Ila tuache mzaha, hawa Watutsi kwenye suala zima la ukachero wako vizuri mno: Ukiwaangalia watu kama Paul Kagame, Fred Rwigyema na Yoweri Museveni utagundua kwamba hawa jamaa ni watu ambao They Mean Businness. Mdogo wake Yoweri Kaguta Museveni kipindi cha mapigano alikuwa anatumia jina feki la Salim Salehe huku jina lake la kuzaliwa akiitwa Caleb Akandwanaho. Huyu General Salim Salehe akiwa na miaka 25 tu ndiye aliongoza uvamizi wa jiji la Kampala kipindi cha The Ugandan Bush-War.
Kuna Professor mmoja wa UDSM alishawahi kumfundisha Museveni, anasema Yoweri was never in a class. And when we ask where he is, they tell us we saw him somewhere carrying a riffle. Jamaa alianza itikadi kali tokea yuko chuoni na kazoea sana vita. Naamini katika maraisi ambao wana uelewa mpana sana kuhusu masuala ya machafuko, vita, jeshi na ujasusi nadhani Museveni na Kagame hawana mpinzani.