Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

SEHEMU YA 16
*******************************
Salome alijitahidi kunipa matumaini pale kitanda akaniambia leo nimekuja kukuona nitafanya kila kitu niweze kukuchuku hapa hospitalini nikamwambia sawa,
Salome aliniacha mule chumbani akaenda kuzungumza na madaktari wa pale muhimbili kwamba anataka kunichukua ila madaktari walionekana kukataa salome asinichukue salome alijitahidi sana kuomba na ndipo madaktari walipomwambia aje baada ya siku mbili kwani bado nipo chini ya uangalizi wao ndipo salome alipokubali kishingo upande na kuondoka pale hospitalini akiniacha,
Atimae usiku wa siku hiyo niliweza kurudishwa kwenye wodi ya kawaida na kuchanganyika na wagonjwa wenzangu,
[emoji116]NILIYOYAONA MAMBO YA KUTISHA PALE MUHIMBILI HOSPITALINI USIKU WA SIKU HIYO#
Ndugu msomaji sipo hapa kwa kuisema vibaya hospital ya taifa ya muhimbili naweza kusema hivi kwa kuwa usiku wa siku hiyo niliweza kukutana na mambo ya kutisha sana pale muhimbili,
Ipo hivi usiku wa siku hiyo aisee niliweza kuona mambo ya ajabu sana yanayotendeka muhimbili pale,
1.nilipokuwa nimelala niliweza kuonyeshwa mambo ya ajabu yaliyopo katika vyumba vya mahiti yaani mochwari pale muhimbili nilishuhudia baadhi ya maiti zilizokuwa mule mochwari kumbe usiku uwa zinaamka na kuanza kuzunguka muhimbili nzima,
2.madaktari kuzini na wagonjwa wakati wa usiku,
Ndugu msomaji niliweza kuonyeshwa tabia chafu za baadhi ya madaktari wanaokuwa wakiwabaka wagonjwa wa kike usiku niliweza kuona haya mambo nikiwa pale kitandani najua ni ngumu kueleza mambo yote maana mambo mengine sitapenda kuyaweka adharani lakini jambo moja la mwisho niliweza kuona kuna daktari mmoja pale muhimbili ni wakala wa gamboshi wakala ambae yupo pale kwa kazi moja ya kuaribu mimba na baadhi ya mimba zinazoaribiwa wanazichukua na kuzipeleka gamboshi ambapo wale watoto uchukuliwa na kupikwa kwenye majungu makubwa na wanatengeneza mafuta so yale mafuta wachawi wa gamboshi wanayapaka na yale mafuta yana nguvu sana na kuwapa wachawi uwezo mkubwa wa kutenda mambo yao ya giza,
Ni mengi sana ngoja tuachane na mambo ya muhimbili niendelee na siku ya pili aliyokuja salome kunichukua hii siku salome alikuja pale wakamruhusu salome anichukue pale kweli tulifanikiwa kuondoka muhimbili salome alikuja na gari dogo private nilikuwa sijui naenda kuishi kwa salome na nitaishi vipi nilikuwa nimetulia tu ndani ya gari safari ilianza kuelekea kwa salome ambae alikuwa anakaa mombasa sasa tuliembea mwendo mrefu na atimae kama masaa kadhaa tuliweza kufika kwa salome nilishangaa sana salome alikuwa amepanga katika nyumba nzuri mno alipanganisha nyumba nzima basi tukaingia ndani pale saloome akanikaribisha na kuniambia niwe na amani nitaishi nae hadi nitakapokuwa sawa nikamshukuru kwa wema wake na atimae maisha ya mimi kuishi kwa salome yalianza tulikuwa hatulali chumba kimoja maana nyumba ilikuwa na vyumba vitatu alinipa chumba kingine nilale na yeye alikuwa akilala chumba kingine,
Niliweza kuumaliza mwezi mmoja wa kukaa kwa salome na kila jumapili salome alikuwa akinichukua na kwenda nae kanisani nikajikuta sasa kanisa nishaanza kulizoea niliweza kujiunga na kwaya ya kanisani maana salome nae alikuwa mwanakwaya pia ila pia ni kwamba salome nilimkuta hana mme na alikuwa ameajiliwa ni mwalimu hadi mda huu hadi ninapoandika simulizi hii mimi na salome tunaishi pamoja lakini kwa hivi sasa tupo mkoa wa morogoro tulishahamaga dar na bahati nzuri salome nimefanikiwa kuzaa nae mtoto mmoja juzi kati sasa ni mwezi[emoji39][emoji39] nampenda sana ni mwanamke alienitoa mbali sana.
[emoji116]*************VITA NA JINI FETTY BAADA YA MIMI KUOKOKA
ITAENDELEA BAADAE
[emoji116]BAADA YA SIMULIZI HII KUISHA HAPO KESHO NITAENDELEA NA KISA KINGINE HAPA HAPA NILIVYOWAHI KUPELEKWA GAMBOSHI NA NILIVYOWAHI KUSHIRIKI KUSABABISHA AJALI NA KUUWA WATU HAPA DUNIANI KITUO CHETU KILIKUWA MLIMA SEKENKE
STORI NDIO KWANZA IMEANZA NAOMBENI KWA SASA NIISHIE HAPA USIKU NITAJITAHIDI NIENDELEE VITA NA JINI FETTY BAADA YA MIMI KUOKOKA NA JINSI NILIVYOANZA MAHUSIANO NA SALOME [emoji122]
 
Swali.. salome alipokuchukua hospitali kwanini mlikuwa mnalala vyumba tofauti wakati unasema alikuwa mpenzi wako hapo kabla? Na mlilala vyumba tofauti kwa muda gani?
 
Swali.. salome alipokuchukua hospitali kwanini mlikuwa mnalala vyumba tofauti wakati unasema alikuwa mpenzi wako hapo kabla? Na mlilala vyumba tofauti kwa muda gani?
Ni kweli mkuu salome alikuwaga mpenzi wangu kipindi tulipokuwa shule kwahyo ilipita miaka mingi sana toka tumeachana na kila mtu akawa ana mishe zake so ilikuwa ngumu kulala kitanda kkmoja kwa haraka haraka maana kila mtu alikuwa ameshapitia mahusuano mengine na hata uhusiano uliporudi tuliaenda hispitalini kupima afya zetu ndio tukaanza mahusiano rasmi
 
Na vipi biashara kariakoo hukuwahi pita kujua nini kinaendelea kwenye ile frame au nani anauza?
 
Na vipi biashara kariakoo hukuwahi pita kujua nini kinaendelea kwenye ile frame au nani anauza?
Niliwahi kwenda ile fremu ishafungwa kabjsa na unajua mimi na fetty tuliachana mwaka 2020 mwezi wa nane ndio ameacha kunifuatilia sema kutoondoa utamu wa stori nitaelezea kila kitu leo na jinsi nilivyounganishwa na chama cha wachawi gamboshi
 
Niliwahi kwenda ile fremu ishafungwa kabjsa na unajua mimi na fetty tuliachana mwaka 2020 mwezi wa nane ndio ameacha kunifuatilia sema kutoondoa utamu wa stori nitaelezea kila kitu leo na jinsi nilivyounganishwa na chama cha wachawi gamboshi
Ok mkuu ngoja nisubirie kwa hamu jioni nitulie kwenye kiti kirefu nimchambe jini Fetty
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…