Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Huyu ni Rais wa 6 Tangu Tanganyika ilipoungana na Zanzibar na kuunda nchi mpya Tanzania.
Marais 5 waliopita wote walizaliwa na huyu wa Sasa alivyozaliwa. Lakini hatujawahi kuona sherehe za kuzaliwa kiongozi zinageuzwa sherehe za kitaifa.
Naziita za kitaifa Kwa sababu zimepangwa kimikoa Kila mwaka. Mwaka huu ilikuwa zamu ya mkoa wa Rukwa na Jana zimefanyika uwanja wa Nelson Mandela mgeni rasmi akiwa Mkuu wa mkoa ambaye analipwa na serikali.
Lakini pia sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi wengi wanaolipwa na serikali na ni waajiriwa wa serikali àmbao badala ya kuhudumia wananchi walikwenda kushinda uwanja wa Mandela kushuhudia sherehe za birthday.
Walikuwepo viongozi wa Halmashauri, Vyombo vya ulinzi na usalama, serikali Kuu nk. Ni kama tumepoteza mwelekeo rasmi na Washauri wa Rais wameacha wapambe wampotoshe kiongozi wa nchi.