Habari za jioni ndugu watanzania wenzangu..!
Salam salamu ndugu mheshiniwa Rais.
Sitaki nimwambie mtu yeyote yule ila maoni na mtazamo wangu uende moja kwa moja kwa rais wa nchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mh. Rais kama kweli ni rais mwenye dhamana ya kuongoza nchi hii kwa mjibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania unalo jukumu la kuwaongoza wananchi wa taifa hili bila misingi ya ubaguzi au upendeleo wa aina yeyote.
Vitendo tunavyoshuhudia katika mwanzo wa kampeni za uchaguzi haviashirii amani wala aina yeyote ya umoja wa kitaifa ambao tumekuwa nao kwa muda miaka zaidi ya hamsini.
Kunyimwa uhuru wa kidemocrasia itakuwa ni moja ya makosa makubwa yatakayorigharimu taifa hili lenye tunu ya amani tuliyorithishwa na mzee wetu hayati baba wa tiafa mwl.j.nyerere.
Kitendo cha kuwanyima upinzani uhuru wa kufanya mikutano sehemu za umma kama viwanja vya taifa, jangwani, kuzuia mikusanyiko ya siasa, kukmata watu, kupiga watu mabomu hakiwezi kuiweka nchi yetu katika hali ya kuitunza tunu ya amani nchini. Na pia kinapelekea kuligawa taifa katika vipande vipande.
Ukiwa kiongozi wa nchi na mwenye dhamana ya kila mtanzania kuwa huru, salama na haki za kiraia ujue unayo dhamana ya kuhusika na kila madhara yatakayo mpata mtu yeyote na taifa kwa ujumla.
Tatizo la haya yote ni hofu ya mabadiriko hasa ya uongozi kwa serikali na chama tawala ila nikukumbushe mh. Rais chukua muda kujifunza kwa baba wa taifa mwaka 1992 juu ya vyama vingi ambapo maoni ya wengi yalionesha kutokukubali vyama vingi. Ila busara ya mzee nyerere nakuona nguvu ya mabadiriko ambayo katika zama zote hajawahi kushindwa alimua kukubali vyama vingi.
Mabadiriko yanayoonekana kuwatia hofu watawala kwa maana ya rais na taasisi ya za chini ya ofisi ya rais wanaamini yamachagizwa na vyama vya upinzani hili ni kosa la kwanza kwa kipngozi makini huitaji kutumia njia za kisayansi kujua kinachochagiza mabadiriko. Nitataja chache hapa chini:-
Wananchi kukata tamaa na maisha hasa kufuatia hali duni za maisha na kutokuwepo mipango thabiti ya kuwakwamua kwa adui huyu namba moja UMASIKINI.
Kingine tabia ya jamiii kubadirika na wakati kufuatia maendeleo ya sayansi na technology uwepo wa mawasiliano ambapo sasa mtu anaweza kujifunza mambo mbalimbali kote duniani kunapelekea mahitaji ya jamiii kimabadiriko kuongezeka na watu hawaoni serikali ikibadirika kuwapatia mahitaji yao mfano utasikia serikali ikijiringanisha na MKOLONI huku ikisahau watu wanajipima na nchi zinazoebdelea.
Mwisho niombe kwa viongozi wenye dhamana ya nchii hii kwa kuanza na RAIS, JESHI, MAHAKAMA na USALAMA WA TAIFA na taasisi nyingine ndogo ndogo za kisekta zenye dhamama katika uchaguzi huu mkuu kuwa sawa maana bila haki au matumizi yeyote ya nguvu kupoka haki ya kidemocrasia hayayaacha taifa hili likiwa salama. Viongozi wenye dhamana hasa wastaafu waache watumizi ya lugha za kuudhi na kebehi kama alivyofanya mzee MZEE MKAPA.
Mwisho nikukumbushe mh. Urejee na kuifanyia kazi kauli yako SOTE TUNAJENGA NYUMBA MOJA (TANZANIA) KWANINI TUGOMBANIE FITO. na busara ile ile ya uliyo waambia wanaccm dodoma kuwa CHAMA KWANZA MTU BADAE itumike pia hapa TAIFA KWANZA (TANZANIA) ALAFU CHAMA(CCM) BADAE. iwapo ccm ikishindwa Tanzania itabaki ile ile na UKAWA au vyama vingine vikishindwa Tanzania itakuwepo vilevile.