Kaparo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 2,072
- 5,053
Umeeleweka mkuu.-Sirecommend kukimbia mara kwa mara kama una lengo la kutaka kujaza mwili, ile siku moja ya kupumzika itumie kwa kukimbia.
-Push ups ni nzuri in fact baadhi ya watu wakimaliza kufanya pull ups hupiga push ups kwanza (kwa beginner ni nzuri zaidi itampa nguvu za mikono).
-Squats ni lazima ili kubalansi mwili, lakini hatuchanganyi mazoezi na kupelekea kutengeneza kachumbari squats ni zoezi la miguu ina siku yake.
-Kuruka kamba ni aina ya cardio, siyo mbaya kuruka kwa kua ni aina ya warm up kabla haujaanza workout yako.
-Kwa mtu anayeanza na anakula ipasavyo, anakunywa maji ipasavyo na kupumzika ipasavyo matokeo ni ndani ya wiki sita. Ila pia kuna factors kama genetics na ubora wa chakula kati ya mtu na mtu.
Noted!