Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

SEHEMU YA 08
****************************************
Ilipoishia ni pale nimeamka kitandani simuoni yule kijana niliekuwa ninalala nae sasa ikanibidi niamke nimtafute yuko wapi sasa nikatoka nikawq natembea tembea sasa wakati nazunguka zunguka ghafla nikawa nimekaribia mlango wa kutoka nje nikawaona fetty na familia yake wapo nje wamekaa kwenye mkeka kama wana swali lakini cha ajabu walikuwa wamebadilika sura zao nitatisha sana mimi hapo nawachungulia tu nawaona wana masikio kama ya mbuzi mbaya zaidi baabake fetty alikuwa ana mdomo meno yake yametoka nje kama ya mnyama ngili hii kitu ilinishtua sana wao walikuwa hawajaniona lakini cha aiabu nikataka kukimbia ila sasa kila nikitaka kukimbia naona nguvu zimeniishia ghafla nikawa naona sina nguvu nikawa nasikia sauti ikiniambia usiogope ilikuwa ni sauti kubwa mno ikabidi nipoteze fahamu ndugu msomaji nilipoteza fahamu na sikujua kipi kiliendelea zaidi ya kwamba niliposhtuka sikujiona tena nipo katika ile dunia niliona nipo kwenye kitanda nimelala nikashangaa hapa ni wapi ikabidi niinuke nilikuja kutambua kumbe nipo kwangu nimelala ikanibid niwashe simu kucheki majira ndugu msomaji ilikuwa ni usiku wa saa kumi na moja nikajiuliza ina maana yale yote yaliyotokea nilikuwa naota hama ni kweli na nimewezaje kurudi tena duniani? Nikawa na maswali mengi kichwani ghafla wakati natafakari usingizi ukanikamata tena nilishtuka baadae sana tayari pamepambazuka na ilikuwa ni saa nne asubuhi nikaamika kitandani pale mwili wangu ulikuwa umechoka sana sasa nikajisemea mbona nimechoka sana hivi ikanibidi niende bafuni kuoga baada ya kuoga nikatoka nje na kwenda sokoni kununua mahitaji yangu nikiwa sokoni nanunua vitu ghafla simu yangu ikaita na jina ni fettt hallow mume wangu pole kwa uchovu najua unajiuliza maswali mengi kichwani mwako maswali yako yote leo mchana nakuja kukujibu byeee nakupenda yalikuwa ni maneno ya fetty baadae simu ikakatwa duuh nikasema mungu wangu nisaidie tu basi nikaondoka kurudi nyumbani baada ya kununua mahitaji muhimu nilipofika nyumbani pale nilisalimiana na wapangaji wenzangu waliokuwa nje pale mda natoka sikuwaona lakini mmoja wa wapangaji wenzangu akaniambia mbona kijana leo inaonekana una mawazo sana kulikuno? Nikamjibu kwann ?, akasema umetupita hapa asubuhi tumekuita hauitiki na salamu zetu umezikataa ulikaa kimya, nikasema duuuh akaendelea sasa tunashangaa mda huu unatusalimia tena kama vile ndio unatuona mda huu nikasema duuh nisameheeni sipo sawa basi nikaingia ndani pale ila nilishangazwa na maneno yao ina maana niliwapita bila kuwasalimu kweli?
Basi nikapika pika pale chakula nikala baadae nikawa nipo nipo tu mule ndani nilikuwa natafakari sana sasa ghafla simu yangu ikaita kucheki namba ilikuwa ni namba ngeni hallow hey mambo vp? Ilikuwa ni sauti ya kike nikajibu safi nani mwenzangu? Akasema mimi salome ina maana umefutaga nambaangu? Salome gani akacheka akasema salome ex wako uliekuwa unampenda sana nimepata taarifa upo chanika na mimi nimekuja chanika kwa dada natamani siku tuonane aliniiambia hivyo,
Ndugu msomaji huyu salome ni mwanamke niliempendaga sana kipindi nasoma nae shule ya secondary kizuka iliyopo mkoani morogoro ni shule ya jeshi sasa kipindi nipo form 3 ndio niliweza kujuana na salome ni mwanamke mzuri sana ila alieshika dini mno nilitokea kunpenda sana na yeye alinipenda hadi tunamaliza masomo pale tukaja baadae kupotezana na ndio mapenzi yetu yalipokufa pale;
Wooow nikajikuta nimepata furaha kuwasiliana tena na salome basi salome akaniambia nimekutafuta nimepewa nambaako na rfk ako mussa nilikutana nae kanisq la ukonga ibadani akaniambia upo siku hizi chanika lakini nqjua unateseka sana kuna mambo magumu nimeoteshwa kuhusu wewe kama utanishirikisha nitakusaidia?
Yalikuwq ni maneno ya salome maneno yake yakaniogopesha sana kajuaje kama nina magumu napitia? Hau mungu kamuonyesha maana salome ni mtu alieshika dini sasa nikaona hatari inaanza kuja juu yangu nikamwambia sinq magumu yote yote ni ndoto tu unaota ww nikakata simu,
Ndugu msomaji sikutaka tena kuendelea kuwasiliana na salome niliihisi uenda amekuja kuyaharibu mapenzi yangu na fetty nilijikuta tu nimeanza kumchukia salome nikajisemea nafsini huyu kajuaje eeh?
Sasa wakati nipo na mawazo ghafla fetty akanipigia simu hello mume mimi ndio nakuja mda huu hapo nyumbani nikamjibu sawa basi baada ya muda fetty alikuja kweli alikuja na gari dogo haina ya v8 akaja hadi pale ninapopanga majirani walishangaa sana akashuka kila mtu alishangaa sana kumuona fetty na gari leo tena alikuwa anakujaga wanamuonaga ila hakuwahi kuja na gari pale ndio kilichowashangaza sana watu akaingia ndani nilimfungulia mlango akanikumbatia pale alikuwa ananukia manukatoa mazuri sana safari hiyo basi tukawa tumekaa kwenye sofa akaniambia leo nimekuja na gari ilo gari ni gari lako kuanzia sasa duuuh nilishangaa mno akaendelea yale yote uliyokuwa unayafikiria ni kweli mimi na ww tulienda wote ujinini siku ile nyumbani na yale yote uliyoyaona kule sio ndoto ni kweli akanendelea kusema wazaz wangu wamekupenda sana na ili gari baba ndio amekpa kama zawadi kuanzia sasa ni lako ili akandelea ameomba msamahaa kwa kitendo cha siku ile ulichotuona tupo nje pale tulikuwa tunapigwa swala ya kuombea mema juu yangu na ww ili ulituona tukiwa katika maumbile tofauti uliyotuzoea najua uliogopa sana akasema ila usijali lakini pia tuna vita kubwq sana,
Nikqmuuliza vita gani?
Akasema salome ndio adui yetu sasa
Maneno haya yalinishtua mno sana
Wakuu nitandelea baadae jioni
Noma sana brother ila Mungu akiamua kumkomboa kiumbe chake hakuna kinachoshindikana
 
SEHEMU YA 03
****************
SIKU ile ilikuwa siku nzuri sana kulionja penzi la Fatumah ni mwanamke mzuri sana kuwahi kumuona katika hii dunia ya watoto wa Adam na Hawa[emoji18]

Basi tuliongea mengi sana na Fatmah siku hiyo alinionyeshea mahaba mazito hadi nikawa najisimemea sasa mke si ndio huyu nimepata kumbe sikujua kuwa nilikuwa nimepatikana[emoji29]

Tulionjoi sana nakumbuka usiku wa siku hiyo ya kwanza ya Fatmah kuja kwangu alinipika wali na kabichi na alinionyeshea upendo mmoja sijawahi pata kwanza alikuwa muda wote yupo kifuani kwangu amejilaza ananiambia maneno matamu mume wangu nashukuru mungu nimekupata wewe ni wangu nitakupa mahaba mazito maneno yake yalikuwa yakinipa faraja nikujua kuwa sasa nimepata mke

Nilihisi dunia ni yangu kufupisha stori siku hiyo ndio ikawa mwanzo wa mapenzi yangu mimi na Fatmah ambae ni jini bila kumjua basi usiku ukapita asubuhi nikiwa nimelala na Fatmah aliniamsha mume mimi leo naondoka naenda kwa dada nikamwambia mbona mapema hapo ilikuwa mida ya saa moja asubuhi nikamwambia kwa dadaako ungeenda hata mchana Fatmah akajifikiria basi akanijibu sawa basi ngoja mimi niamke nioge nikufanyie usafi leo

Basi akaamka pale kitanda ni mwanamke mrembo aisee yaani ukiambiwa kuwa ni jini unaweza bisha mazima basi mimi nikiwa kitandani pale nimejilaza Fetty akawa anaosha vyombo punde si punde akaanza kupika chai katika kitu ambacho kilikuwa kinanipa furaha ni jinsi Fatmah alivyokuwa akifanya kazi yaani ilishukua dk 30 kashapika chai kashaosha vyombo kashaoga kamaliza kila kitu akaja kuniambia amka uoge chai tayari nilishangaa sana nikamuuliza aisee umenishangaza sana yaani wewe mchapakazi mno dk 30 ushamaliza kila kitu akawa anacheka

Basi nikaenda bafuni kakuta maji nimeekewa na sabuni kila kitu kinaoga niliporudi sebuleni nilimkuta amekaa kwenye kitu akawa anatabasamu akaniambia mume umependeza ulivyoloana na maji alikuwa akiniangalia garden love zangu basi nikavaa nguo pale basi Fetty akaniambia mume nina zawadi nataka nikupe nikamwambia nipe tu akaniambia nina hii perfume ni kwaajili yako akanipa nilipoipuliza pale ilikuwa ni perfume yenye manukato makali mno yaani inanukia vizuri sana yeye Fetty akawa anafurahi tu nikamwambia ni nzuri mno ndio maana wewe unanukia vizuri kumbe unatumia perfume hii akasema ndio basi tukanywa chai pale huku tukipiga stori Fetty aliniambia swali moja ambalo lilinipa hofu aliniuliza......

Mimi nataka nizae na wewe watoto halafu nije niishi na wewe hivi karibuni upo tayari?

Swali lake lilinishtua mno ukiangalia na maisha yangu ya kuunga unga ningewezaje kuishi na Fatmah walihali sina kitu nikamjibu natamani niishi na wewe hata leo nizae na wewe pia ila sasa maisha yangu ndio bado najitafuta nilipomjibu hivyo akatabasamu halafu akaniambia usijali kuanzia sasa maisha yako yameshakuwa mazuri niamini mimi na kesho utapata dili la hela nyingi ambalo haujawahi kupata

Maneno yake yalinipa furahaa na kunipa wasi wasi pia nikamuuliza umejuaje?

Akacheka halafu akaniambia nimeota tu jana jambo ndoto sio lazima itimie muda mwingine inaweza kutokea kweli au isitokee jibu lake likanifanya nicheke nikamvuta karibu yangu na kumwambia nakupenda sana ni mwanamke wa kipekee sana huku nikamshika na kumpiga busu moja zito mdomoni mwake utamu wa busu langu ulimfanya Fatmah kulalama na kunishika kwa nguvu huku akiendelea na yeye kujivinjali utamu wa mate yangu mdomoni mwake kitendo kilichofanya wote kuangukia kitandani na sasa game kati ya yanga na simba ikaanza rasmi dimbani kwa mkapa stadium huku refa wa mchezo akiwa ni martin saanya ilipigwa mechi ya karibia masaa 2 bila mapumziko huku sauti ya chaga za kitanda zikisikika kwachuuu kwachuuu kachwuuuu baaada ya muda wote tukajikuta tupo hoii hooi tumechoka

Tukiwa tumetulia kitandani Fatmah akaniambia nakupenda sana nitahakikisha nakupa kila kitu kinachokiweza nikamwambia nitafurahi basi ikabidi twende kuoga na Fatmah asikwambie mtu mahaba tuliyokuwa nayo ni zaidi ya Julliette na Romi basi kufupisha stori baada ya kuoga tukavaa then Fattuma akaniambia sasa anataka kwenda kwa dadaake ila alinisisitiza nisije kumsaliti kwani ananipenda sana aliniambia kuja kwangu tena itachukua siku 3 atakuja tena basi nikamsindikiza hadi mtaa wao anapoishi na dadaake Sakina yule fundi msusi wa saloon maarufu kipindi hicho mtaa x.... Chanika tukaagana na mimi nikawa nimeenda kumcheki mwanangu Juma ni kama kakaangu kwani tumekuwa tukisaidiana kwenye shida na raha alikuwa hakai mbali na mimi bahati nzuri nimefika kwake nimekuta ndio nae amefika kutoka mizunguko yake

ooh kaka mambo vp adimu sana kaka sema una balaa ww juma aliniambia huku anacheka akinikalibisha ndani nikamwambia mimi nipo vp balaa gani tena akacheka sana akaniambia nimepata taarifa zako mtaani sasa hivi una bonge moja la demu mtoto shombe shombe, akaongezea haya buana dunia yako hii sema watoto wazuri wanataka hela nikamwambia ndio ni kweli nimepata tu demu kizali zali bro basi akaniambia ni jambo jema basi tukawa tunapiga stori zingine za kawaida,

Bro juma akaniambia vp madili yako ya ufundi yanaendeleaje?
Nikamwambia daah madili magumu sasa maana nilishagombana fundi mkuu akasema pole sana ila tuzidi kupambana basi tulipiga piga stori pale na bro basi ikabidi nimuage niende magetoni

Basi nikiwa nipo njiani naelekea ghetto nikaona sms imeingia kwenye simu yangu sms ilisomeka ni Fatmah hello mume wangu kwa mapenzi uliyonipa jana na leo nimekuachia zawadi ila ni surprise sikukwambia ipo kwako nenda angalia kitandani kwenye ule mto wa mwekundu utaiona nakupenda,

Sms hiyo ilinishtua sana nikajaribu kumpigia fatmah simu yake haipatikani nikawaza zawadi gani hiyo ikabidi nipige mguu wa haraka kurudi nyumbani huku maswali mengi kichwani nilipofika nyumbani kitu cha kwanza nilipofungua mlango ni kwenda kitandani kuutafuta huo mtu mwekundu kujua kuna nn sikuamini nilipotoa foronya ya mto ndani nilikutana na kitita cha elfu 10 kumi tupu ikabidi nizichukue niziesabu zilikuwa ni shs laki 4 nikashangaa sana ikabidi nijiulize hizi hela zote Fatmah amenipa kwaajili ya nini na kazitoa wapi nikiwa katika wimbi la mawazo nilipigwa na mshangao nilipoona mlio wa simu yangu ikimaanisha kuna sms imekuja ikabidi niusome huo ujumbe alikuwa ni fatmah ujumbe ulionishtua...

Itaendelea usikose sehemu ya 04 kujua nn kiliendelea baada ya kuziona laki 4 nilizopewa na fattmah na je nilipatwa na mshangao gan baada ya kusoma ujumbe ...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Fatumah huyu huyu karume [emoji4][emoji4]
 
Story tellers nawapongeza sana sio kazi ndogo kuwaza, kutunga ,kuipangilia na kuiwasilisha story katika uhalisia kama huu...yaani unasoma story huku unajenga taswira kichwani hatua baada ya hatua...

NB
Mnaojifanya investigators na wajuaji, tungeni za kwenu kama mnaona ni kazi rahisi. Jifunzeni kuthamini kazi za wenzenu, mafamba nyie. Ikikuuma chomoa.
 
Nimeacha kusoma baada ya kuskia ktk nyumba ya majini kuna flat screen[emoji2][emoji2]. Majini wana kisimbuzi gani sasa.
SEHEMU YA 07
********************************
#ILIPOISHIA#
Ni pale nilipojikuta nipo katika ulimwengu nisioulewa nimezungukwa na watu waliokuwa wamevaa mavazi meupe wote nilishtishwa na sauti iliyokuwa inajirudia rudia kama sauti ya mwangi iliniambia karibu ni miongoni mwa wale watu waliokuwa wamenizunguka pale,basi nikainuka pale chini nilipokuwepo nilikutana na fetty miongoni mwa hao watu waliokuwa wamenizunguka pale nae alikuwa amevaa mavazi meupe kama wenzie akaniambia karibu nyumbani hawa ni ndugu zangu wamefurahi kukuona leo usiwaogope basi walikuwa ni mmama mmoja wa makamo pamoja na mzee mmoja wa makamo pamoja na fetty na kijana mmoja inaonekana hii ndio ilikuwa familia ya fetty basi yule mzee wa makamo akaongea huku sauti ikiwa kama inajirudia kuwa nisiogope yeye ni babaake fetty na yule mama wa makamo ni mke wake yaani mama fetty yule wale wengine ni watoto wake yaani fetty na yule mwingine karibu sana kuwa na amani basi nikasema ahsante,
Ndugu msomaji nilishangaa sina uoga nawaona kama watu wa kawaida tu basi wakaanza kunipeleka kwao sasa hapo nilikuwa nipo sehemu tofauti na dunia yetu sasa kipindi tunatembea nilishuhuudia majengo mazuri sana sijawahi kuona ulikuwa ni mji mmoja mzuri mno yaani ni kama ulaya maghorofa kila mahali sasa cha ajabu kila tuliekuwa tunakutana nae njiani wale wapita njia walikuwa wakinishangaa mimi fetty akasema wale ni majini kama sisi wanakushangaa ww binadamu ila usiogope hawawezi kukudhulu mimi tayari nilishakuwekea ulinzi hakuna jini lolote linaloweza kukudhuru,
Fetty alikuwa akiniambia hivyo wakati tunatembea sasa kitu cha ajabu nilichokuja kukiona ni pale wakati tunatembea kulekea kwa kina fetty tupo tumeongozana na familia yake katika ule mji wa ajabu nisiojua ni tulipokutana na mtu mmoja ana mgui mmoja ana masikio kama ya mbuzi alikuwa anaendesha piki piki yule mtu aliniogopesha sana kiasi nilitamani kukimbia fetty akaniambia usiogope yule ni kama sisi tu yeye leo ana adhabu amepewa ndio maana unamuona hivyo nikamuuliza adhabu gani akasema nitakwambia tu basi baada ya dk 30 tukafika kwenye jumba moja kubwa na hapo mlango yaani geti la ile nyumba ukajifungua wenyewe tukawa tumeingia ndani yule baabake fetty akasema karibu sana nyumbani kijana safari hii sauti yake ilikuwa haijirudia rudii kama mwanzo basi tukaingia ndani ni nyumba nzuri sana kuna masofa na flat screen ndugu msomaji katika ile dunia ya ujinini ni kuwa majini kumbe na wao wanaishi kama sisi binadamu japo hii dunia yao ipo chini ya bahari maana fetty alikuja kunieleza baadae basi nilikaribishwa vizuri sana walipika chakula nikala safi kabisa basi usiku. Yule mzee na mamaake fetty na fetty mwenyewe waliniita kwenye sofa na kuanza kunipa kikao kikao kilikuwa hivi yule mzee aliniambia amefurahi mwanae kuja kunitambulisha pia mwanae kamwambia ana mimba na yeye kama baba ametoa baraka zote ila aliniambia kuwa kama nimempenda mwanae nisije kwenda kinyume kwani usalama wangu utakuwa ni mdogo nae mamaake fetty akaongezea kuwa yeye amenipenda ni kijana mpole sana hana neno zaidi ya kunitakia maisha mema na mwanae pia akasema yeye ananipa zawadi ya pete hii pete itakuwq kama ulinzi wangu dhidi ya majini mabaya yatakayo taka kunidhulu akae delea kusema hapa mtaani kwetu kuna majini mabaya tayari yameshauona ujio wangu na nisipokuwa na ulinzi wa kutosha yatanidhulu ila nisijari nipo salama sasa basi ni mengi waliniambia na atimae usiku ukapita nilienda kulala nirudi nyuma siku ile nilipelekwa chumba kimoja nilale na yule kakaake fetty ambae aliniambia jina lake kuwa anaitwa abdulkarim basi nililala na yule kakaake fetty usiku ukapita sasa asubuhi wa siku ya pili nilipoamka nilimkuta yule kakaake fetty simuoni kitandani nikashtuka sana ikanibidi nitoke nje sasa wakati natoka nje niliufikia mlango wa nje sasa kama mungu tu kuna kitu kikaniambia angalie nje pale nilipopiga jicho nje sikuamini sikuamini ndugu msomaji kwa nilichokiona nusu nikimbie
Niwaona fetty baaabake na mamaake na yule kakaao wamekaa kwenye mkeka kama wanaswali ila walikuwa na sura zinazotisha mno walikuwa wana masikio ya mbuzi miguuni mwao wana kwato za ng^ombe na yule babaao alikuwa akiendeleza swala meno yake yalikuwa yametoka nje kama meno ya mnyama ngili niogopa sana nilitetemeka nikataka kukimbia lakini ghafla mwili wangu nikauona umeishiwa nguvu ghafla nikasikia sauti ikiniambia.......

Wakuu itandelea kesho asubuhi saa sita sehemu inayofuata sitasahau katika maisha yangu
 
Mkuu funguka kidogo
Niliwahi weka humu zaidi ya miaka nane, (nafupisha sana) kwangu ilikuwa tofauti. yeye ili nionane nae lzm nilale usingizi ndio nakuwa nae ilifika mahali hata stand ya basi nitasinzia kama anataka tuwe wote uzuri hakuna wa kusumbua wala kuniibia.

Kuna mahali nilikuwa nafanya kazi nikamwambia mlinzi wa wapo khs hii hali akaniambia atanisaidia dawa.

Siku hiyo ilikuwa ugomvi na vita kubwa na yeye wkt huo sasa hata nikiwa macho naweza kujua anakuja ila inabidi nikae mahali nitulie ndio aje.

Alinilaumu sana kwa maamuzi nayotaka kufanya na kuwa nisifanye hivyo maana ananipenda sana.

Na alinipeleka sehemu nyingi (kiuhalisia kuna mambo mengi yanaendelea ktk huu ulimwengu hatuyaoni) mahali napoishi nimewahi kupelekwa hadi chini ya ardhi kuonyeshwa yanayoendelea na baadhi ya maeneo waliyopo wana tekinilogia kubwa hata binadamu wa kawaida hajafikia.

Sasa ile dawa alinipa yule mzee ilikuwa ya kuweka kwenye maji na kuoga, akasema ndani ya siku saba lazima atakuja kukuaga ila utapitia magumu usiogope.

siku ya pili alikuja na wadada wenzake kama wanne wakanichukua wakanipeleka juu sana angani akaniambia huu ndio mwisho wako nakuachia hapa, nikamsihi asifanye hivyo wenzake wakaniambia kwa nini lkn namkataa mwenzao nikasema naomba tu tuachane kwa amani. aliniangalia kwa hasira hakusema chochote nikaamka nipo poa na biashara iliishia hapo ingawa nilivyomwambia yule mzee alizema endelea kutumia dawa hadi siku saba.

kiukweli ni mwanamke mzuri kuwahi kutokea na kuna wakati huwa namwaza kwani kuna kilele nilikuwa nafikia sijawahi kukipata ila alifanya nikikutana na demu uume hausimami alafu nikiachana na huyo binti nae anakuja ananiambia kwani mimi sikutoshi hadi utafute wanawake wengine? nikaona hapa sasa nadhalilika.
 
Nimeacha kusoma baada ya kuskia ktk nyumba ya majini kuna flat screen[emoji2][emoji2]. Majini wana kisimbuzi gani sasa.
haya mambo kwa aliyekutana nayo anaelewa vzr tofauti na hapo unakuwa unaona kama furahisha genge ndio maana hadi wengine wanasema amka usingizini.

kiuhalisia mahali ulipo kuna shughuli nyingi sana zinaendelea ila huwezi kuziona na uwezo wa hawa viumbe binadamu wa kawaida bado hajaufikia hata robo.

pia tofautisha sana kati ya majini na wachawi.
 
niliwahi weka humu zaidi ya miaka nane, (nafupisha sana) kwangu ilikuwa tofauti. yeye ili nionane nae lzm nilale usingizi ndio nakuwa nae ilifika mahali hata stand ya basi nitasinzia kama anataka tuwe wote uzuri hakuna wa kusumbua wala kuniibia.
Teh basi hapo ukute ulimuacha kisa tu hauna uhuru wa kuchepuka na wanawake wengine. Wanaume bana.
 
Back
Top Bottom