoka Wizara ya Mambo ya Nje.
Naunga mkono hili wageni wa nje wapate clearance kutoka wizara ya mambo ya nje kwanza

Na ipeleke nakala za clearance kwa mahakama .ikitaja majina yao ,nchi watokako na passport copy zao kuwa wameruhusiwa kuhudhuria kesi
 
buku 7,000/= zimefifisha uwezo wa baadhi ya vijana kufikiri sawasawa.
 
Tusubili siku ukipata changamoto wakili wako awe mchina, kikikiki

Swali fikirishi je watu wote wana vitambulisho vya NIDA?
Mahakama za kesi za ndani ya Tanzania sio the Hague kwenye Mahakama ya kimataifa
Hizi zetu ni local courts mchina wakili wa nini?
 
Siku kesi ya Lisu ikiletwa mahakama ya Kisutu wahudhuriaji waende na vitambulisho vya taifa vya NIDA sababu hiyo kesi inahusu mambo ya ndani ya nchi .Wahudhuruaji lazima wawe watanzania sio wageni.

Na wahakikiwe kwa madole kwenye mashine kama hivyo vitambulisho vyao

Hiyo itazuia watu wa nje kuhangaika na mambo yetu ya ndani ya nchi

Asiyeenda na kitambulisho cha NIDA asiruhusiwe kuingia getini
Kuingia Mahakamani mwongozi u atolewa ba Mahakama. Hakuna kwenye maamuzi ya Mahakama ikisema watu waingie na vitambulisho.
 
Watu wengi wanaokagua Uraia wa Watanzania sio Watanzania na wazawa wanasumbuliwa kweli kupata hata hati za kusafiria kuliko wageni nadhani hapa utakua umenielewa..
 
Kuingia Mahakamani mwongozi u atolewa ba Mahakama. Hakuna kwenye maamuzi ya Mahakama ikisema watu waingie na vitambulisho.
Ndio maana nimesema nashauri
Mahakama sio choo ambacho raia yeyote wa nje aweza amua kwenda akijisikia
 
Siku kesi ya Lisu ikiletwa mahakama ya Kisutu wahudhuriaji waende na vitambulisho vya taifa vya NIDA sababu hiyo kesi inahusu mambo ya ndani ya nchi .Wahudhuruaji lazima wawe watanzania sio wageni.

Na wahakikiwe kwa madole kwenye mashine kama hivyo vitambulisho vyao

Hiyo itazuia watu wa nje kuhangaika na mambo yetu ya ndani ya nchi

Asiyeenda na kitambulisho cha NIDA asiruhusiwe kuingia getini
Kijana kasome historia unajua mwalimu nyerere ameingilia mamlaka za nchi ngapi kipindi zinatafuta uhuru kipindi hicho mpaka wengine tuliwahifadhi nchini kwetu halafu nyinyi mnafanya maovu halafu mnataka majirani wasiingilie nenda ukasome historia uone Tanzania imeingilia nchi ngapi kwenye maamuzi.
 
Huko shuleni mnasomea ujinga?

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, haki ya kusikilizwa mahakamani ni haki ya kikatiba (Ibara ya 13(6)(a)).

Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), Sura ya 20, haijaweka sharti kuwa wasikilizaji lazima waonyeshe kitambulisho cha NIDA kuhudhuria kesi.
 
Kijana kasome historia unajua mwalimu nyerere ameingilia mamlaka za nchi ngapi kipindi zinatafuta uhuru kipindi hicho mpaka wengine tuliwahifadhi nchini kwetu halafu nyinyi mnafanya maovu halafu mnataka majirani wasiingilie nenda ukasome historia uone Tanzania imeingilia nchi ngapi kwenye maamuzi.
Nterere Aliingilia hizo nchi sababu walikuwa wakishambulia Tanzania mipaka ya kusini

Makaburu na wareno walisumbua sana mipaka yetu ndio maana akaamua kupeleka majeshi ya Tanzania kupambana nao nchi zote za kusini mwa Afrika waziachie washike waafrika Tanzania tupate amani

Sisi Tanzania sio tishio kwa Kenya kiusalama hao mabwege wanaharakati wa Kenya sio kama Nyerere huwezi walinganisha na Nyerere
 
Siku kesi ya Lisu ikiletwa mahakama ya Kisutu wahudhuriaji waende na vitambulisho vya taifa vya NIDA sababu hiyo kesi inahusu mambo ya ndani ya nchi .Wahudhuruaji lazima wawe watanzania sio wageni.

Na wahakikiwe kwa madole kwenye mashine kama hivyo vitambulisho vyao

Hiyo itazuia watu wa nje kuhangaika na mambo yetu ya ndani ya nchi

Asiyeenda na kitambulisho cha NIDA asiruhusiwe kuingia getini
Think tank kama think tank.
 
Back
Top Bottom