SEHEMU YA 05
******************************
Ilipoishia sehemu ya 04 ni pale nilipokuwa nimekutana na dada bar akanipeleka kwake kumbe yule dada ni fetty aligeuza alichukua surq ya mtu mwingine na ndio siku hiyo nilipojua fetty mchumbaangu kuwa ni jini na aliniambia kuwa yeye ni jini na amenipenda toka nipo mdogo na alikuwa ameolewa na babu yangu marehemu mzee msekwa.
#########
SASA INAENDELEA#
nilitetemeka sana mule ndani mkojo ulinitoka sio kitoto ikabidi nimuulize fatma ww ni jini kwann sasa muda wote ule haujaniweka wazi na ww na babu yangu mzee msekwa mmejuanaje?
Akacheka sanaa then akaniambia ni stori ndefu ipo siku nitakwambia kwa sasa sio muda sahihi kikubwa ni kuwa ole wako utoe hii siri na mimi nipo kwako kwa amani sina nia mbaya na ww maana nakupenda toka nilimuua babu yako miaka 25 iliyopita kipindi upo mdogo niliamua kukupa ww ulinzi hadi unakuwa niakikishe nakuwa na ww maana toka upo mdogo nilikupenda,
Ikabidi nimuulize sasa nyie majini mnaishi miaka mingapi na mbona hauzeeki?
Ndugu msomaji yule jini aliibadilisha akili yangu kwa muda mfupi nikajikuta tu napiga nae stori nishaanza kumzoea pale na uoga ulikuwa ushapungua,
Akanijibu kuwa wao majini ni immortal ni viumbe ambao wanaweza kuishi miaka mingi akananianbia yeye hadi mda huu yupo duniani ana miaka 300 sasa jibu lake likanishangaza saana nikamuuliza sawa sasa ww una mpango gani na mimi?
Akanijibu kuwa yeye anataka nimpatie watoto azae na mimi na anataka aishi na mimi,
Nikamuuliza sasa jini na binadamu wanawezaje kuishi ?
Akacheka sana akasema inawezekana baada ya kunijibu hivyo akaniambia leo ndio umejua ukweli wangu iwe siri na ole wako hii siri uitoe kwa ndugu yako yoyote yule.
Baadae fetty akainuka na kuniletea juice akanipa ninywee ilikuwa juice ya embe nikaanza kunywa wakati nakunywa ile juice nilijiona nguvu zinaniishia ghafla nikapoteza fahamu nilipoteza fahamu kwa mda mrefu nilikuja kushtuka asubuhi simu yangu inaiita sana nilipoamka ndugu msomaji nilijikuta nipo kwangu kabisa wakati nakumbuka usiku wa jana nilikuwa kwa fetty sikushangaa sana niliihisi pale nilipopoteza fahamu labda fetty aliniyayusha kichawi,
Nikapokea simu alikuwa ni fetty hallow mume wangu umeamkaje?
Aliniuliza hivyo nikamwambia sijambo nipo sawa akaniambia leo mchana nakuja hapo kwako nikamwambia sawa ila akaniambia niende dukani nikanunue udi halafu nilipuulize marashi chumbani kisha akaongeza unajua sasa mimi na ww ni wapenzi rasmi na ushanijua mimi ni jini sisi majini hatupendi uchafu inaidi uwe unasafisha chumba chako kiwe safi kila siku na uwe msafi nikamwambia sawa basi akaniambia kuna hela nakutumia muda huu mchana mimi nakuja nikamwambia sawa basi akakata simu,
Baada ya mda sms ya mpesa ilionyesha nimepokea shs laki 2 kutoka kwa fattuma
Nikasema kimoyoni daah japo majini ni viumbe hatari ila sasa hela napata nitamvumilia tu ndugu msomaji ni kuwa akili yangu ilishabadilishwa na fatma nikawa naona ni mtu wa kawaida tu kwangu basi kufupisha stori kweli mchana fatma alikuja nilifanya kama alivyoniambia asubuhi chumba kilikuwa kisafi alipokuja sasa alinisifia kuwa chumba kipo safi na nilikuwa nimevaa mavazi masafi na nilipuulizia manukato kama alivyosema,
Fatma siku hiyo alikuwa na furaha alipokuja alinirukia na kunibusu sana baadae tukiwa ndani akaniambia leo nataka nikwambie kitu kizuri nikamwambia sawa akasema kuanzia wiki inayoanza nitaamia kwako tutakuwa tunaishi kama mke na mume maneno yake kiukweli yaliniogopesha yaani aje akae na mimi ili nilimkubalia tu basi akaniambia mume wangu halafu nataka leo usiku nikupeleke nyumbani kwetu ukawaone ndugu zangu wanataka wakuone ikabidi nimuulize kwani kwenu wapi?
Akacheka sana akaniambia mimi nyumbani kwetu ni baharini
Jibu lake lilinishangaza mno nikqmuuliza baharini wapi posta hau?
Ghafla fatma......
Wakuu itaendelea wakuu sasa ndio nataka nipelekwe na fatma kwao baharini sijui ni bahari gani ambapo ndio ndugu zake wanaishi
Niwaombe radhi kwa ucheleweshaji wa muendelezo toka juzi nilipata dharula wife amejifungua na muda mwingi nakuwa nae kwa hiyo nakosq muda wa kuingia humu ila leo nitajitahidi nilete muendelezo usiku