Siku nikifika kanisani kwa Mwamposa kama pale haabudiwi Mungu wa kweli huduma yake nitaifunga na atachakaa.

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hello!
Katika kazi ya utumishi wa Mungu kuna watumishi wa aina 3, watumishi wa kweli (Watumishi wa Mungu aliye hai), watumishi fake na watumishi wa uongo.
Kila kundi lina makundi mengine madogo madogo lakini nitaeleza kwa ufupi tu.
1. Watumishi wa kweli
Hawa ni watu wa Mungu ndani ya kanisa wamepokea wito wa Mungu direct au indirect. Wanaotumika kwa hofu ya Mungu na kufanya utumishi kwa kanuni za Kimungu.
2. Watumishi wa uongo.
Hawa ni watumishi wanaofanya kazi ya kanisa kijanjajanja. Hawana wito wa Mungu na wenyewe wanalifahamu hilo. Ila kwako wanatumia shuhuda za uongo na maneno ya ulaghai. Hawa hujaza haraka kwenye nyumba zao za ibada kwakuwa hutumia saikolojia ya mwanadamu. Hutoa tumaini kwenye mioyo ya watu , watu hufarijika pasipo kupata majibu sahihi ya matatizo yao. Katika watu 3000 lazima tu wapo watakaoolewa, kupata kazi nzuri, kufungua biashara nzuri, hao watu akilini mwao watajua kuwa maombi ya mtumishi yamefanya kazi kumbe ni nature tu ya dunia.
3. Watumishi fake.
Hawa wana nguvu ya kuponya, kuona yaliyo sitirika na kutenda miujiza mingine lakini roho zitendazo kazi ni za ibilisi (cult spirits).
Tarehe 26 Agosti 2014 nilienda kanisani kwa Nabii Flora kipindi hicho yuko hot sana hapa mjini. Nikamkuta akiwa kwenye utumishi nambari 2 na 3 yaani ni nabii wa uongo na ni fake. Nikaifunga kazi yake. Tangu siku hiyo alianza kufilisika, hakuwika tena, mpaka anaingia kaburini mwaka huu.
Sasa kelele zimekuwa nyingi.
Nitaenda kwa Mwamposa, kama sometimes na Mungu wa Israel atastawi zaidi ila kama yuko kwenye kundi nambari 2 au 3 nitawapa jibu. Hatasimama, nitaifunga huduma yake.
 
Kwanza kabisa, thibitisha Mungu yupo kweli.
 
Mkeo awaite ndugu zako ukamatwe ukanywe dawa/dozi yako kwanza ndo uje hapa jukwaan usome upya ulichoandika
 
Umesema kweli kabisa. Unaweza pia kuifunga bila kwenda kanisani kwake.
 
Ujue tu huyo Yesu ni mchongo tu wa Wayahudi, Mungu wa kweli hatoi kafara. Kimantiki hakuna nabii wa kweli.
 
ULIENDA TUNAOMBA MAJIBU
 
Oya vip ulienda?
 
Kilasiku mnavyozidi kumtukana MWAMPOSA ndivyo anazidi kujaza kanisa lake na mamlaka wanaona umuhimu wake wanamuongezea eneo...
Shida yenu WaTz mkiona mtu ameinuka kimafanikio mnapata wivu chuki makasiriko husda vinyongo na roho mbaya...
Ndiyo maana mnakufa masikini
 
Mbona iko wazi sana kuwa mwamposa ni janja janja ila wafuasi wake kama mko apa nyie na ng'ombe tofauti hakuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…