Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

SEHEMU YA 03
****************
SIKU ile ilikuwa siku nzuri sana kulionja penzi la Fatumah ni mwanamke mzuri sana kuwahi kumuona katika hii dunia ya watoto wa Adam na Hawa[emoji18]
SEHEMU YA 04
******************************************
SMS ya fatmah ilinishtua sana na ilisomeka hivi "hello mpenzi wangu naona umeiona huyo zawadi hapo niliyokuwekea kwenye huo mto mwekundu hiyo hela itakusaidia katika shughuli zako nakupenda sana ila usije ukaitumia kwenye mambo yafuatayo ulevi hau starehe za kuhonga wanawake byee",

Sms ya fatma hii aliyonitumia ikanichanganya kwann ameniambia maneno hayo ikabidi nimpigie simu yake lakini wapi kila nikipiga haipatikani nikawa najiuliza labda simu yake itakuwa imezima chaji ni nini na maneno yake sikuyaweka sana kichwani ndugu msomaji nilikuwa sijawahi kushika kiasi kikubwa cha hela kama kile katika maisha yangu ya nyuma laki 4 niliiona kubwa mno nikawa nimechanganyikiwa akili akili hii ikiniambia fanya kitu hiki huku nyingine ikiniambia hela itumie tu kwa mambo mengine basi nikasema ngoja hii hela ninunue vitu vya ndani maana nilikuwa nalala kwenye kitanda cha inchi 4 kwa 5 na godoro dogo ikabidi siku hiyo hiyo niingie dukani nilifanikiwa kupata kitanda cha tano kwa sita nikapata na godoro kwa kipindi hicho bei ya vifaa hivi ilikuwa sio kubwa sana basi hela nyingine iliyobakia nikanunua vyakula ndani nakumbuka nilinunua unga kilo 10 na mchele na dagaa na maharage nikabakia na kiasi kidogo cha hela nikasema inabidi ninunue mavazi kweli nilienda kuchagua mavazi.

Nguo za bei nafuu suruali kavaa na mashati nikawa nimebakia kama na shs elfu 40 mfukoni baada ya kufanya manunuzi yote hayo siku hiyo niliporudi nyumbani baada ya kuleta vitu vyote nilivyonunua sasa chumba kilianza kupendeza ukiangalia kitanda kipya na godoro jipya chumba kilikaa safi sana basi ukafika usiku maana siku hiyo nizunguka sana kununua manunuzi usiku wa siku hiyo ulikuwa mkubwa mno kwangu. Sitousahau ilikuwa hivi ilikuwa mida ya saa mbili usiku niliamua kuondoka nyumbani kutokana nilikuwa na kiasi flani cha pesa nilichobakia nacho elfu 40 nikasema leo ngoja niingie mahali pa kujirusha nakumbuka chanika kipindi hicho kulikuwa na bar moja maarufu jina naliifadhi bar hiyo ilikuwa on top watu walikuwa wakijazana hapo kulikuwa na kila aina ya starehe mimi ni mpenzi wa bia na wanawake sasa nikasema niende nikapate bia kadhaa kweli nilivaa zile nguo nilizonunua safi nikaenda hadi hapo bar sio mbali sana na home nilifika nikakuta watu kibao wadada warembo wazuri utadhani hawaendi chooni watoto figa kali[emoji1] na mabrazimen kibao basi nikaagiza bia zangu nne pale mezani

Basi nikaanza kupiga tungi wakati nipo nishachapa bia mbili simu yangu ikaanza kuita nikawa nakata sitaki usumbufu kila nikikata inaita nikasema nanii huyu ananisumbua kucheki jina fatma anapiga kama mnavyoufahamu utamu wa bia aisee nikasema huyu demu ngoja nimzimie simu ananisumbua acha nichape gambee[emoji1] nilipiga bia nne pale zote nikawa hoii sasa nikiwa pale kuna mdada mmoja mweupe mzuriii kama malaika akawa ameingia amevaa kigauni kifupi inaonekana amekuja kunywa nae kiukweli akawa amenivutia alikuja akawa amekaa pembeni ya meza yangu akaagiza bia 2 pale kwa muhudumu sasa muhudumu alipomletea bia zake yule dada akampa mimi nikamuita muhudumu nikamwambia weweee muhudumuuuu mpe dada huyo bia 2 zingine helaaa nalipaa yule muhudumu akaenda akaleta bia hizo mbili na kumkabidhi yule dada yule dada akanigeukia akaniambia ahsante kakaangu nikamwambia dada mrembo samahani naweza kujumuika na ww hapo mezani akaniambia sawa njoo basi nikahama meza na kwenda kwa yule dada tukawa tunapiga stori yeye anapiga gambe yule dada alikuwa nu mzurii mno sijapata kuona katikati ya stori nikamwambia nimekuelewa aisee dada mzuri unaishi wapi akanijibu naishi mtaani x jibu liliponipa shaka mtaa alionitajia ndio mtaa ninaoishi mimi nikamwambi kumbe tunaishi wote mtaa mmoja? Akasema inapendeza kusikia hivyo then akaniuliza upo single? Nikamwambia ndio nipo nipo single akaniuliza tena upo single ww hauna mtu kwani?

Nikamwambia sina mtu hauniamini akachekaaa sana akasema sawa nyie wanaume bhana haya mimi nimekukubalia jibu lake lilinipa furaha sana sikujua kwann alicheka sana kutokana nilikuwa nimeelewa tungi basi kufupisha stori nilifanikiwa kuondoka na yule dada hadi kwake aliniambia twende kwangu nikawa nimekubali maana alisema anaishi mwenyewe kweli tukafika kwake kurudi nyuma ni kwamba huyo dada alikuwa na gari lake so ililaisisha usafiri kama dk 30 tukawa tumefika kwake ni bonge moja la mgheto cha ajabu mtaa tulioenda ni karibia na mtaa wangu lakini ilo gheto nilikuwa sijawahi kuliona ila kutokana na pombe sikutia mashaka kweli tukaiingia ndani ni nyumba kubwa anasemq anaishi mwenyewe akanikalibisha vizuri nikiwa nimekaa kwenye sofa akaniomba aende kuoga nikawa pale kwenye sofa baada ya dk30 akarudi pale alivaa khanga tu akaja akaa karibu yangu aisee mtoto alikuwa mzuri mno akawa ananitazama usoni ananiambia kwangu umepapenda mimi ndio basi tukiwa katika stori ananishika shika akaniambiia unajua nakupenda sana yaani shukuru upendo nilioanao kwako kuna kitu kibaya ningekufanyia sema tu basi nashindwa meneno yake yalinishtua nikamuuliza unaaminisha nini akacheka sana akaniambia ina maana haujui mimi ni nani hadi mda huu?

Swali lake likanitisha sana nikiwa natafakari ghafla taa zikazima kama dk 1 ghafla taa zikawa nikamuona amegeuka amekuwa fatma nikiwa nashangaa shangaa natetemeka ndugu msomaji mkojo ulinitoka mnoo fatma safari hii alikuja akiwa amekasirika sana machoni mwake alikuwa ana macho mekundu mno akasema leo ndio ulikuwa mwisho wa maisha yako sema una bahati sana nakupenda ila umenikasirisha mno nikamuuliza ina maana ww ni jini?

Akasema mimi ni jini mimi ni jini niliokupenda ww toka upo mdogo hadi leo nikajiuliza sana akaendelea kusema umeniudhi kunywa pombe kufanya mambo ambayo nilikukataza sasa nilipanga nikupe adhabu kali sana ila kwakuwa ni kosa lako la kwanza na ulikuwa haunijui mimi ni nani nakusamehee kwa leo ndugu msomaji mambo hayo yote yalinitokea ndani ya usiku mmoja sitakuja niiusahau maishani mwangu yote sasa fatma akanisogelea na kuniambia kuwa rasmi mimi na yeye tumeshafunga ndoa toka siku yakwanza tulipokutana kimwili na ni ngumu mimi kumkimbia na akaniambia tayari nina mimba yako na mda sio mrefu nitakupeleka kwetu nikamuuliza huku natetemeka kwanini unanifanyiaa. Hayo yote akacheka sana akaniambia ni stori ndefu ila haya yote amesababisha babu yako nikamuuliza babu yangu unamfahamu ? Umemjuaje akacheka sana akaniambia babu yako marehemu msekwa mimi ndio niliemuua baada ya kunikosea na kunisaliti sana jibu lake lilinipa hofu ghafla .......

WAKUU ITAENDELEA SEHEMU YA 05 SIMULIZI IMEFIKIA PATAMU SASA NIMESHAJUA NIPO KWENYE MAPENZI NA JINI NINI KINAFUATA SOON NAMALIZIA SEHEMU YA 05 NDIO KWANZA TUP0 MWANZO HII SIMULIZI YA UKWELI WA MAISHA YANGU NI NDEFU MNO MWISHO NI SEHEMU YA 28 NDIO NAMALIZA KWAHYO NAOMBENI MZIDI KUNIAZIMA MASIKIO

MUENDELEZO Soma Siku niliyokutana na jini kwenye daladala
 
Iwe chai,iwe ghahawa mi binafsi nimeipenda

Haya Sasa jini Lina mimba yako,ni hatari

Lakini Bora kumpa mimba jini kuliko hivi vifaranga vya mama Samia,ukajikuta unaozea jela[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
SEHEMU YA 04
******************************************
SMS ya fatmah ilinishtua sana na ilisomeka hivi "hello mpenzi wangu naona umeiona huyo zawadi hapo niliyokuwekea kwenye huo mto mwekundu hiyo hela itakusaidia katika shughuli zako nakupenda sana ila usije ukaitumia kwenye mambo yafuatayo ulevi hau starehe za kuhonga wanawake byee",
Sms ya fatma hii aliyonitumia ikanichanganya kwann ameniambia maneno hayo ikabidi nimpigie simu yake lakini wapi kila nikipiga haipatikani nikawa
Kwako hapakua mbali na bar, dem mnatoka mtaa mmoja ila mwendo wa gari iliwachukua dakika 30..sawa ndugu msimuliaji tunaomba sehemu ya 5
 
Back
Top Bottom