Siku Museveni Aliponusurika Kutekwa Nairobi

Siku Museveni Aliponusurika Kutekwa Nairobi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Bongo Hapo Zamani:

Siku Museveni Aliponusurika Kutekwa Nairobi..

Ndugu zangu,

Kuna matukio makubwa yalitokea sambamba na Vita Vya Kagera vilivyokuwa vikiendelea mwaka 1978.

Kwenye kitabu chake ' Sowing The Mustard Seed', Yoweri Museveni anasimulia tukio la kijasusi mlengwa akiwa ni yeye, Museveni.

Museveni alikuwa Nairobi kukutana na baadhi ya Waganda wanaharakati. Ndani ya intelijensia ya Tanzania, kulikuwa na mkakati wa kushawishi uasi wa kijeshi ndani ya jeshi la Idi Amin. Museveni alishirikishwa.

Pale Nairobi, Museveni alikuwa akitembea akigawa kwa Waganda wanaharakati nyaraka zenye hotuba ya Julius Nyerere.

Makachero wa Kenya walizinasa harakati za Yoweri. Wakapanga kumnasa Museveni. Walimtuma jasusi Mzungu mwenye uraia wa Kenya. Aliitwa Patrick Shaw.

Huyu alikuwa jasusi lilokubuhu. Inasemwa, jasusi huyu alikuwepo kwenye mpango uliotekelezwa wa kumteka na kumwua mwanasiasa wa Kenya wa enzi hizo, J. M Kariuki. Ni mwaka 1976.

Museveni anasimulia;

kuwa alipokaa na rafiki yake akinywa kahawa mgahawani, Nairobi Hilton Hotel, ghafla, alimwona mzungu mnene mwenye madevu akiingia. Alikuwa jasusi Patrick Shaw.

Jasusi Shaw alikaa mbali kidogo na Museveni. Akachukua gazeti na kujifanya analisoma huku akitupa jicho kwa kuvizia kwa Yoweri Museveni.

Museveni akafanya maamuzi ya haraka. Akamwambia rafiki yake abaki hapo hapo. Naye Museveni akakunjua gazeti kujifanya yuko bize analisoma.

Kisha akaagiza kahawa nyingine. Muhudumu alipokuja nayo tu, basi, Museveni, akainuka akijifanya anakwenda msalani. Ikawa kimoja...breki ya kwanza ikawa Namanga, mpakani mwa Kenya na Tanzania.

Nini kilimtokea Museveni alipofika Namanga, bila passsport wala nyaraka nyingine za kumwezesha kuvuka mpaka kuingia Tanzania?

Itaendelea...
maggid
138472046_10222085604581902_2195085750023900833_n.jpg
 
Bongo Hapo Zamani: maggid

Siku Museveni Aliponusurika Kutekwa Nairobi ( 2)

Siku ile pale Hilton Hotel, Museveni alitumia maarifa yake katika medani za kiintelijensia kuweza kunusurika kutekwa.

Maana, alipotoka tu hotelini pale, Museveni alikata kona moja ya mtaa na kusimamisha teksi.

Akamwambia dereva ampeleke Serena Hotel. Alipofika Serena Hotel, Museveni akabadilisha teksi. Akamwambia dereva mwingine wa teksi amwahishe kituo cha mabasi.

Museveni alipofika kituo cha mabasi, akaparamia basi la ' Matatu' kuelekea Namanga.

Kwenye medani za kiintelijensia, kubadilisha vyombo vya usafiri ni njia ya kufuta nyayo zako kwa adui anayekufuatilia.

Museveni alijua kuwa huko nyuma alikotoka, jasusi Shaw angefanya jitihada za kuwasiliana na makachero wa Kenya ili watu wa Uhamiaji Namanga wahakikishe Museveni anakamatwa. Lakini, Museveni hakuwa na mashaka, alitaka afike Namanga tu.

Kama nilivyopata kubainisha huko nyuma, kuwa si wengi wenye kufahamu, kuwa Yoweri Museveni aliunganishwa kwenye mfumo wa Intelijensia ( Usalama) wa Tanzania tangu mwaka 1976.

Kwa kupitia Edward Sokoine, Museveni akaunganishwa na watu wa Intelijensia, mmoja wao ni Kapteni Issonde. Hivyo, Museveni alipata mafunzo yake ya Kiintelijensia akiwa Tanzania.

Pale Hilton Hotel, Museveni alimwachia balaa kubwa rafiki yake aliyekuwa akinywa naye kahawa, maana , alikuwa ni Mganda asiyeelewa lolote.

Jasusi Patrick Shaw, baada yakuona saa nzima na nusu imepita bila Museveni kurudi kumalizia kahawa yake, akabaini, kuwa Museveni amemtoroka. Ndipo Jasusi Shaw akamkamata Mganda yule na kumpa wakati mgumu. Kumwuliza maswali yasiyojibika.

Akampeleka hadi kituo cha polisi. Huko Mganda yule akahojiwa na makachero wa Kenya na kisha kuachiwa.

Alipofika Namanga Museveni akapumua. Maana, ni kama amefika nyumbani. Museveni alifahamika sana Namanga, upande wa Kenya na Tanzania. Hata wafanyabiashara wadogo wadogo walimjua Museveni.

Alikuwa maarufu kama ' Mzee Kassim'. Hilo lilikuwa moja ya majina matatu aliyotumia Museveni kuficha utambulisho wake kwa sababu za kiusalama.

Akiwa Nairobi alijulikana kama Kassim, na Dar es salaam aliitwa Mussa. Na mara kadhaa alipenda sana kuvaa kanzu na kibaraghashea. Hiyo ya kanzu na kibaraghashea ilimwwzesha Museveni kuingia Kampala hata enzi za Idd Amin.

Museveni kupitia kitabu chake anasimulia pia alivyokuwa akiingia Kampala kukusanya taarifa za kijasusi. Kwamba alikuwa akitembea mitaani akiinekana kama ' Ustaadh' kwa kanzu na kofia za kiislamu alizovalia. Usiku alilala misikitini.

Kila Museveni alipofika Namanga, watu walisema sasa amefika ' Mzee Kassim wa kutumia! ' Maana wakati huo kulikuwa na wimbo maarufu wa ' Kassim' ulioimbwa na Mlimani Park Orchestre.

Kassim aliiimbwa kama mtu aliyekuwa wa matumizi na kusahau familia. Namanga Museveni akinunua kitu hakuhangaika na chenji iliyobaki. ( Fedha za Usalama?)

Namanga Museveni alifahamika pia kama mfanyabiashara. Museveni alikuwa kweli akipita akiuza biashara zake za kuficha utambulisho wake. ( TRA ya Tanzania wakimfuatilia Museveni watabaini malimbikizo makubwa ya kodi ambayo hakupata kulipa TRA kwa biashara zake za mpakani enzi hizo! )

Hivyo, kwa Museveni, Namanga aliweza kuvuka mpakani , awe na passport au bila passport!

Kwa ufupi kabisa, nyendo za Yoweri Museveni zilikuwa zikifahamika na watu wa intelijensia ya Tanzania, watu wa aina ya Captain Issonde.

Ni kwa vile, Museveni aliifanya kazi ya Intelijensia ya Tanzania pia.
138494830_10222086263078364_5836923695840125357_n.jpg
 
Huyu Ndiye Mtanzania Major Issonda Aliyekabidhiwa Museveni Kwenye Intelijensia Ya Tanzania...

Ni mwaka 1976. Yoweri Museveni kwenye kitabu chake anaeleza mchakato wa yeye Museveni kuunganishwa kwenye intelijensia ya Tanzania ( Usalama) na kutambulishwa na Major Issonda wakati huo akiwa Captain.
Asante sana John Issonda ( Mtoto wa Major Issonda) kwa picha hii. Nimefurahi kusikia kuwa Mzee Museveni bado anaikumbuka na kuisaidia familia ya Major Issonda aliyefariki dunia mwaka 1992.
138634452_10222086862213342_2437787520999248929_n.jpg
 
Kwa hizi Haso.... halafu eti

kuna mbuzi mahali anataka kuchukua nchi kwa kipande cha karatasi

Jamani uliona wapi ? Haya mambo siyo mepesi kama kwenda washroom

Watu wamejipanga na wakapangika, nashauri tuendelee kuwa washabiki tu!
 
OK,nafikiri kichwani mwake akifikiria maisha aliyopitia hadi kuitawala Uganda anakaa na kusikitika tu kuwa bado hajaona wa kuchukua nafasi yake ana zaidi ile miaka yake aliyonayo sasa hivi anaona bado ni gentlemen kabisa,bado barobaro la haja.....hizi ni akili za watawala wasiojali kitu kabisa wanapatikana kwa wingi barani afrika
 
Alisha sema haoni mtu wa kumuachia nchi
Uzuri ni kwamba hana ahadi na Mungu, ajifunze kwa mwenzake wa Burundi.... Yeye mwenyewe aliingizwa madarakani na Tanzania baada ya kumfurusha Iddi Amini, kwa asili ya binadamu hata ufanye mazuri mengi kiasi gani uki over stay in power watakuchoka tuu. Haiwezekani ifikie mahali uwe unagombea madaraka na mjukuu wako na pia kizazi unachotaka kukiongoza 80 % ni vijana na wewe ni babu yao!!! Hii maana yake ni moja tuu since 1986 alipoingia madarakani ameshindwa kuandaa mtu wa kumrithi, sasa anahangaika amuweke mtoto wake.
 
Back
Top Bottom