Tuliza akili yako,kama unataka mwambie ukweli na abadili no ya simu,akigoma ujue tayari utakuwa mume mwenza muda si mrefu. Usitumie hasira,tumia akili na hakuna adhabu mbaya ya kumpa mtu kama adhabu ya kisaikolojia.Nitakupa mfano:
Kuna jamaa aliambiwa mkeo anachepuka,hakutaka kukurupuka akafanya uchunguzi wake akajua ni kweli. Akapanga shambulizi moja la hatari sijui hata niliitaje. Siku ya kutoa adhabu akarudi home mchana akamwambia mkewe anajisikia vibaya anataka apumzike. Mkewe akamwambia anaenda sokoni fasta lakini jamaa akamwagiza kwenye duka la madawa ambalo lipo mtaa wa pili akamwandikia dawa.Kumbe jamaa haumwi anazuga tu,akamwambia ukishaniletea dawa ndio uende sokoni.
Mke kuondoka tu jamaa akaingia jikoni akakuta msosi kwenye hotpot,akachota wali upande mmoja hadi chini ya hotpot na kuuweka pembeni, huo msosi ulikuwa unapelekwa kwa mchepuko. Sasa jamaa akaingia chooni akakata "gogo", halafu akachota kimba kidogo akaingia jikoni na kuweka kimba alichochota kwenye hotpot kwa chini.
Sasa akajazia ule wali aliouweka pembeni kwenye hotpot kisha akapakua mboga nyingine na kuweka juu ya msosi ili uonekane haukutolewa kuwekwa pambeni.
Mke akarudi akampa dawa na kwenda sokoni,akabeba na msosi. Kilichotokea huko kwa mchepuko siri anaijua mke mwenyewe.
Sasa siku moja wakaonana njiani mwenye mke na mwizi wake,jamaa akamwambia kila kitu kuhusu yeye na mkewe na akamwambia hainiumi kuwa na mke wangu ila inaniuma unakula msosi wa mwanaume mwenzio na kwa ushenzi nikaamua nikuwekee na makapi ya msosi wangu(yaani kimba),umekula msosi wangu umekula na kimba changu.
Mchepuko ulihama mtaa wenyewe,kumbe mchepuko lilifakamia msosi humohumo kwenye hotpot halafu chini kuna kimba cha jamaa..