Zaidi ya kukubaliana kanuni (za majadiliano), kuna kitu cha msingi (substantive issue) ambacho CHADEMA na CCM wanaweza kukubaliana ili kuenzi umoja wa kitaifa? Ningependa kufahamishwa hata kimoja tu.
Nivuavyo, CCM hawataki uwepo wa chama cha upinzani makini (serious) kiasi cha kudhamiria kupambania hatamu za dola - kwa dhati. Lengo kuu ni CCM iendelee kuwa madarakani na kuendesha nchi kwa mtindo wa “state party dictatorship” ambapo maagizo ya Rais/Mwenyekiti wa CCM ndio yanakuwa sheria kuu ya nchi.
Tangu 2010, CHADEMA imejipambanua kuwa mwiba na changamoto kubwa sana kwa uwepo na ukuu wa CCM. 2015, Magufuli alidhani akijidai kutekeleza “ajenda za CHADEMA” hasa ya ufisadi basi watahamia kwake na chama hicho kitakufa. Badala yake wakamwashia moto wa kudai demokrasia, haki za binadamu, katiba na tume huru! Akaghadhibika na kupania kuwaua kichama hata “literally”!
Baada ya JPM kaja Mama SSH na hatua za “kuondoa dhulma” na kurejesha uhuru wa shughuli za kisiasa na habari. CHADEMA wakamshukuru lakini hapohapo wakamshushia nyundo ya “katiba mpya”. Wamegusa “roho ya CCM”. Matokeo yameonekana.
CHADEMA wajiandae kwa mapambano makali katika mazungumzo na CCM kama wamedhamiria kuhakikisha msimamo wao haubadiliki. Wajue wakuu huko chama tawala wanatamani kuwaambia:”guys, why don’t you just name your price, play dead and drop out?”