Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ilikuwa form V, baada ya orientation, tunes za kujuana. Wengi tulishapewa majina ya rafiki wa rafiki ambae anakuja shule ile.

Dining siku ya kwanza mdada mmoja alimwaga magarage kisa alimkuta mende ndani ya bakuli. Kwakuwa bado tulikuwa na makula kula kuna waliomtengenezea orange squash na marie biscuits.

Baada ya miezi miwili pale shule, mdada alikuwa hodari wa kutoa mende kwa kijiko na kuendelea na menu.
 
Kuna shule inaitwa Mwakavuta (wenyeji wanaiita Mwakauta) nikavuta siku za kuripoti kwa kua nilitaka nitoke nyumbani baada ya valentine day.

Nafika siku hiyo ni jumapili siku ya wali. Nikala kidogo nikaugawa, naenda kuosha sahani ghafla ukungu umetanda kiasi hauwezi kuona hatua mbili mbele.
Nikasimama pale pale kwa zaidi ya dakika 45 ili ukungu upite nisije nikapotea nikaingia msituni. Sehemu yenye baridi kali kama haujavaa viatu au ni vyepesi vidole vya miguuni unaanza kuhisi vinachomwa chomwa na sindano. Nahisi ni dalili za kua frostbitten.

Ukungu unamalizikia vidole vikawa vinaonyesha kama damu imevilia. Tumelala bwenini nakutana na watu kutoka Chunya, Kilimanjaro, Moshi, Kigoma, Mafinga n.k. na wote wanasema baridi la pale si mchezo.

Asubuhi naamka. Njia za shule zote zina theluji, boksa niliyoiacha jana kwenye kamba imeganda kwa barafu.

Nikaanza kupima pros na cons.
-Kwanza walimu walituambia watoto wa O Level wote wana ngoma, kumbe na wale watoto waliambiwa sisi wote tuna ngoma. Ingawa wakinga siyo wabanaji lakini hilo doa litachukua muda wangu.

-Shule haina mabinti wazuri, hao waliopo wavuna mbao na wanakijiji wote mnawagombea.

-Unaweza kua na hela lakini hakuna cha kununua.

-Umbali mpaka wilayani ni 22KM na gari ni moja likipita limepita ama utembee, nilitembea aisee nilikoma, kila sehem ya mwili iliuma. Nilienda kupiga PPS hadi PPS zinatoka ndo nagundua kuna makamasi yalikua yananitoka. Sijui mpiga picha alidhani urembo.

-Rate ya kupiga puchu ikawa juu.

-Walimu wawili wa masomo yangu walikua wanakukaririsha kitu cha kitabuni hawakichambui wala nini halafu ni unasomewa sasa akiwa anasoma unagundua na yeye kuna vitu anavijua hapo. Mmoja alienda Mbeya akakaa zaidi ya mwezi huku somo limesimama.

-Chakula kibaya sijapata kujua. Kuna wadudu hua wanaranda randa kwenye balbu ukiwaua wanatoa harufu mbaya, sasa wale unawakuta kwenye maharage wapo kibao. Wali ikawa ndiyo luxury food, ugali unaula kidogo, asubuhi unanywea uji, makande, unakula kidogo asubuhi unanywea uji.
Wali ulisababisha watu wapigane, kulikua kuna paper two sasa form six wanajihisi wao ndiyo wanatakiwa kuanza, jamaa wa form five akafosi kingi ebwana washkaji wawili akaanza kumpiga.
Ila baadaye na yeye aliwatafuta mmoja mmoja na wakamheshimu.

Nilifeli kwa mengi.
 
Ok hiki ninachoandika ni off topic.

Kuna jamaa aliripoti shule, bishoo si mchezo. Kuna jamaa akawa anamuonea onea tu akimkuta anakula anachukua chakula, anachukua madaftari yake. Halafu anamwambia kama unaweza si upigane? Ishu ilienda kama mwezi.

Maji yakikata kuna kama kijito cha maji ndiyo hua tunayafuata, basi yule bishoo akavaa traki raba na fulana akamkuta mshkaji yupo na sisi akamwambia twende mtoni. Jamaa akajibu kwa dharau "Unataka nikakuf.ire?" mshkaji akajibu hapana nataka tukapigane, Ila tuwe wawili tu atakayerudi shule hapa ndiyo mshindi, jamaa akakubali wakaenda.

Dakika 10 nyingi tunamuona bishoo anarudi. Akatuambia kamchukueni jamaa, tumefika kule yule jamaa kila unapomgusa analia akafuatwa na gari la shule gari lenyewe wipers hazifanyi kazi na ukungu umeshakuja ikabidi mmoja akae kwenye boneti awe anafuta futa na mwendo uwe wa kobe.

Baada ya kupona akatuambia "Yaani sijaambulia hata ngumi moja, huyo jamaa hafai" kumbe yule bishoo ni mshindi wa Judo ngazi ya mkoa huko mkoani kwao. Halafu ikatokea wakawa marafiki vibaya mno.
 
Siku ya kwanza nilianza kula menu ya jioni ilikuwa ugali

Ugali ulikuwa wa unga uliokaa kwa muda mrefu hadi ukavundika ukawa na harufu fulani amaizing.

Nilikula matonge hayazidi matano nikaacha nikaenda kuumwaga, kesho yake njaa ililikamata maana sikula vizuri jana yake.

Ilipofika lunch ile harufi sikuiona tena(sikuijali) niliparamia menu bila kubakisha hata punje ya tonge. Kuanzia hapo nikazoea ugali moja kwa moja
 
Siku ya kwanza nafika kidato cha 5 nikapokewa na watoto wa olevel wakanifikisha kwe bweni nililopangiwa sababu hiyo shule ilikua unapangwa kabla hata hujareport, nimefika tu nikatoa malapa nikaoge nabadili nguo kugeuka hamna malapa wala ndoo vyote vimeibiwa[emoji3] [emoji3] nilichukia shule mpaka nikaomba uhamisho
 
Ha ha ha ha uzur nilikuwa mwenyeji wa hilo eneo naingia form V fresh tu madogo wakaja kunipokea na kunipeleka dom letu baada ya hapo maisha fresh tu jumatatu jumatano jumamos usiku siku za wali alhamis mchana siku ya nyama hapo ndio kimbembe.
 
Mkuu hii shule au Guantanamo ndogo
 
Good story. Nimecheka sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Alimuweza aisee khaa
 
Form one nareport siku ya kwanza ugali maharage ulinishnda nkala ugali na ndizi za kuivaa...! Kesho yake nkanunua maandazi kibao sema nkaja kuzoeaa maana kuna mama alikuwa analeta na dagaaa....
 
Nilifika usiku nikapokelewa vzr n mpk namaliza hakukuwa na shida kubwa.
Sema mambo nayokumbuka, tulikuwa na HG mbabe balaa basi ikifika mida ya kula hasa wali lazima awe wa kwanza.
Ila mambo za kujificha dom na kukacha kwenda prepal ilikuwa kawaida sana, ukifua inabidi kuzichunga nguo tofauti na hapo hukuti kitu.
 
Hahaahahahhaaa...
 
Kisa kizuri kimenichekesha sana!!!
 
Mara yangu ya kwanza naenda boarding nakumbuka nilipekekwa na Baba mdogo..nilikua na shauku mno...nikaenda reception nikaandikishwa kila kitu nikapimwa na uniform..ile shule ukiicheki kwa nje unaona bonge la shule ..basi bana nikakabidhiwa pale dingi mdogo akageuza...naelekea maeneo ya shule nikawa naona pa ovyo ovyo

Nikapelekwa bwenini si unajua kuku mgeni lazima ajulikane..kila mtu anakushangaa ..nashukuru Mungu kuna wadada kama watatu wakaja kunipokea wakanipeleka chumbani kwao..ile shule ilikua ya ovyo sana ila kutokana na marafiki niliokua nao room nikaanza kuipenda

Ingawa siku ya kufunga nikasema sirudi tena katika hii shule na sikurudi
 
Nakumbuka shule langu na Old Moshi.. Noumer sana, hapo nimehamia form two nikitokea Moshi Ufundi..

Kule Moshi Tech nilisoma na viziwi,

Huku Old Moshi nikakutana na vipofu.. Ilikuwa raha sana.. But nashukuru nilijua lugha ya viziwi na vidoti vya vipofu..!

Day one naingia Old Moshi, nakumbuka nilipangiwa mambweni ya Meru.. Kuna wahuni walikuwa wanakaa Mawenzi, wakisikia mgeni tu wanataka kuja kumfanyia.... walipofika kwangu tu.. kabla ya salamu.. nikaanza kuwapa vitasa vya uhakika.. wakawa hawelewi... wakakimbia wote.. from dat day, niliheshimika mpaka namaliza form four..
 
Ni kizu nini?
Ha ha ha ha uzur nilikuwa mwenyeji wa hilo eneo naingia form V fresh tu madogo wakaja kunipokea na kunipeleka dom letu baada ya hapo maisha fresh tu jumatatu jumatano jumamos usiku siku za wali alhamis mchana siku ya nyama hapo ndio kimbembe.
 
Ilichukua kama week kwenda kupanga foleni..rafiki zangu walikua wananichukulia chakula..maana nilikua nafikiria kwenda kujipangisha mstari kisa chakula nikawa nasema hapana

Ila baada ya kuzoea ndio nilikua kinara kuwahi dinning kwenye foleni ya msosi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…