Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

SEHEMU YA 14
***********************
nilijitahidi sana kumuomba msamahaa fetty asinipe mateso lakini wapi nakumbuka alinifungia kwenye chumba kimoja mule ghorofani niliweza kukaa mule kwenye chumba kwa zaidi ya mwaka nilikuwa kama msukule sikupata huduma nzuri zaidi tu ya kupewa chakula na maji huduma za aja kubwq na ndogo nilikuwa nikizitoa mule mulw chumbani yaani nilikuwa najisaidia mule mule chumbani na kukojoa mule mule mwaka mzima sikuweza hata kuliona wingi la nje maisha yangu yalikuwa ni kama mfungwa niliefungwa kwenye gereza hatari zaidi la guentanamo[emoji29],
Hii ilikuwa ni adhabu aliyonipa fetty kwa kumsaliti sasa nikaona kwann majini na binadamu hayawezi kukaa pamoja nilijutia sana kukutana na jini fetty,
Fetty sasa alinionyesha roho ya kikatili mno,
Mateso yalizidi kuendelea kila siku fetty alipokuwa anakuja kunipa chakula alikuwa akija na kunirushia chakula kama mbwa na kuniambia maneno machafu ya karaa,
Ndugu msomaji nywele zangu zilikuwa kubwa mno kqma msukule nilikuwa na makucha marefu sasa nilikata tamaa ya maisha niliqmini sitaweza kuiona tena dunia niliamini nitafia kwenye lile gorofa la fetty na ndugu zangu wasingeona hata mfupa wangu,
Niliteswa sana zaidi ya mwaka nipo mule nfani sasa nakumbuka usiku mmoja nipo nimelala mule ndani kwenye chumba kilichojaa mauza uza ya kila aina niliota ndoto namuonq salome kaja yupo mbele yangu kashika bibilia ananiambiq nisikate tamaa ipo siku nitatoka katika haya mateso nilimuona salome akiwa kanisimqmia mbele yangu akiwa na bibilia na mavazi meupe nilipofumbua macho sikumuona nikqsema hii ni ndoto nikalala asubuhi ikafika ghafla asubuhi muda ya saa 4 kama hivi maana nilikuwa sijui hata majira yanaendaje zaidi ya kukisia tu hapo ndugu msomaji kipindi nipo kwenye kile chumba cha mateso bado mgongo wangu ulikuwa unaniuma kama kawaida na mbaya zaidi hata miguu sasa ilikuwa tayari ni kama imepalqlazi sikuwa na uwezo wa kutembea,
Sasa asubuhi ya siku hiyo mida ya saa 4 hivi niliona mlango ukifunguliwa ghafla nikatazama mlangoni kuona ni nani kaingia mule ndani, alikuwa ni fetty alikuwa kaja huku amekasirika sana akanifuata na kuniambia ww mpumbavu nilitaka kukuuwa kabisa lakini kwa sababu nakupenda na nilikupenda sana nashindwa kukuua ila hii adhabu niliyokupa ndani ya mwaka sasa imekutosha then akaendelea kusema huu ugonjwa wa kiuno na kupapalaizi kwako hautapona tena hii adhabu itakutosha sasa unaweza kuwa huru nitakuchukua na kukutupa sehemu lakini haya yote uliyataka ww na kama babu yako nilivyomuua ndio nilitaka nikuue na ww ila ww nimeshindwa mungu wako ni mkubwa mno,
Fetty alimaliza kwa kuja na kunishika kichwani ghafla nikajikuta nimepoteza fahamu sikujua kipi kiliendelea ila nilikuja kushtuka nikiwa sipo eneo lile nipo eneo lingine geni tena nimezungukwa na watu wengi nilipozidi kushangaa ghafla sauti za wale watu walionizunguka mmoja wao alisema kwa sauti naonaa ameamkaaa.

Itaendelea
 
Endelea kutupa nondo usipotee tena kwa muda mrefu ukiwa kimya. Story tamu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…