Siku moja na Sheikh Ponda Mahakamani Morogoro 2015

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SIKU MOJA NA SHEIKH PONDA MAHAKAMANI MOROGORO

Miaka saba iliyopita siku kama ya leo.

Siku nyingi zilikuwa zimepita sijamuona Sheikh Ponda si kwa kuwa alikuwa kifungoni mahabusi bali nilikuwa nje ya Dar es Salaam kwa muda mrefu.

Nikaamua kwenda kumuona mahakamani Morogoro kesi yake ilipokuwa inasikilizwa.

Nikapanda basi la kwanza ili niwahi mahakamani Morogoro.

Kufikia mahakamani nikakuta ulinzi mkali kupita kawaida na kisa ni kuwa kabla sijafika Waislam walikuwa wametiana misukosuko na polisi nje ya jengo la mahakama.

Kwa ajili hii polisi wakawa wamewazuia Waislam kuingia mahakamani.

Baadhi ya watu wanaonifahamu kuniona nimefika pale wakanifuata kunisalimia na kunifahamisha yaliyotokea pale punde wakisikitika kuwa nimekuja kutoka mbali lakini sitaweza kusalimiana na Sheikh Ponda.

Hata hivyo wakanishauri kwenda pale getini nizungumze na askari huenda akaniruhusu kuingia mahakamani kusikiliza kesi na kupata nafasi ya kuonana na Sheikh Ponda.

Baada ya kunisaili yule askari akaniruhusu kupita akiniambia kuwa amefanya staha ya umri wangu na kuwa ni ndugu yake sheikh na nimekuja kutoka mbali.

Mahakamani nilimkuta Mzee Bilal Rehani Waikela katoka Tabora kaja Morogoro kusikiliza kesi ya Sheikh Ponda.

Ilikuwa hapo Morogoro miaka mitatun iliyopita asubuhi najitayarisha kwenda studio za Radio Imaan kufanya kipindi ndipo niliposikia katika taarifa ya habari kuwa Sheikh Ponda amekwenda kwenye kiwanja cha iliyokuwa EAMWS kiwanja palipokusudiwa kujengwa Chuo Kikuu Cha Waislam mwaka wa 1968 na amechukua sehemu ndogo kurejesha kwa Waislam na patajengwa msikiti utakaoitwa Masjid Sheikh Hassan bin Ameir.

Yaliyomfika Sheikh Ponda yanafahamika.

Kumuona Mzee Waikela ndani ya mahakama na Sheikh Ponda kasimama kizimbani machozi yalinilengalenga.

Machozi yalinitoka kwa kuwa nilikuwa naijua nafasi ya Mzee Waikela na Sheikh Hassan bin Ameir katika historia ya Tanganyika.

Miaka mingi imepita toka watu hawa walipokuwa pamoja kama viongozi wa Waislam katika EAMWS.

Lakini niliingiwa na simanzi na kumuonea wivu Sheikh Ponda kuwa leo jina lake linatajwa pamoja na jina la Sheikh Hassan bin Ameir na mwanafunzi wa Sheikh Hassan bin Ameir, Mzee Waikela yuko mahakamani kusikiliza kesi yake.

Sheikh Ponda aliposhinda kesi zote alinialika kwenye shule ambayo yeye ni kiongozi, Ilala Islamic nimzungumze na vijana kuhusu mchango wa Sheikh Hassan bin Ameir katika elimu na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Sheikh Ponda ana historia kubwa sana
Naamini iko siku In Shaa Allah atanyanyua kalamu kuiandika.

1641386114877.png

Kulia ni Wakili Msomi Juma Nassor na Sheikh Ponda Mahakamani Morogoro

1641386315783.png

Kushoto wa kwanza ni Mzee Bilal Rehani Waikela akiwa mahakamani Morogoro
 
Ahsante kwa hii briefing mzee Mo

Huwa napenda sana lafudhi ya Alwatan wetu, Sheikh Ponda.

Namna huwa anaongea kwa utaratibu na intonations maridhawa katika kujenga hoja.
 
View attachment 2069458
Kulia ni Wakili Msomi Juma Nassor na Sheikh Ponda Mahakamani Morogoro

View attachment 2069462
Kushoto wa kwanza ni Mzee Bilal Rehani Waikela akiwa
mahakamani Morogoro

Mzee Mohamed Said Shikamoo. Je Mzee hao waliokuwa mahakamani walivaa Label au walikuwa na alama gani kujua kwamba ndani yake huyu ni mwislamu, Mkristo, Kafiri au hana dini??
Ahsante
 
Shukraani mzee Mo
Allah awahifadhi na kuwa yalo mema hawa wazee wetu
 
SIKU MOJA NA SHEIKH PONDA MAHAKAMANI MOROGORO

Miaka saba iliyopita siku kama ya leo.

Siku nyingi zilikuwa zimepita sijamuona Sheikh Ponda si kwa kuwa alikuwa kifungoni mahabusi bali nilikuwa nje ya Dar es Salaam kwa muda mrefu.

Nikaamua kwenda kumuona mahakamani Morogoro kesi yake ilipokuwa inasikilizwa.

Nikapanda basi la kwanza ili niwahi mahakamani Morogoro.

Kufikia mahakamani nikakuta ulinzi mkali kupita kawaida na kisa ni kuwa kabla sijafika Waislam walikuwa wametiana misukosuko na polisi nje ya jengo la mahakama.

Kwa ajili hii polisi wakawa wamewazuia Waislam kuingia mahakamani.

Baadhi ya watu wanaonifahamu kuniona nimefika pale wakanifuata kunisalimia na kunifahamisha yaliyotokea pale punde wakisikitika kuwa nimekuja kutoka mbali lakini sitaweza kusalimiana na Sheikh Ponda.

Hata hivyo wakanishauri kwenda pale getini nizungumze na askari huenda akaniruhusu kuingia mahakamani kusikiliza kesi na kupata nafasi ya kuonana na Sheikh Ponda.

Baada ya kunisaili yule askari akaniruhusu kupita akiniambia kuwa amefanya staha ya umri wangu na kuwa ni ndugu yake sheikh na nimekuja kutoka mbali.

Mahakamani nilimkuta Mzee Bilal Rehani Waikela katoka Tabora kaja Morogoro kusikiliza kesi ya Sheikh Ponda.

Ilikuwa hapo Morogoro miaka mitatun iliyopita asubuhi najitayarisha kwenda studio za Radio Imaan kufanya kipindi ndipo niliposikia katika taarifa ya habari kuwa Sheikh Ponda amekwenda kwenye kiwanja cha iliyokuwa EAMWS kiwanja palipokusudiwa kujengwa Chuo Kikuu Cha Waislam mwaka wa 1968 na amechukua sehemu ndogo kurejesha kwa Waislam na patajengwa msikiti utakaoitwa Masjid Sheikh Hassan bin Ameir.

Yaliyomfika Sheikh Ponda yanafahamika.

Kumuona Mzee Waikela ndani ya mahakama na Sheikh Ponda kasimama kizimbani machozi yalinilengalenga.

Machozi yalinitoka kwa kuwa nilikuwa naijua nafasi ya Mzee Waikela na Sheikh Hassan bin Ameir katika historia ya Tanganyika.

Miaka mingi imepita toka watu hawa walipokuwa pamoja kama viongozi wa Waislam katika EAMWS.

Lakini niliingiwa na simanzi na kumuonea wivu Sheikh Ponda kuwa leo jina lake linatajwa pamoja na jina la Sheikh Hassan bin Ameir na mwanafunzi wa Sheikh Hassan bin Ameir, Mzee Waikela yuko mahakamani kusikiliza kesi yake.

Sheikh Ponda aliposhinda kesi zote alinialika kwenye shule ambayo yeye ni kiongozi, Ilala Islamic nimzungumze na vijana kuhusu mchango wa Sheikh Hassan bin Ameir katika elimu na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Sheikh Ponda ana historia kubwa sana
Naamini iko siku In Shaa Allah atanyanyua kalamu kuiandika.

View attachment 2069458
Kulia ni Wakili Msomi Juma Nassor na Sheikh Ponda Mahakamani Morogoro

View attachment 2069462
Kushoto wa kwanza ni Mzee Bilal Rehani Waikela akiwa mahakamani Morogoro
Natamani kizazi hiki kiwe na waandishi wazuri wa matukio ya kukumbukwa, LAKINI Vijana hawaandiki na hata diary hawana.
 
Hivi hivyo vitu vya EAMWS vimeshindikana kurejeshwa? Wanavihodhi wanajisikiaje?
Cheche...
Hayo maneno hapo chini yatajibu swali lako na kukupa mengine yatakayokusaidia kuelewa mengine pia.

Haya nimeandika katika kitabu cha Abdul Sykes:

"Baada ya Sheikh Hassan bin Ameir kukamatwa, kurudishwa Zanzibar na kupigwa marufuku kuingia Tanganyika serikali ilisimamia uchaguzi wa kuundwa kwa BAKWATA.

Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.

Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama.

Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza.

Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali iiyokuwa inaongozwa na Julius Nyerere kuonekana inasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam.

Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kuchukua mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.

Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe.

Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoangukia katika mikono ya BAKWATA.

BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa.
 
Natamani kizazi hiki kiwe na waandishi wazuri wa matukio ya kukumbukwa, LAKINI Vijana hawaandiki na hata diary hawana.
Buji,
Ni wajibu wetu sisi wazazi wao kuwafunza watoto wetu faida za kusoma na kuandika.
Nakuwekea hapo chini kukurasa mmoja kutoka dairy yangu ya mwaka wa 1991.

1641439857908.png

Ahmed unayemasoma ni Ahmed Rajab, Babu ni Abdulrahman Babu, Mlamali ni Mohamed Mlamali Adam.
 
Asante sana kwakuendelea kutupa historia hususani mchango wa waislamu ktk kupigania uhuru wa nchi.
Hakuna asiyetambua nguvu kubwa ya waislam ktk kupata uhuru na hatimaye kuundwa serikali ya kizalendo.
Lkn ifike pahala waislam wakiongozwa na wazee kama nyie waache kulia lia. Yapo makundi mengi tofauti yaliporwa mali zao/nyadhifa/haki na serikali ya kizalenfo.

Wapo machifu waliolazimishwa kuacha milki na tawala zao wakabaki machiefu jina. Hawa machifu walikuwa na ardhi, majeshi, utawala na maamuzi, walikusanya kodi n.k, lkn kwa kuwa walielewa serikali ya kizalendo nini wakaacha vyote wakaunga mkono juhudi.

Zipo taasisi za kidini za kikristo, hizi zilihodhi karibia kila sekta ya huduma na uchumi, kuanzia mahospitali, mashamba, shule, vyuo, mifugo nk. Tena hawa ndio walifilisiwa kweli kweli lkn waliunga mkono juhudi na wakakubali kuanza upya.

Sasa shida ipo kwa waislam tena wachache sana wakiongozwa na wazee wenye mawazo mgando kuaminisha umma kama wameonewa kuliko makundi yawayo tanganyika.
Camon people let us be positive, to hell with these -ve thinkings
 
Asante sana kwakuendelea kutupa historia hususani mchango wa waislamu ktk kupigania uhuru wa nchi.
Hakuna asiyetambua nguvu kubwa ya waislam ktk kupata uhuru na hatimaye kuundwa serikali ya kizalendo.
Lkn ifike pahala waislam wakiongozwa na wazee kama nyie waache kulia lia. Yapo makundi mengi tofauti yaliporwa mali zao/nyadhifa/haki na serikali ya kizalenfo.

Wapo machifu waliolazimishwa kuacha milki na tawala zao wakabaki machiefu jina. Hawa machifu walikuwa na ardhi, majeshi, utawala na maamuzi, walikusanya kodi n.k, lkn kwa kuwa walielewa serikali ya kizalendo nini wakaacha vyote wakaunga mklno juhudi.

Zipo taasisi za kidini za kikristo, hizi zilihodhi karibia kila sekta ya huduma na uchumi, kuanzia mahospitali, mashamba, shule, vyuo, mifugo nk. Tena hawa ndio walifilisiwa kweli kweli lkn waliunga mkono juhudi na wakakubali kuanza upya.

Sasa shida ipo kwa waislam tena wachache sana wakiongozwa na wazee wenye mawaxo mgando kuaminisha umma kama wameonewa kuliko makundi yawayo tanganyika.
Camon people let us be positive
Kawoli,
Umechangia fikra na ni vizuri ila kwa hilo neno, ''kulialia.''

Lugha ya kejeli na kebehi huvuruga majadiliano kwani hukaribisha watu hodari wa lugha kama hizi na matokeo yake ni vurugu.

Hili neno halifai linaweza kuchukuliwa kama dharau.

Mimi nimeandika historia ya mali za Waislam baada ya kuulizwa swali kuhusu hizo mali,
Nimejibu swali.

Sikulia.
 
Kawoli,
Umechangia fikra na ni vizuri ila kwa hilo neno, ''kulialia.''

Lugha ya kejeli na kebehi huvuruga majadiliano kwani hukaribisha watu hodari wa lugha kama hizi na matokeo yake ni vurugu.

Hili neno halifai linaweza kuchukuliwa kama dharau.

Mimi nieandika historia ya mali za Waislam baada ya kuulizwa swali kuhusu hizo mali,
Nimejibu swali.

Sikulia.
Nisamehe mzee wangu. Nimekosea mimi, nimekosea sana, ndio mana naomba msamaha
 
Cheche...
Hayo maneno hapo chini yatajibu swali lako na kukupa mengine yatakayokusaidia kuelewa mengine pia.

Haya nimeandika katika kitabu cha Abdul Sykes:

"Baada ya Sheikh Hassan bin Ameir kukamatwa, kurudishwa Zanzibar na kupigwa marufuku kuingia Tanganyika serikali ilisimamia uchaguzi wa kuundwa kwa BAKWATA.

Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS.

Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama.

Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza.

Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali iiyokuwa inaongozwa na Julius Nyerere kuonekana inasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam.

Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kuchukua mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA.

Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe.

Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoangukia katika mikono ya BAKWATA.

BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa.
Aisee. Very sad. Ipo siku hilo dubwana lililoundwa na sirikali litaparaganyika na hatimaye uhalisia utatalamaki
 
Ilikuwa hapo Morogoro miaka mitatun iliyopita asubuhi najitayarisha kwenda studio za Radio Imaan kufanya kipindi ndipo niliposikia katika taarifa ya habari kuwa Sheikh Ponda amekwenda kwenye kiwanja cha iliyokuwa EAMWS kiwanja palipokusudiwa kujengwa Chuo Kikuu Cha Waislam mwaka wa 1968 na amechukua sehemu ndogo kurejesha kwa Waislam na patajengwa msikiti utakaoitwa Masjid Sheikh Hassan bin Ameir.
Pamoja na kumkubali sana Sheikh Ponda lakini jambo moja najiuliza, kiwanja cha kujenga chuo kikuu kinabadirishwa na kujengwa msikiti? Hivi Morogoro misikiti imejaa kiasi kwamba chuo kikuu kiwe hakina maana tena badala yake pajengwe msikiti? Hi inanifikirisha kidogo
 
SIKU MOJA NA SHEIKH PONDA MAHAKAMANI MOROGORO

Miaka saba iliyopita siku kama ya leo.

Siku nyingi zilikuwa zimepita sijamuona Sheikh Ponda si kwa kuwa alikuwa kifungoni mahabusi bali nilikuwa nje ya Dar es Salaam kwa muda mrefu.

Nikaamua kwenda kumuona mahakamani Morogoro kesi yake ilipokuwa inasikilizwa.

Nikapanda basi la kwanza ili niwahi mahakamani Morogoro.

Kufikia mahakamani nikakuta ulinzi mkali kupita kawaida na kisa ni kuwa kabla sijafika Waislam walikuwa wametiana misukosuko na polisi nje ya jengo la mahakama.

Kwa ajili hii polisi wakawa wamewazuia Waislam kuingia mahakamani.

Baadhi ya watu wanaonifahamu kuniona nimefika pale wakanifuata kunisalimia na kunifahamisha yaliyotokea pale punde wakisikitika kuwa nimekuja kutoka mbali lakini sitaweza kusalimiana na Sheikh Ponda.

Hata hivyo wakanishauri kwenda pale getini nizungumze na askari huenda akaniruhusu kuingia mahakamani kusikiliza kesi na kupata nafasi ya kuonana na Sheikh Ponda.

Baada ya kunisaili yule askari akaniruhusu kupita akiniambia kuwa amefanya staha ya umri wangu na kuwa ni ndugu yake sheikh na nimekuja kutoka mbali.

Mahakamani nilimkuta Mzee Bilal Rehani Waikela katoka Tabora kaja Morogoro kusikiliza kesi ya Sheikh Ponda.

Ilikuwa hapo Morogoro miaka mitatun iliyopita asubuhi najitayarisha kwenda studio za Radio Imaan kufanya kipindi ndipo niliposikia katika taarifa ya habari kuwa Sheikh Ponda amekwenda kwenye kiwanja cha iliyokuwa EAMWS kiwanja palipokusudiwa kujengwa Chuo Kikuu Cha Waislam mwaka wa 1968 na amechukua sehemu ndogo kurejesha kwa Waislam na patajengwa msikiti utakaoitwa Masjid Sheikh Hassan bin Ameir.

Yaliyomfika Sheikh Ponda yanafahamika.

Kumuona Mzee Waikela ndani ya mahakama na Sheikh Ponda kasimama kizimbani machozi yalinilengalenga.

Machozi yalinitoka kwa kuwa nilikuwa naijua nafasi ya Mzee Waikela na Sheikh Hassan bin Ameir katika historia ya Tanganyika.

Miaka mingi imepita toka watu hawa walipokuwa pamoja kama viongozi wa Waislam katika EAMWS.

Lakini niliingiwa na simanzi na kumuonea wivu Sheikh Ponda kuwa leo jina lake linatajwa pamoja na jina la Sheikh Hassan bin Ameir na mwanafunzi wa Sheikh Hassan bin Ameir, Mzee Waikela yuko mahakamani kusikiliza kesi yake.

Sheikh Ponda aliposhinda kesi zote alinialika kwenye shule ambayo yeye ni kiongozi, Ilala Islamic nimzungumze na vijana kuhusu mchango wa Sheikh Hassan bin Ameir katika elimu na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Sheikh Ponda ana historia kubwa sana
Naamini iko siku In Shaa Allah atanyanyua kalamu kuiandika.

View attachment 2069458
Kulia ni Wakili Msomi Juma Nassor na Sheikh Ponda Mahakamani Morogoro

View attachment 2069462
Kushoto wa kwanza ni Mzee Bilal Rehani Waikela akiwa mahakamani Morogoro
Mzee Said, hivi Mzee Waikela bado yupo hai? Mwamba sana huyu mzee..Namkumbuka alikuwa anakaa mtaan Ng'ambo au Kanyeye. Ni mzee anayeheshimika Sana na waislamu na wanaharakati. Ni mtu mwenye kauli thabiti! Huwezi taja uhuru wa Tanganyika bila kulitaja jina la huyu mzee ( hii ni kwa watu maalumu tu wanaojua mchango wake kwenye uhuru wa Tanganyika)
 
Back
Top Bottom