Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SIKU MOJA NA AHMED RAJAB MWALIMU WANGU NAIROBI
Ahmed Rajab akinipa kazi si haba nyingine ''investigative'' na hapa akitaka sana kusoma ubongo wangu na fikra zangu kwa jambo fulani hizo hazichapwi na jina si lake wala langu kwa hiyo hutoziona popote na akinilipa fedha.
Makala hizi hazina byline.
Ila siku moja nikaona makala katika Economist.
Jarida hili likichapwa Marekani.
Siku hizi majarida haya kama Newsweek na Time hayapo tena sijui mtandaoni.
Hii makala ya Economist sikupata tabu kujua kuwa ile ni kalamu yangu.
Kichwa kikanivimba.
Ahmed alikuwa mtu.
Wala yeye hakuniambia kuwa makala ipo mahali fulani.
Nadhani hizo ndizo zilikuwa sheria za mchezo wenyewe.
Ahmed Rajab akanifunza kuwa mbahili wa maneno katika kuandikia majarida fulani fulani mfano wa jarida lake Africa Analysis.
Nikimwonyesha makala anasema, ''Mohamed futa hii, futa hii, futa hii.
Haya yote weka sentensi moja.
Unawaandikia watu maalum na unawapa ujumbe maalum wao wakisoma sentensi moja wameshaelewa kila kitu.''
Siku moja kaja Nairobi akitokea Lagos.
Tukakutana kwa rafiki yetu mmoja Muthaiga.
Siku hii naikumbuka sana nilikuwa nimekwenda kuwafata wanangu wamefunga shule.
Tukazungumza sana kwani muda mrefu tulikuwa hatujaonana.
Ghafla akafungua mkoba wake, ''Mohamed kuna fedha unanidai na zipo hapa ngoja nikupe."
Ahmed Rajab akaingiza mkono mkobani akatoa bunda la noti za kila aina, Naira, USD, Sterling Pound...
Ahmed Rajab anajua Watanzania fedha gani tunapenda.
Akanikatia kibunda akanikabidhi.
Fedha nyingi kuliko kazi niliyofanya ya kuandika, ''Sentensi moja inatosha.''
Hii picha nilimpiga siku hiyo.