SEHEMU YA 08
****************************************
Ilipoishia ni pale nimeamka kitandani simuoni yule kijana niliekuwa ninalala nae sasa ikanibidi niamke nimtafute yuko wapi sasa nikatoka nikawq natembea tembea sasa wakati nazunguka zunguka ghafla nikawa nimekaribia mlango wa kutoka nje nikawaona fetty na familia yake wapo nje wamekaa kwenye mkeka kama wana swali lakini cha ajabu walikuwa wamebadilika sura zao nitatisha sana mimi hapo nawachungulia tu nawaona wana masikio kama ya mbuzi mbaya zaidi baabake fetty alikuwa ana mdomo meno yake yametoka nje kama ya mnyama ngili hii kitu ilinishtua sana wao walikuwa hawajaniona lakini cha aiabu nikataka kukimbia ila sasa kila nikitaka kukimbia naona nguvu zimeniishia ghafla nikawa naona sina nguvu nikawa nasikia sauti ikiniambia usiogope ilikuwa ni sauti kubwa mno ikabidi nipoteze fahamu ndugu msomaji nilipoteza fahamu na sikujua kipi kiliendelea zaidi ya kwamba niliposhtuka sikujiona tena nipo katika ile dunia niliona nipo kwenye kitanda nimelala nikashangaa hapa ni wapi ikabidi niinuke nilikuja kutambua kumbe nipo kwangu nimelala ikanibid niwashe simu kucheki majira ndugu msomaji ilikuwa ni usiku wa saa kumi na moja nikajiuliza ina maana yale yote yaliyotokea nilikuwa naota hama ni kweli na nimewezaje kurudi tena duniani? Nikawa na maswali mengi kichwani ghafla wakati natafakari usingizi ukanikamata tena nilishtuka baadae sana tayari pamepambazuka na ilikuwa ni saa nne asubuhi nikaamika kitandani pale mwili wangu ulikuwa umechoka sana sasa nikajisemea mbona nimechoka sana hivi ikanibidi niende bafuni kuoga baada ya kuoga nikatoka nje na kwenda sokoni kununua mahitaji yangu nikiwa sokoni nanunua vitu ghafla simu yangu ikaita na jina ni fettt hallow mume wangu pole kwa uchovu najua unajiuliza maswali mengi kichwani mwako maswali yako yote leo mchana nakuja kukujibu byeee nakupenda yalikuwa ni maneno ya fetty baadae simu ikakatwa duuh nikasema mungu wangu nisaidie tu basi nikaondoka kurudi nyumbani baada ya kununua mahitaji muhimu nilipofika nyumbani pale nilisalimiana na wapangaji wenzangu waliokuwa nje pale mda natoka sikuwaona lakini mmoja wa wapangaji wenzangu akaniambia mbona kijana leo inaonekana una mawazo sana kulikuno? Nikamjibu kwann ?, akasema umetupita hapa asubuhi tumekuita hauitiki na salamu zetu umezikataa ulikaa kimya, nikasema duuuh akaendelea sasa tunashangaa mda huu unatusalimia tena kama vile ndio unatuona mda huu nikasema duuh nisameheeni sipo sawa basi nikaingia ndani pale ila nilishangazwa na maneno yao ina maana niliwapita bila kuwasalimu kweli?
Basi nikapika pika pale chakula nikala baadae nikawa nipo nipo tu mule ndani nilikuwa natafakari sana sasa ghafla simu yangu ikaita kucheki namba ilikuwa ni namba ngeni hallow hey mambo vp? Ilikuwa ni sauti ya kike nikajibu safi nani mwenzangu? Akasema mimi salome ina maana umefutaga nambaangu? Salome gani akacheka akasema salome ex wako uliekuwa unampenda sana nimepata taarifa upo chanika na mimi nimekuja chanika kwa dada natamani siku tuonane aliniiambia hivyo,
Ndugu msomaji huyu salome ni mwanamke niliempendaga sana kipindi nasoma nae shule ya secondary kizuka iliyopo mkoani morogoro ni shule ya jeshi sasa kipindi nipo form 3 ndio niliweza kujuana na salome ni mwanamke mzuri sana ila alieshika dini mno nilitokea kunpenda sana na yeye alinipenda hadi tunamaliza masomo pale tukaja baadae kupotezana na ndio mapenzi yetu yalipokufa pale;
Wooow nikajikuta nimepata furaha kuwasiliana tena na salome basi salome akaniambia nimekutafuta nimepewa nambaako na rfk ako mussa nilikutana nae kanisq la ukonga ibadani akaniambia upo siku hizi chanika lakini nqjua unateseka sana kuna mambo magumu nimeoteshwa kuhusu wewe kama utanishirikisha nitakusaidia?
Yalikuwq ni maneno ya salome maneno yake yakaniogopesha sana kajuaje kama nina magumu napitia? Hau mungu kamuonyesha maana salome ni mtu alieshika dini sasa nikaona hatari inaanza kuja juu yangu nikamwambia sinq magumu yote yote ni ndoto tu unaota ww nikakata simu,
Ndugu msomaji sikutaka tena kuendelea kuwasiliana na salome niliihisi uenda amekuja kuyaharibu mapenzi yangu na fetty nilijikuta tu nimeanza kumchukia salome nikajisemea nafsini huyu kajuaje eeh?
Sasa wakati nipo na mawazo ghafla fetty akanipigia simu hello mume mimi ndio nakuja mda huu hapo nyumbani nikamjibu sawa basi baada ya muda fetty alikuja kweli alikuja na gari dogo haina ya v8 akaja hadi pale ninapopanga majirani walishangaa sana akashuka kila mtu alishangaa sana kumuona fetty na gari leo tena alikuwa anakujaga wanamuonaga ila hakuwahi kuja na gari pale ndio kilichowashangaza sana watu akaingia ndani nilimfungulia mlango akanikumbatia pale alikuwa ananukia manukatoa mazuri sana safari hiyo basi tukawa tumekaa kwenye sofa akaniambia leo nimekuja na gari ilo gari ni gari lako kuanzia sasa duuuh nilishangaa mno akaendelea yale yote uliyokuwa unayafikiria ni kweli mimi na ww tulienda wote ujinini siku ile nyumbani na yale yote uliyoyaona kule sio ndoto ni kweli akanendelea kusema wazaz wangu wamekupenda sana na ili gari baba ndio amekpa kama zawadi kuanzia sasa ni lako ili akandelea ameomba msamahaa kwa kitendo cha siku ile ulichotuona tupo nje pale tulikuwa tunapigwa swala ya kuombea mema juu yangu na ww ili ulituona tukiwa katika maumbile tofauti uliyotuzoea najua uliogopa sana akasema ila usijali lakini pia tuna vita kubwq sana,
Nikqmuuliza vita gani?
Akasema salome ndio adui yetu sasa
Maneno haya yalinishtua mno sana
Wakuu nitandelea baadae jioni