2011 nimefika kwa Kaka yangu namkuta anaumwa balaa..halafu mke wake yaan full ujuaji..ooh Kaka yako atakuwa karogwa na na yule Malaya wake ..ooh Mara hivi Mara vile..nikalala pale usiku sielewi elewi Kaka analia chumban mbavu zinabana halafu mke hajali...nikawagongea nikambeba bro had chumba changu..asubuhi nikaondoka nae nikasema akacheki hospital..ile tumetoka nje ya getini nikamwambia kaka tunaenda kigoma..Moja kwa Moja From kogamboni to Kigoma..huko mtaalamu akabaini mke ndo muhusika..bro akatibiwa kwa miezi miwili...akapona...
Huku nyuma Shem akaanza kulalamika nimemuiba mgonjwa hajui alipo mume wake..akalaani Sana..
Mtaalamu akaeleza uchawi uliofanyika shemeji akishirikiana na mama Yake mzaz walitumia mjusi mwenye mimba ambae walimpasua na kutoa kitoto Cha mjusi ambacho walikisaga na kuchanganya na dawa zingine wakamtilia kwenye chakula..ile kitu ikaenda ikafunga utumbo mpana na kusababisha vichomi..broo akawa hapati haha kubwa ..anakula lakn haendi chooni ....
To cut the story short broo alipona ila yule shemeji amepooza yuko kwao hapo kaskazin mwa Tanzania..