Siku Moja na Mwalimu Wangu Ahmed Rajab Nairobi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SIKU MOJA NA AHMED RAJAB MWALIMU WANGU NAIROBI

Ahmed Rajab akinipa kazi si haba nyingine ''investigative'' na hapa akitaka sana kusoma ubongo wangu na fikra zangu kwa jambo fulani hizo hazichapwi na jina si lake wala langu kwa hiyo hutoziona popote na akinilipa fedha.

Makala hizi hazina byline.
Ila siku moja nikaona makala katika Economist.

Jarida hili likichapwa Marekani.
Siku hizi majarida haya kama Newsweek na Time hayapo tena sijui mtandaoni.

Hii makala ya Economist sikupata tabu kujua kuwa ile ni kalamu yangu.

Kichwa kikanivimba.
Ahmed alikuwa mtu.

Wala yeye hakuniambia kuwa makala ipo mahali fulani.
Nadhani hizo ndizo zilikuwa sheria za mchezo wenyewe.

Ahmed Rajab akanifunza kuwa mbahili wa maneno katika kuandikia majarida fulani fulani mfano wa jarida lake Africa Analysis.

Nikimwonyesha makala anasema, ''Mohamed futa hii, futa hii, futa hii.
Haya yote weka sentensi moja.

Unawaandikia watu maalum na unawapa ujumbe maalum wao wakisoma sentensi moja wameshaelewa kila kitu.''

Siku moja kaja Nairobi akitokea Lagos.
Tukakutana kwa rafiki yetu mmoja Muthaiga.

Siku hii naikumbuka sana nilikuwa nimekwenda kuwafata wanangu wamefunga shule.
Tukazungumza sana kwani muda mrefu tulikuwa hatujaonana.

Ghafla akafungua mkoba wake, ''Mohamed kuna fedha unanidai na zipo hapa ngoja nikupe."
Ahmed Rajab akaingiza mkono mkobani akatoa bunda la noti za kila aina, Naira, USD, Sterling Pound...

Ahmed Rajab anajua Watanzania fedha gani tunapenda.
Akanikatia kibunda akanikabidhi.

Fedha nyingi kuliko kazi niliyofanya ya kuandika, ''Sentensi moja inatosha.''

1739542939579.jpeg

Hii picha nilimpiga siku hiyo.
 
Pole sana Kaka, kumpoteza swahiba wako.
Vipi ulikwenda London kumsindikiza?
 
pole father(uzee unaukataaga)

nawaza hapa atakuandika nani hapa JF mana bado hatujakufahamu au unakitabu umejiandika
 
Kina Kirefu,
Itakuwa kufru kwangu mimi kukataa umri wangu.
Umri mrefu ni zawadi kutoka kwa Allah.

Angependa angenichukua katika ujana wangu kwani wenzangu wengi wametangulia.

Ila wewe ukiinta mimi babu yako nakueleza kuwa hapana si sawa wewe ni mwanangu wa kuniita ''babu'' ni wanao.

Ama hilo la taazia yangu subiri nife In Shaa Allah utawaona hao watakaoniandika.

Nimeufaidi ujana wangu nikizunguka dunia hii na kuingia katika maduka makubwa kufanya shopping ya nguo nk.

Alhamdulillah.
Niangalie hapo chini:

1739543245383.jpeg

Grande Mosque, Paris 1993
 
View attachment 3236410
Grande Mosque, Paris 1993
nimekupata father kwann NYERERE aliwatuma sana ulaya huko ila tuntemeke sanga na kambona wawili tu wakaamua kumchana NYERERE juu ya ubovu wa ujamaa au nyie ilikuwa kupiga Hela za taifa
 
Sikutumwa na Nyerere wala sikula fedha za serikali.
Ukiwa unataka kunijua niulize nitakufahamisha.

Katika maisha yangu sina cha kuficha ndiyo maana
unaniona hapa natumia jina langu halisi na nipo kwa picha na sauti.

Wewe umejificha.
Kipi kinakutisha?
 
Mzee mood

sio naogopa kanuni za JF zinaruhusu kutumia jina kivuli

mwaka huu taaluma yako hiyo NAMI nikaisome mana naona wajinga wengi kweli tofauti na mlivyokuwa nyie
tumuenzi ahamed rajab...NAMI uje uaze kuniambia futa haya maneno
 
Kina...
Mimi siko hapa kutaniana na yeyote awae yule.

Nakuomba tafadhali usiniite Mzee Mood.
Nakusihi niwekee staha.
 
Kina Kirefu,
Itakuwa kufru kwangu mimi kukataa umri wangu.
Umri mrefu ni zawadi kutoka kwa Allah.

Angependa angenichukua katika ujana wangu kwani wenzangu wengi wametangulia.

Ila wewe ukiinta mimi babu yako nakueleza kuwa hapana si sawa wewe ni mwanangu wa kuniita ''babu'' ni wanao.

Ama hilo la taazia yangu subiri nife In Shaa Allah utawaona hao watakaoniandika.

Nimeufaidi ujana wangu nikizunguka dunia hii na kuingia katika maduka makubwa kufanya shopping ya nguo nk.

Alhamdulillah.
Niangalie hapo chini:

View attachment 3236410
Grande Mosque, Paris 1993
Mkuu,
Hapo msikitini wanaruhusu kuingia na viatu?
 
Gagmija,
Ndani ya msikiti panaposali watu lazima kuvua viatu lakini nje ya msikiti unavaa viatu.

Hii ilikuwa 1993.

In Shaa Allah nitakuwekea picha nyingine ya 2011 nipo msikiti huo huo tuko waumini wengi nje ya msikiti tumevaa viatu.

1739736193803.jpeg
 
SIKU MOJA NA AHMED RAJAB MWALIMU WANGU NAIROBI

Ahmed Rajab akinipa kazi si haba nyingine ''investigative'' na hapa akitaka sana kusoma ubongo wangu na fikra zangu kwa jambo fulani hizo hazichapwi na jina si lake wala langu kwa hiyo hutoziona popote na akinilipa fedha.

Makala hizi hazina byline.
Ila siku moja nikaona makala katika Economist.

Jarida hili likichapwa Marekani.
Siku hizi majarida haya kama Newsweek na Time hayapo tena sijui mtandaoni.

Hii makala ya Economist sikupata tabu kujua kuwa ile ni kalamu yangu.

Kichwa kikanivimba.
Ahmed alikuwa mtu.

Wala yeye hakuniambia kuwa makala ipo mahali fulani.
Nadhani hizo ndizo zilikuwa sheria za mchezo wenyewe.

Ahmed Rajab akanifunza kuwa mbahili wa maneno katika kuandikia majarida fulani fulani mfano wa jarida lake Africa Analysis.

Nikimwonyesha makala anasema, ''Mohamed futa hii, futa hii, futa hii.
Haya yote weka sentensi moja.

Unawaandikia watu maalum na unawapa ujumbe maalum wao wakisoma sentensi moja wameshaelewa kila kitu.''

Siku moja kaja Nairobi akitokea Lagos.
Tukakutana kwa rafiki yetu mmoja Muthaiga.

Siku hii naikumbuka sana nilikuwa nimekwenda kuwafata wanangu wamefunga shule.
Tukazungumza sana kwani muda mrefu tulikuwa hatujaonana.

Ghafla akafungua mkoba wake, ''Mohamed kuna fedha unanidai na zipo hapa ngoja nikupe."
Ahmed Rajab akaingiza mkono mkobani akatoa bunda la noti za kila aina, Naira, USD, Sterling Pound...

Ahmed Rajab anajua Watanzania fedha gani tunapenda.
Akanikatia kibunda akanikabidhi.

Fedha nyingi kuliko kazi niliyofanya ya kuandika, ''Sentensi moja inatosha.''

View attachment 3236403
Hii picha nilimpiga siku hiyo.
Mkuu Mohamed pole tena, naona bado ulikuwa unataka kuandika zaidi kuhusu Ahmed lakini kwa majonzi makubwa ukaamua kuacha. Anyway naona ukitulia utaandika zaidi kuhusu huyu nguli
 
Kina Kirefu,
Itakuwa kufru kwangu mimi kukataa umri wangu.
Umri mrefu ni zawadi kutoka kwa Allah.

Angependa angenichukua katika ujana wangu kwani wenzangu wengi wametangulia.

Ila wewe ukiinta mimi babu yako nakueleza kuwa hapana si sawa wewe ni mwanangu wa kuniita ''babu'' ni wanao.

Ama hilo la taazia yangu subiri nife In Shaa Allah utawaona hao watakaoniandika.

Nimeufaidi ujana wangu nikizunguka dunia hii na kuingia katika maduka makubwa kufanya shopping ya nguo nk.

Alhamdulillah.
Niangalie hapo chini:

View attachment 3236410
Grande Mosque, Paris 1993
Mzee Said, enzi za ujana wako ulikuwa mnyamwezi kweli kweli.
 
Back
Top Bottom