niliwahi weka humu zaidi ya miaka nane, (nafupisha sana) kwangu ilikuwa tofauti. yeye ili nionane nae lzm nilale usingizi ndio nakuwa nae ilifika mahali hata stand ya basi nitasinzia kama anataka tuwe wote uzuri hakuna wa kusumbua wala kuniibia.
kuna mahali nilikuwa nafanya kazi nikamwambia mlinzi wa wapo khs hii hali akaniambia atanisaidia dawa.
siku hiyo ilikuwa ugomvi na vita kubwa na yeye wkt huo sasa hata nikiwa macho naweza kujua anakuja ila inabidi nikae mahali nitulie ndio aje.
alinilaumu sana kwa maamuzi nayotaka kufanya na kuwa nisifanye hivyo maana ananipenda sana.
na alinipeleka sehemu nyingi (kiuhalisia kuna mambo mengi yanaendelea ktk huu ulimwengu hatuyaoni) mahali napoishi nimewahi kupelekwa hadi chini ya ardhi kuonyeshwa yanayoendelea na baadhi ya maeneo waliyopo wana tekinilogia kubwa hata binadamu wa kawaida hajafikia.
sasa ile dawa alinipa yule mzee ilikuwa ya kuweka kwenye maji na kuoga, akasema ndani ya siku saba lazima atakuja kukuaga ila utapitia magumu usiogope.
siku ya pili alikuja na wadada wenzake kama wanne wakanichukua wakanipeleka juu sana angani akaniambia huu ndio mwisho wako nakuachia hapa, nikamsihi asifanye hivyo wenzake wakaniambia kwa nini lkn namkataa mwenzao nikasema naomba tu tuachane kwa amani. aliniangalia kwa hasira hakusema chochote nikaamka nipo poa na biashara iliishia hapo ingawa nilivyomwambia yule mzee alizema endelea kutumia dawa hadi siku saba.
kiukweli ni mwanamke mzuri kuwahi kutokea na kuna wakati huwa namwaza kwani kuna kilele nilikuwa nafikia sijawahi kukipata ila alifanya nikikutana na demu uume hausimami alafu nikiachana na huyo binti nae anakuja ananiambia kwani mimi sikutoshi hadi utafute wanawake wengine? nikaona hapa sasa nadhalilika.