Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

SEHEMU YA 15
****************************************
ILIPOISHIA*#
Nilijikuta nazinduka pale nilipokuwa sipajui palikuwa pembezoni mwa bahari ya indi fukwe za coco beach watu walikuwa wamenizunguka wakinishangaa sana,
Sauti moja ilisikika ilikuwa ya mmama mmoja miongoni mwa wale watu ikisema sasa kaamka ndio niliposhikwa mkono na kunyanyuliwa pale chini,
Kulikuwa na watu wawili waliokuwa wameshika camera miongoni mwa wale watu waliokuwa wamenizunguka mmoja wa wale watu waliokuwa na camera pamoja na kipaza sauti yaani mic alikuwa amevaa tisheti iliyokuwa imeandikwa tbc1 ndio nilipogundua hawa ni waandishi wa habari,
Kijana kuwa na amani sisi ni raia wema tumekukuta hapa umelala toka asubuhi ikabidi tuite waandishi wa habari ,
Ilisikika sauti ya mzee mmoja miongoni mwa wale watu waliokuwa wamenizunguka ndugu msomaji kama unavyofahamu fukwe ya cooc beach uwa inakuwa na watu sana pale ndipo mahojiano na watu pale na wale watangazaji wa tbc1 yakaanza nilikuwa nahojiwa kuhusu nn kimetokea sikuweza kuongea sana zaidi ya kuwaambia mimi nipo salama ila naombeni mnipeleke hospitalini kwanza maana hali yangu sio nzuri niliwajibu hivyo wale waandishi wa habari ndipo nikaulizwa kwani unaitwa nani na umetokea wapi?
Nikaaa kimya kidogo ndipo kinasema nimetokea hapa hapa masaki sasa wakati nataka niendelee kuzungumza zaidi ghafla miongoni mwa wale watu waliokuwa wamekusanyika pale wakinitizama nilimuona fetty akiwa nae yupo pale tena ana kichwa kina mapembe halafu akaewa ananyooshea kidogo cha shiiiio yaani nisiendelee kuongea mengi ndipo nilipoanza kupiga kelele kama nimepandisha kichaa nikaanza kusema ondoka hapa ww ndio umenipa haya matatizo niache na maisha yangu nilikuwa nikipiga kelele huku nikimnyooshea mkono fetty ndipo watu walipozidi kunishangaa pamoja na wale waandishi wa habari, watu wakaanza kuongea ya kwao mmoja nilimsikia akisema huyu chizi kachanganyikiwa mpelekeni hospitali ndipo watu wanne waliokuwa wamejaazia walinikamata na kusimamisha gari safari safari ikaanza kupelekwa nisipopajua niliweza kuona msururu wa magari ukifuata gari letu sikujua nn kiliendelea maana nilijikuta tu fahamu zanfu zimetoweka nilikuja kuzinduka nipo hospitalin ilikuwa ni hospitali ya muhimbili niliweza kuijua hii baadae kujua nipo muhimbili nilikuwa nimefungwa kwenye kitanda mikono yangu yote nikawa nashangaa hapa wapi hapa, katika hiyo wodi kulikuwa na wagonjwa kibao niliwaona sasa nikiwa natazama mazingira hayo mara nikasikia mmoja wa wale wagonjwa waliokuwa wamelazwa jirani yangu akisema naona kaamka huyu jamaa ndugu msomaji sikuwa tena na kipi cha kufanya maana niliona kabisa akili yangu haipo sawa nilijiona ni mtu niliechanganyikiwa nilimkumbuka mamaaangu mzazi niliemuacha kule kwetu kijijini nikaanza kulia kwa uchungu haya ni maisha gani nilikuwa nishakata tamaa ya maisha yangu,
Sasa nilipokuwa nalia ghafla manesi wanne wakaja pale kwangu wakaanza kuongea nilimsikia mmoja akiongea kwa kunikashifu naona chizi umeamka uchizi wako umeanza tena nilimtizama sana yule nesi nilikasirika kuitwa chizi nikataka kuinuka kitandani nimvamie lakini mikono yangu ilikuwa imefungwa kamba kote nikaanza kupiga kelele ghafla nilianza kulia milio kama ya paka nyauuuu nyauuuu nilikuwa nikilia hivyo kiasi wale manesi walioogopa wakaita watu wa ulinzi na madaktari zaidi ambao walikuja kunituliza nilichomwa sindano nikajikuta napoteza fahamu,
Muonekano wangu wa nywele nyingi kichwani pamoja na kucha ndefu na meno yangu kuwa ya njano na harufu kali iliyokuwa inatoka mwilini mwangu ilionyesha kabisa kuwa nilikuwa ni chizi hau mtu niliekuwa nimechanganyikiwa.
**************************************
Taarifa zangu zilienea tanzania nzima kituo cha tbc1 kililipoti habari zangu habari za kuonekana kichaa katika fukwe za coco beach zilienea mji mzima na kwa bahati nzuri zilimfikia binti salome ambae alikuwa ni classmates wangu niliewahi kusoma nae ni mtu wa mungu kweli ndipo salome alipoamua kufunga safari na kuja hospitalini muhimbili kuniona akiwa na ndugu zake,
Salome alifika hospitalini akaanza kuliulizia mimi wale madakatari pamoja na walinzi wa muhimbili walimuuliza maswali mengi kama ananijua kivipi salome aliongea nao kuwa yeye ni dada angu alihojiwa karibia masaa 2 kuhusu mimi akawaambia anayoyjua japo hajui nn kimenipata zaidi nadhani aliamua kuwadanganya wala hakutaka habari zangu za ndani azitoe hadharani,
Salome aliweza kuhusiwa kuja kuniona na sasa nilikuwa nimewekwa chumba cha pekee angu kwa maangalizi zaidi, salome alifika nilipomuona salome nilililia sana salome alinifuata na kuniambia sasa wakati wa mungu umefika nyamaza usilie,
Wakuu itaendelea hiki kipande sitakuja kukisahau maishani[emoji29][emoji29][emoji29][emoji29][emoji29]
SEHEMU YA 16
*******************************
Salome alijitahidi kunipa matumaini pale kitanda akaniambia leo nimekuja kukuona nitafanya kila kitu niweze kukuchuku hapa hospitalini nikamwambia sawa,
Salome aliniacha mule chumbani akaenda kuzungumza na madaktari wa pale muhimbili kwamba anataka kunichukua ila madaktari walionekana kukataa salome asinichukue salome alijitahidi sana kuomba na ndipo madaktari walipomwambia aje baada ya siku mbili kwani bado nipo chini ya uangalizi wao ndipo salome alipokubali kishingo upande na kuondoka pale hospitalini akiniacha,
Atimae usiku wa siku hiyo niliweza kurudishwa kwenye wodi ya kawaida na kuchanganyika na wagonjwa wenzangu,
[emoji116]NILIYOYAONA MAMBO YA KUTISHA PALE MUHIMBILI HOSPITALINI USIKU WA SIKU HIYO#
Ndugu msomaji sipo hapa kwa kuisema vibaya hospital ya taifa ya muhimbili naweza kusema hivi kwa kuwa usiku wa siku hiyo niliweza kukutana na mambo ya kutisha sana pale muhimbili,
Ipo hivi usiku wa siku hiyo aisee niliweza kuona mambo ya ajabu sana yanayotendeka muhimbili pale,
1.nilipokuwa nimelala niliweza kuonyeshwa mambo ya ajabu yaliyopo katika vyumba vya mahiti yaani mochwari pale muhimbili nilishuhudia baadhi ya maiti zilizokuwa mule mochwari kumbe usiku uwa zinaamka na kuanza kuzunguka muhimbili nzima,
2.madaktari kuzini na wagonjwa wakati wa usiku,
Ndugu msomaji niliweza kuonyeshwa tabia chafu za baadhi ya madaktari wanaokuwa wakiwabaka wagonjwa wa kike usiku niliweza kuona haya mambo nikiwa pale kitandani najua ni ngumu kueleza mambo yote maana mambo mengine sitapenda kuyaweka adharani lakini jambo moja la mwisho niliweza kuona kuna daktari mmoja pale muhimbili ni wakala wa gamboshi wakala ambae yupo pale kwa kazi moja ya kuaribu mimba na baadhi ya mimba zinazoaribiwa wanazichukua na kuzipeleka gamboshi ambapo wale watoto uchukuliwa na kupikwa kwenye majungu makubwa na wanatengeneza mafuta so yale mafuta wachawi wa gamboshi wanayapaka na yale mafuta yana nguvu sana na kuwapa wachawi uwezo mkubwa wa kutenda mambo yao ya giza,
Ni mengi sana ngoja tuachane na mambo ya muhimbili niendelee na siku ya pili aliyokuja salome kunichukua hii siku salome alikuja pale wakamruhusu salome anichukue pale kweli tulifanikiwa kuondoka muhimbili salome alikuja na gari dogo private nilikuwa sijui naenda kuishi kwa salome na nitaishi vipi nilikuwa nimetulia tu ndani ya gari safari ilianza kuelekea kwa salome ambae alikuwa anakaa mombasa sasa tuliembea mwendo mrefu na atimae kama masaa kadhaa tuliweza kufika kwa salome nilishangaa sana salome alikuwa amepanga katika nyumba nzuri mno alipanganisha nyumba nzima basi tukaingia ndani pale saloome akanikaribisha na kuniambia niwe na amani nitaishi nae hadi nitakapokuwa sawa nikamshukuru kwa wema wake na atimae maisha ya mimi kuishi kwa salome yalianza tulikuwa hatulali chumba kimoja maana nyumba ilikuwa na vyumba vitatu alinipa chumba kingine nilale na yeye alikuwa akilala chumba kingine,
Niliweza kuumaliza mwezi mmoja wa kukaa kwa salome na kila jumapili salome alikuwa akinichukua na kwenda nae kanisani nikajikuta sasa kanisa nishaanza kulizoea niliweza kujiunga na kwaya ya kanisani maana salome nae alikuwa mwanakwaya pia ila pia ni kwamba salome nilimkuta hana mme na alikuwa ameajiliwa ni mwalimu hadi mda huu hadi ninapoandika simulizi hii mimi na salome tunaishi pamoja lakini kwa hivi sasa tupo mkoa wa morogoro tulishahamaga dar na bahati nzuri salome nimefanikiwa kuzaa nae mtoto mmoja juzi kati sasa ni mwezi[emoji39][emoji39] nampenda sana ni mwanamke alienitoa mbali sana.
[emoji116]*************VITA NA JINI FETTY BAADA YA MIMI KUOKOKA
ITAENDELEA BAADAE
[emoji116]BAADA YA SIMULIZI HII KUISHA HAPO KESHO NITAENDELEA NA KISA KINGINE HAPA HAPA NILIVYOWAHI KUPELEKWA GAMBOSHI NA NILIVYOWAHI KUSHIRIKI KUSABABISHA AJALI NA KUUWA WATU HAPA DUNIANI KITUO CHETU KILIKUWA MLIMA SEKENKE
STORI NDIO KWANZA IMEANZA NAOMBENI KWA SASA NIISHIE HAPA USIKU NITAJITAHIDI NIENDELEE VITA NA JINI FETTY BAADA YA MIMI KUOKOKA NA JINSI NILIVYOANZA MAHUSIANO NA SALOME [emoji122]
 
Swali.. salome alipokuchukua hospitali kwanini mlikuwa mnalala vyumba tofauti wakati unasema alikuwa mpenzi wako hapo kabla? Na mlilala vyumba tofauti kwa muda gani?
 
Swali.. salome alipokuchukua hospitali kwanini mlikuwa mnalala vyumba tofauti wakati unasema alikuwa mpenzi wako hapo kabla? Na mlilala vyumba tofauti kwa muda gani?
Ni kweli mkuu salome alikuwaga mpenzi wangu kipindi tulipokuwa shule kwahyo ilipita miaka mingi sana toka tumeachana na kila mtu akawa ana mishe zake so ilikuwa ngumu kulala kitanda kkmoja kwa haraka haraka maana kila mtu alikuwa ameshapitia mahusuano mengine na hata uhusiano uliporudi tuliaenda hispitalini kupima afya zetu ndio tukaanza mahusiano rasmi
 
Ni kweli mkuu salome alikuwaga mpenzi wangu kipindi tulipokuwa shule kwahyo ilipita miaka mingi sana toka tumeachana na kila mtu akawa ana mishe zake so ilikuwa ngumu kulala kitanda kkmoja kwa haraka haraka maana kila mtu alikuwa ameshapitia mahusuano mengine na hata uhusiano uliporudi tuliaenda hispitalini kupima afya zetu ndio tukaanza mahusiano rasmi
Na vipi biashara kariakoo hukuwahi pita kujua nini kinaendelea kwenye ile frame au nani anauza?
 
Na vipi biashara kariakoo hukuwahi pita kujua nini kinaendelea kwenye ile frame au nani anauza?
Niliwahi kwenda ile fremu ishafungwa kabjsa na unajua mimi na fetty tuliachana mwaka 2020 mwezi wa nane ndio ameacha kunifuatilia sema kutoondoa utamu wa stori nitaelezea kila kitu leo na jinsi nilivyounganishwa na chama cha wachawi gamboshi
 
Niliwahi kwenda ile fremu ishafungwa kabjsa na unajua mimi na fetty tuliachana mwaka 2020 mwezi wa nane ndio ameacha kunifuatilia sema kutoondoa utamu wa stori nitaelezea kila kitu leo na jinsi nilivyounganishwa na chama cha wachawi gamboshi
Ok mkuu ngoja nisubirie kwa hamu jioni nitulie kwenye kiti kirefu nimchambe jini Fetty
 
Back
Top Bottom