Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio maana ICC watakuwepo uchaguzi huu kukusanya ushahidi kabisa sio wategemee serikali iwape ushahidi ili kuepuka yaliyotokea Kenya kuficha ushahidi.
siku tano za kampeni: Yafuatayo yanaonesha dhahiri kuwa vyombo vya ulinzi na usalama na mamlaka za serikali zinashirikiana na ccm kujaribu kuharibu uchaguzi huu;
1. Kumzuia mgombea urais wa chadema/ukawa kuhudhuria msibani eti kwa sababu amesindikizwa na watu, kana kwamba watu walewale kwa idadi ileile wangekwenda wenyewe wangeleta madhara yoyote. Najiuliza tu, ingekuwaje mgombea na watu wale wangelazimisha kwenda msibani; jibu: Mapambano na polisi, mgombea kukamatwa na kufunguliwa kesi, wafuasi kujeruhiwa kwa risasi, kuuawa ama kukamatwa.
2. Kupiga marufuku maandamano na mbwembwe za kuwasindikiza wagombea kurejesha fomu. Hili lilifanywa mara baada ya magufuli na lowassa kwenda kwa maandamano lakini yale ya lowassa yakionekana kuwa na maelfu mengi ya watu zaidi kuliko ya magufuli. Lakini pamoja na marufuku hiyo majuzi nimejionea wafuasi wa ccm wakiandamana kutoka manzese hadi jangwani wakiwa na masaburi, bila polisi kuwazuia.
3. Kuzuia mgombea wa ukawa/chadema kufanya ziara maalum za kushtukiza kuwatembelea wananchi wa kawaida. Hizi zinapigwa marufuku kwa mgombea huyu wakati wale wa ccm wakifanya watakavyo. Mfano ni bi. Samia suluhu alivyoonekana moshi akiacha ratiba ya ziara na kutembelea raia mtaani bila kukatazwa na polisi.
4. Kuzuia ukawa kufanya mkutano wake wa uzinduzi uwanja wa taifa na hata ukawa ilipoamua kufanyia mkutano huo katika viwanja wa jangwani umezuiwa na manispaa ya ilala nadhani kwa shinikizo la ccm chini ya sababu dhaifu sana kwamba kuna watu wameshaukodi, ni halmshauri ipi hivi sasa ambayo ina-prioritize shughuli zingine kwenye viwanja vikubwa wakati vyama vya siasa viko kwenye uchaguzi mkuu jambo ambalo ni kipaumbele cha taifa kwa sasa?
5. Ccm kufanya mkutano wake wa uzinduzi hadi saa 12.38 jioni tena mbele ya mkuu wa nchi na viongozi wote wa serikali wakati wanajua fika kuwa sheria inawataka kufunga mkutano saa 12.00 jioni. Kwamba ccm na inavionesha vyama vingine kuwa iko juu ya sheria na kwamba wengine wakiiga watajiju. Na baada ya kupitisha muda huo ccm inamshinikiza mkurugenzi wa manispaa ya ilala aandike barua nec kuijulisha kuwa ni yeye ndiye alielekeza mkutano uendelee hadi muda huo (very illogical reason).
6. Rais mstaafu wa awamu ya 3 benjamin william mkapa kusimama hadharani na kuwatukana wapinzani kuwa ni "malofa na wapumbafu". Mpumbavu ni neno kali na lina maana ya "juha", "zuzu", "mtu asiyejielewa", "-----", "----", n.k. Wakati mkapa akitukana hivyo hadharani na kuachwa juu ya sheria, lawrence masha ambaye ni mwana ukawa (hivi sasa) lakini zamani akiwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ya tanzania, yeye amekamatwa na kuwekwa rumande na kunyimwa dhamana (inacheleweshwa kimakusudi) kwa "kosa" la kumtukana askari polisi (wengi kama sikosei) kwamba ni "washenzi", "wasio na shukrani na wasio na dini". Kwamba kwa tafsiri ya ccm na serikali yake pamoja na vyombo vinavyosimamia sheria (polisi), neno "upumbavu na ulofa" siyo tusi lakini neno "ushenzi na kutokuwa na shukrani" ni tusi baya sana.
Hayo mambo sita niliyoyataja na mengine kadhaa ni dalili tosha kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaweza kuishia mahali pabaya. Hadi sasa sijaona chokochoko kutoka upande wa ukawa, hii ina maana kwamba hizi za ccm, vyombo vya dola na mamlaka za serikali zikiendelea na zikawa zinahujumu kwa dhahiri maslahi ya upinzani na ukawa, lolote lile linaweza kutokea.
mod;
angalia kichwa cha habari hapo juu,
badilisha ; jf inatumika vibaya
Chadema imeshauzwa. Kuna kila dalili kuwa mnunuzi wa Chadema anataka kuibadilisha iwe kikundi cha sanaa...
SIKU TANO ZA KAMPENI: YAFUATAYO YANAONESHA DHAHIRI KUWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZINASHIRIKIANA NA CCM KUJARIBU KUHARIBU UCHAGUZI HUU;
Na. Julius Mtatiro.
1. Kumzuia mgombea urais wa CHADEMA/UKAWA kuhudhuria msibani eti kwa sababu amesindikizwa na watu, kana kwamba watu walewale kwa idadi ileile wangekwenda wenyewe wangeleta madhara yoyote. Najiuliza tu, ingekuwaje mgombea na watu wale wangelazimisha kwenda msibani; JIBU: Mapambano na Polisi, mgombea kukamatwa na kufunguliwa kesi, wafuasi kujeruhiwa kwa risasi, kuuawa ama kukamatwa.
2. Kupiga Marufuku maandamano na mbwembwe za kuwasindikiza wagombea kurejesha fomu. Hili lilifanywa mara baada ya Magufuli na Lowassa kwenda kwa maandamano lakini yale ya Lowassa yakionekana kuwa na maelfu mengi ya watu zaidi kuliko ya magufuli. Lakini pamoja na marufuku hiyo majuzi nimejionea wafuasi wa CCM wakiandamana kutoka Manzese hadi Jangwani wakiwa na MASABURI, bila polisi kuwazuia.
3. Kuzuia mgombea wa UKAWA/CHADEMA kufanya ziara maalum za kushtukiza kuwatembelea wananchi wa kawaida. Hizi zinapigwa marufuku kwa mgombea huyu wakati wale wa CCM wakifanya watakavyo. Mfano ni Bi. Samia Suluhu alivyoonekana Moshi akiacha ratiba ya ziara na kutembelea raia mtaani bila kukatazwa na Polisi.
4. Kuzuia UKAWA kufanya mkutano wake wa uzinduzi Uwanja wa Taifa na hata UKAWA ilipoamua kufanyia mkutano huo katika viwanja wa JANGWANI umezuiwa na Manispaa ya Ilala nadhani kwa shinikizo la CCM chini ya sababu dhaifu sana kwamba kuna watu wameshaukodi, Ni halmshauri ipi hivi sasa ambayo ina-PRIORITIZE shughuli zingine kwenye viwanja vikubwa wakati vyama vya siasa viko kwenye uchaguzi mkuu jambo ambalo ni kipaumbele cha taifa kwa sasa?
5. CCM kufanya mkutano wake wa uzinduzi hadi saa 12.38 jioni tena mbele ya Mkuu wa nchi na viongozi wote wa serikali wakati wanajua fika kuwa sheria inawataka kufunga mkutano saa 12.00 jioni. Kwamba CCM na inavionesha vyama vingine kuwa iko juu ya sheria na kwamba wengine wakiiga watajiju. Na baada ya kupitisha muda huo CCM inamshinikiza Mkurugenzi wa manispaa ya ILALA aandike barua NEC kuijulisha kuwa ni yeye ndiye alielekeza mkutano uendelee hadi muda huo (very illogical reason).
6. Rais mstaafu wa awamu ya 3 Benjamin William Mkapa kusimama hadharani na kuwatukana wapinzani kuwa ni "MALOFA na WAPUMBAFU". Mpumbavu ni neno kali na lina maana ya "juha", "zuzu", "mtu asiyejielewa", "-----", "----", n.k. Wakati Mkapa akitukana hivyo hadharani na kuachwa juu ya Sheria, Lawrence Masha ambaye ni mwana UKAWA (hivi sasa) lakini zamani akiwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Tanzania, yeye amekamatwa na kuwekwa rumande na kunyimwa dhamana (inacheleweshwa kimakusudi) kwa "kosa" la kumtukana askari polisi (wengi kama sikosei) kwamba ni "washenzi", "wasio na shukrani na wasio na dini". Kwamba kwa tafsiri ya CCM na serikali yake pamoja na vyombo vinavyosimamia sheria (POLISI), neno "Upumbavu na Ulofa" siyo tusi lakini neno "Ushenzi na Kutokuwa na shukrani" ni tusi baya sana.
Hayo mambo sita niliyoyataja na mengine kadhaa ni dalili tosha kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaweza kuishia mahali pabaya. Hadi sasa sijaona CHOKOCHOKO kutoka upande wa UKAWA, hii ina maana kwamba hizi za CCM, VYOMBO VYA DOLA NA MAMLAKA ZA SERIKALI zikiendelea na zikawa zinahujumu kwa dhahiri maslahi ya UPINZANI na UKAWA, lolote lile linaweza kutokea.
Julius Sunday Mtatiro,
Dar Es Salaam.
Dawa yako Humphrey Polepole, unamuogopa kama nyuki
Huku ikwiriri tulishajipanga kuja kwenye ufunguzi wa mkutano kwa gharama zetu na vihiace kama 8 na mabango yetu. Hatuvunjiki nguvu
Wananchi wamepandwa na hasira sana,
Kila kona ukipita mazungumzo ni hayohayo,kwamba ukawa wameanza kufanyiwa hila na fitina mapemaa,hii ni hofu za chama dola.Enyi chama dola kwenye vikao vyenu iwe vya siri au vya wazi kuhusu nia yenu ya umwagaji damu katika nchii hii ya Tanzania,mshindwe katika jina la Yesu kristo wa Nazareti aliye hai.
Katika madhabahu zenu zote mnazodaiwa damu iwe za Albino au za ajali ambazo mmeshindwa kutimiza na kutaka kusababisha mauaji ya Kimbari mshindwe katika jina la Yesu.
Damu ya Yesu inenayo mema inene kinyume na mabaya yote katika ardhi hii ya Tanzania inayolia sababu ya damu zisizo na hatia.
Ee Mungu baba kwa yeyote aliye wahi kumwaga damu ya mtanzania kwa hila, kwa mauaji ya albino na ajali za namna nyingine yeyote,na kwa wenye nia ya kumwaga damu kwenye nchii hiii.
Tunakuomba Yehova Mungu mkuu,damu hiyo iwe juu ya vichwa vyao wenyewe,pamoja na familia zao kama ilivyotokea katika nyumba ya Sauli.Kwa wanaoandaa mashimo ya kuzika watanzania ee Mungu tunakuomba kwenye mashimo hayo waingie wenyewe.
Amen
Dalili za chama cha Mapinduzi kusababisha vurugu katika uchaguzi mkuu zimeanza kuonekana mapema kutokana Na vikwazo vinavyowekwa Na watendaji Wa serikali.Vikwazo hivyo in pamoja Na kuvizuia vyama vya Upinzani kufanya mikutano yao katika viwanja vya Umma.Tunaishauri CCM kwa namna moja au nyingine iache kutumia mbinu hizi chafu kwa wananchi wakikosa uvumilivu watataka kuzizuia kwa nguvu Na kusabisha uvunjifu Wa amani.Ni vema kampeni zikaendelea bila hujuma zozote.