Elections 2015 Siku tano za kampeni: Chokochoko za CCM, serikali yake na vyombo vya ulinzi

Elections 2015 Siku tano za kampeni: Chokochoko za CCM, serikali yake na vyombo vya ulinzi

Chadema imeshauzwa. Kuna kila dalili kuwa mnunuzi wa Chadema anataka kuibadilisha iwe kikundi cha sanaa...
hivi wewe ndiye ZeMarcopolo yuleyule mjenga hoja wa zamani au hizi id nazo zikikaa muda mrefu bila kutumika anapewa mtu mwingine kama zilivyo line za simu ?
 
Segerea umepita lakini kugombea kwa mwavuli wa ukawa??????????????????

Sio baadae unaanza kukandya , ukawa.

Maliza yako ; ndo ulete hizi porojo
 
Mtatiro acha kuchochea vurugu Tanzania tambua kuwa amani ikivurugika utakuwa sehemu ya washitakiwa ICC The Hague.

Kwani hayo aliyoyaorodhesha hayajatokea. Unafikiri ICC wanafedha za mchezo za kuendeshea kesi za kipuuzi kama unayojisadikisha?
 
Nilikuwa sijui kuwa machafuko yanaanzaje kwenye nchi, sasa ninachokiona Tanzania tunaelekea hukohuko.
 
Julius Nakushukuru mno kwa kuweka wazi nia ovu ya chama tawala. Ningeomba sana tufanye kila namna kuwafikia wananchi wote kwa matangazo au kwa mikutano na kuwaeleza uovu unaofanywa na vyombo vya umma kuilinda serikali dhalimu ya ccm. na tuwahamasishe kwamba wakiendelea kutubania basi wananchi watumie vyema vichinjio vyao na tuwachinjie baharini oktoba 25. TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA OKTOBA 25. TULIANZA NA MUNGU, TUPO NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU.SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU..UDUMU UKAWA...VIDUMU CDM CUF NCCR NA NLD KWA KUTUONYESHA NJIA.
SIKU TANO ZA KAMPENI: YAFUATAYO YANAONESHA DHAHIRI KUWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZINASHIRIKIANA NA CCM KUJARIBU KUHARIBU UCHAGUZI HUU;


Na. Julius Mtatiro.


1. Kumzuia mgombea urais wa CHADEMA/UKAWA kuhudhuria msibani eti kwa sababu amesindikizwa na watu, kana kwamba watu walewale kwa idadi ileile wangekwenda wenyewe wangeleta madhara yoyote. Najiuliza tu, ingekuwaje mgombea na watu wale wangelazimisha kwenda msibani; JIBU: Mapambano na Polisi, mgombea kukamatwa na kufunguliwa kesi, wafuasi kujeruhiwa kwa risasi, kuuawa ama kukamatwa.


2. Kupiga Marufuku maandamano na mbwembwe za kuwasindikiza wagombea kurejesha fomu. Hili lilifanywa mara baada ya Magufuli na Lowassa kwenda kwa maandamano lakini yale ya Lowassa yakionekana kuwa na maelfu mengi ya watu zaidi kuliko ya magufuli. Lakini pamoja na marufuku hiyo majuzi nimejionea wafuasi wa CCM wakiandamana kutoka Manzese hadi Jangwani wakiwa na MASABURI, bila polisi kuwazuia.


3. Kuzuia mgombea wa UKAWA/CHADEMA kufanya ziara maalum za kushtukiza kuwatembelea wananchi wa kawaida. Hizi zinapigwa marufuku kwa mgombea huyu wakati wale wa CCM wakifanya watakavyo. Mfano ni Bi. Samia Suluhu alivyoonekana Moshi akiacha ratiba ya ziara na kutembelea raia mtaani bila kukatazwa na Polisi.


4. Kuzuia UKAWA kufanya mkutano wake wa uzinduzi Uwanja wa Taifa na hata UKAWA ilipoamua kufanyia mkutano huo katika viwanja wa JANGWANI umezuiwa na Manispaa ya Ilala nadhani kwa shinikizo la CCM chini ya sababu dhaifu sana kwamba kuna watu wameshaukodi, Ni halmshauri ipi hivi sasa ambayo ina-PRIORITIZE shughuli zingine kwenye viwanja vikubwa wakati vyama vya siasa viko kwenye uchaguzi mkuu jambo ambalo ni kipaumbele cha taifa kwa sasa?


5. CCM kufanya mkutano wake wa uzinduzi hadi saa 12.38 jioni tena mbele ya Mkuu wa nchi na viongozi wote wa serikali wakati wanajua fika kuwa sheria inawataka kufunga mkutano saa 12.00 jioni. Kwamba CCM na inavionesha vyama vingine kuwa iko juu ya sheria na kwamba wengine wakiiga watajiju. Na baada ya kupitisha muda huo CCM inamshinikiza Mkurugenzi wa manispaa ya ILALA aandike barua NEC kuijulisha kuwa ni yeye ndiye alielekeza mkutano uendelee hadi muda huo (very illogical reason).


6. Rais mstaafu wa awamu ya 3 Benjamin William Mkapa kusimama hadharani na kuwatukana wapinzani kuwa ni "MALOFA na WAPUMBAFU". Mpumbavu ni neno kali na lina maana ya "juha", "zuzu", "mtu asiyejielewa", "-----", "----", n.k. Wakati Mkapa akitukana hivyo hadharani na kuachwa juu ya Sheria, Lawrence Masha ambaye ni mwana UKAWA (hivi sasa) lakini zamani akiwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Tanzania, yeye amekamatwa na kuwekwa rumande na kunyimwa dhamana (inacheleweshwa kimakusudi) kwa "kosa" la kumtukana askari polisi (wengi kama sikosei) kwamba ni "washenzi", "wasio na shukrani na wasio na dini". Kwamba kwa tafsiri ya CCM na serikali yake pamoja na vyombo vinavyosimamia sheria (POLISI), neno "Upumbavu na Ulofa" siyo tusi lakini neno "Ushenzi na Kutokuwa na shukrani" ni tusi baya sana.


Hayo mambo sita niliyoyataja na mengine kadhaa ni dalili tosha kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaweza kuishia mahali pabaya. Hadi sasa sijaona CHOKOCHOKO kutoka upande wa UKAWA, hii ina maana kwamba hizi za CCM, VYOMBO VYA DOLA NA MAMLAKA ZA SERIKALI zikiendelea na zikawa zinahujumu kwa dhahiri maslahi ya UPINZANI na UKAWA, lolote lile linaweza kutokea.


Julius Sunday Mtatiro,
Dar Es Salaam.
 
Ni akili ya kawaida tu, kwamba jinsi ccm wanavyoendeleza fitna (rejea: Katazo la kuzindulia kampeni uwanja wa TAIFA, Katazo la Lowassa kupanda daladala na kutembelea wananchi, Hila ya kunyima ukawa wasitumie uwanja wa JANGWANI, nakadhalika) ndivyo ambavyo wananchi wa kawaida (Malofa na Wapumbavu) wanavyozidi kujiuliza kwanini, na kuichukika CCM.

Kazi kwenu, endelezeni fitna, watu ndio wanazidi kuwaona mlivyo wababaishaji.

VIVA UKAWA!!!!!!!!!
 
Nashukuru Ndg Yang Lakn,Nahsi Ulivoandika Unaonekana Unahx Kama Mnaonewa.Mi Naomba Nijibu Tu
1.Nikuulize Tu,hv Lowassa Kabla Ya Kuwa Mgombea Wa Urais(ukawa)alikua Anaenda Na Hao Watu Wote Msibani?
2.Hayo Maandamano Yalikatazwa Kwa Wote Kutokana Yalionekana Yana Athar,mbna Mlivorudisha Fomu Hakukua Na Tamko Lolote Lile?
3.Nadhani Ukiwa Mshabiki Zaid Jambo La Ziara Ya Lowassa Utahx Kama Ni Uonevu,lkn Kaul Ya Polis Imejieleza Vizur Tu.Na Samia Ziara Yake Inaeleweka Tayar Ana Ulinz Lkn Lowassa Hakua Na Ulinz Kutokana Na Kushtukiza
4.Kwa Hali Ya Kawaida Tu,hata Kumbi Zetu Wakwanza Ndo Anapewa Great Priorty Dan Anthr,same To Jangwan.Na Mliona Wap Uwanja Wa Taifa Ukafanyiwa Siasa?
5.Nazani Nec Ilitoa Tamko Lake Na Kukemea Juu Ya Ccm Kuongeza Mda,kwa Hyo Unaposema Walikua Wapo Juu Ya Sheria Sikubalian,na Tukubaliane Tu Sheria Walizosain Za Uchaguz Viongoz Wenu Kuna Sehemu Inayoibana Chama Kama Kimezidisha Mda Wa Kampeni?
6.Kutukana Hata Nyie Mnatukana,hata Huyo Mnaemnadi Sasa Mlishamtukana,ni Series Jihojini Nanyie
 
Mtatiro acha kuchochea vurugu Tanzania tambua kuwa amani ikivurugika utakuwa sehemu ya washitakiwa ICC The Hague.

kuna chochote kati ya hayo aliyoyasema ni uongo?kati ya mtatiro aliyeandika haya na hizo mamlaka zinazofanya haya nani anazua vurugu?
 
Neno Mapinduzi kutumika mpaka leo ni dhahiri linaweza kutumika Kishetani zaidi kipindi hiki!

Umekariri jibu? Hapo ulipoquote kuna mahali umeona neno "Mapinduzi"?
 
Haya yanayoendelea nchini naona kayakalia kimya kabisa. Au mpaka hali iwe ya sintofahamu?
 
Hapa kazi tu maigizo mwachie Lowassa
 
Habari za jioni ndugu watanzania wenzangu..!

Salam salamu ndugu mheshiniwa Rais.

Sitaki nimwambie mtu yeyote yule ila maoni na mtazamo wangu uende moja kwa moja kwa rais wa nchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mh. Rais kama kweli ni rais mwenye dhamana ya kuongoza nchi hii kwa mjibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania unalo jukumu la kuwaongoza wananchi wa taifa hili bila misingi ya ubaguzi au upendeleo wa aina yeyote.

Vitendo tunavyoshuhudia katika mwanzo wa kampeni za uchaguzi haviashirii amani wala aina yeyote ya umoja wa kitaifa ambao tumekuwa nao kwa muda miaka zaidi ya hamsini.

Kunyimwa uhuru wa kidemocrasia itakuwa ni moja ya makosa makubwa yatakayorigharimu taifa hili lenye tunu ya amani tuliyorithishwa na mzee wetu hayati baba wa tiafa mwl.j.nyerere.

Kitendo cha kuwanyima upinzani uhuru wa kufanya mikutano sehemu za umma kama viwanja vya taifa, jangwani, kuzuia mikusanyiko ya siasa, kukmata watu, kupiga watu mabomu hakiwezi kuiweka nchi yetu katika hali ya kuitunza tunu ya amani nchini. Na pia kinapelekea kuligawa taifa katika vipande vipande.

Ukiwa kiongozi wa nchi na mwenye dhamana ya kila mtanzania kuwa huru, salama na haki za kiraia ujue unayo dhamana ya kuhusika na kila madhara yatakayo mpata mtu yeyote na taifa kwa ujumla.

Tatizo la haya yote ni hofu ya mabadiriko hasa ya uongozi kwa serikali na chama tawala ila nikukumbushe mh. Rais chukua muda kujifunza kwa baba wa taifa mwaka 1992 juu ya vyama vingi ambapo maoni ya wengi yalionesha kutokukubali vyama vingi. Ila busara ya mzee nyerere nakuona nguvu ya mabadiriko ambayo katika zama zote hajawahi kushindwa alimua kukubali vyama vingi.

Mabadiriko yanayoonekana kuwatia hofu watawala kwa maana ya rais na taasisi ya za chini ya ofisi ya rais wanaamini yamachagizwa na vyama vya upinzani hili ni kosa la kwanza kwa kipngozi makini huitaji kutumia njia za kisayansi kujua kinachochagiza mabadiriko. Nitataja chache hapa chini:-

Wananchi kukata tamaa na maisha hasa kufuatia hali duni za maisha na kutokuwepo mipango thabiti ya kuwakwamua kwa adui huyu namba moja UMASIKINI.

Kingine tabia ya jamiii kubadirika na wakati kufuatia maendeleo ya sayansi na technology uwepo wa mawasiliano ambapo sasa mtu anaweza kujifunza mambo mbalimbali kote duniani kunapelekea mahitaji ya jamiii kimabadiriko kuongezeka na watu hawaoni serikali ikibadirika kuwapatia mahitaji yao mfano utasikia serikali ikijiringanisha na MKOLONI huku ikisahau watu wanajipima na nchi zinazoebdelea.

Mwisho niombe kwa viongozi wenye dhamana ya nchii hii kwa kuanza na RAIS, JESHI, MAHAKAMA na USALAMA WA TAIFA na taasisi nyingine ndogo ndogo za kisekta zenye dhamama katika uchaguzi huu mkuu kuwa sawa maana bila haki au matumizi yeyote ya nguvu kupoka haki ya kidemocrasia hayayaacha taifa hili likiwa salama. Viongozi wenye dhamana hasa wastaafu waache watumizi ya lugha za kuudhi na kebehi kama alivyofanya mzee MZEE MKAPA.

Mwisho nikukumbushe mh. Urejee na kuifanyia kazi kauli yako SOTE TUNAJENGA NYUMBA MOJA (TANZANIA) KWANINI TUGOMBANIE FITO. na busara ile ile ya uliyo waambia wanaccm dodoma kuwa CHAMA KWANZA MTU BADAE itumike pia hapa TAIFA KWANZA (TANZANIA) ALAFU CHAMA(CCM) BADAE. iwapo ccm ikishindwa Tanzania itabaki ile ile na UKAWA au vyama vingine vikishindwa Tanzania itakuwepo vilevile.
 
Sheria ya vyama intaka vyama vipewe muda -pawe na mgawanyo sawa kipindi cha kampeni kwa vyama na wagombea , NEC inawajibika kuona vyama vinatendewa haki, msajiliwa vyama na mabalozi wanapaswa kufahamishwa panapokuwa hakuna haki, UKAWA mkiwa legelege hakuna kitakachoendele lazima mshupae liwalo na liwe
 
Usiwashtue CCM wewe!!!

Acha waendelee na fitna zao tutakutana 25/10/2015.
 
ni muda mwafaka TBC na TBC Taifa kuonesha mikutano ya ukawa live
 
Hofu yangu ni mipango yao wanayopanga kupindua matokeo endapo CCM itaanguka na tayari kuna kila dalili ya CCM kuangukia pua mwaka huu. Nasikia kuna Rais mstaafu aliyewaita watanzania wapumbavu na malofa ndiye amejiapiza kupanda juu ya hata rais wa sasa ili kupindua matokeo. Sasa huko wanakotaka kutupeleka ndo hatari zaidi, Kenya iwe mfano tusirudi huko. Pia wakumbuke aliyekuwa rais wa Gambia yuko wapi sasa.
 
Nadhani nchi ikija kuingia matatizoni wa kwanza kulaumiwa ni amiri jeshi mkuu na vyombo vya usalama kutokutenda kazi zao inavotakiwa. Vyombo vya ulinzi vifanye kazi kwa masilahi ya umma na sio chama tawala. Watu wanataka mabadiliko wamechokwa kwa nini vyombo husika viwaamulie watu. Na kama walitaka mfumo wa chama kimoja kwa nini waliruhusu vyama vingi . Hakuna mwenye hati miliki na hii nchi mana Jk jangwani alisema atamkabidhi nchi magufuli it means hawataangalia maamuzi ya wananchi. Jk na washauri wako Watanzania wamebadilika na wamejikatia tamaa ya maisha na hawana cha kupoteza kabisa msitake kutuvurugia amani ya nchi yetu kwa kutotenda haki mana huinua taifa. Hata egpty ilianza utani hivi hivi ikaja Libya wakatumia kigezo hicho kwa gadafi na Tanzania tusipokua makini na hekima nchi zenye masilahi na kuvuruga nchi zitatumia huo mwanya
 
Halafu katika vijana wenye upeo finyu na mitazamo ya kizembe mtatilo yupo kundi A jamaa akili yake siku zote ni akili ya kutazamia tu.
 
Back
Top Bottom