Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Nilifika shule kama saa tano nikafanya usajili na kila kitu nikaonyeshwa bweni. Kufika bwenini nakuta wenzangu busy na mechanics wakati huo sijui hata kitabu kimoja cha Physics. Muda naenda kuoga nakuta maji yamejaa bafuni kote. Na mimi nimebeba vimalapa vy kisistaduu kumbe natakiwa viatu vyenye soli ndefu kuingilia bafuni. Nikasimama kwenye ngazi nawaza niende nisiende na muda huo watu wanakaribia kwenda kula. Nikaanza kulia maana hata iweje ningesoma hapo tu. Nikapita kwenye yale maji machafu nikaenda kuoga nikarudi na mengine nikajisuuza ila moyoni nawaza hawa walioanza hapa form one waliwezaje. Sasa kwenye chakula ndo kulikua na shughuli yenyewe. Watu wanapanga mstaari mara wanaanza kusukumana. Nikasogea pembeni nikajitolea kulala njaa ila sio kula kwa foleni.
Kuna mdada nilikua namjua kumbe anafanya kazi kwa walimu. Wakati anapeleka chakula akaniona nimesimama pembeni watu wanagombania akaniambia nisubiri nakuletea chakula. Msosi ukaja wali nyama roast na mboga majani. Wakati wenzangu wanapigania ugali supu ya nyama na maharage mabayaaa.
Kuanzia siku hiyo nikawa nakula msosi wa walimu. Nilikua sipendi chakula cha shule kabisa. Baada ya kuzoea shule aiseee. Siku ya nyama nawahisha kontena langu kwa wapishi. Wakati wengine wakila nyama za kushemshwa mimi na rafiki zangu tushajaziwa nyama za kukaanga na maharage yaloungwa vizuri.
Ile shule niliishi kama chuo vile maisha ya msosi hayakusumbua. Simu ikiisha chaji napeleka kwa mwalimu ananichajia. Kila baada ya week mbili narudi home. Ukiacha tatizo la mabafu kujaa maji na kupanic wenzangu wamenipita baada ya kuzoea yale maisha nikajuta kukataa kwenda boarding O Level.
 
Nakumbuka shule yetu ilikuwa na wanafunzi wengi walikuwa ni kutoka Kigoma,Tabora na Mwanza...washamba balaa...umeme ukikatika tunawapa ndoo wakachote umeme...yaani hata watu wazima walikuwa wanabeba ndoo kwenda kuchota umeme.....na tulikuwa tunawaambia wasiporudi na umeme wabaki huko huko....walipata taabu sana
 
nlikuwa nimeriport form one. Baaada ya kufanya registration baada yakumaliza naelekea bwenini kuna jamaaa mmoja akaja kunipokea. Akabeba godoro. Akakunja kona sijui akaingilia wapi. Akapotea na godoro.

Baada ya kuzoea nkaja kujua lile godoro alienda kuuza mtaaan bei ya kutupwa.

Governement schools zina tabu na raha yake saana
 
Nimesoma Makongo swala la mlo lilikuwa fresh sana kilichokuwa kinaboa adhabu tu ukizingua unakabidhiwa kwa wajeda unakula mbata na kazingumu
 
Siwezi sahau scandia pale kibaha nikamwambia mzee shule hii mbaya mzee hakunisikiliza sana Sana aliwasha gari akateleza ila nikahamia pangani... Msosi Siku ile ilikua ugali na supu.. Yani futa kama lote.. Ila nimiaka 8 iliyopita now nipo namalizia PhD yangu ufaransa
 
Nakumbuka shule yetu ilikuwa na wanafunzi wengi walikuwa ni kutoka Kigoma,Tabora na Mwanza...washamba balaa...umeme ukikatika tunawapa ndoo wakachote umeme...yaani hata watu wazima walikuwa wanabeba ndoo kwenda kuchota umeme.....na tulikuwa tunawaambia wasiporudi na umeme wabaki huko huko....walipata taabu sana
😁😁😁
 
nlikuwa nimeriport form one. Baaada ya kufanya registration baada yakumaliza naelekea bwenini kuna jamaaa mmoja akaja kunipokea. Akabeba godoro. Akakunja kona sijui akaingilia wapi. Akapotea na godoro.

Baada ya kuzoea nkaja kujua lile godoro alienda kuuza mtaaan bei ya kutupwa.

Governement schools zina tabu na raha yake saana
Hahahaa
 
Siku ya kwanza nilianza kula menu ya jioni ilikuwa ugali

Ugali ulikuwa wa unga uliokaa kwa muda mrefu hadi ukavundika ukawa na harufu fulani amaizing.

Nilikula matonge hayazidi matano nikaacha nikaenda kuumwaga, kesho yake njaa ililikamata maana sikula vizuri jana yake.

Ilipofika lunch ile harufi sikuiona tena(sikuijali) niliparamia menu bila kubakisha hata punje ya tonge. Kuanzia hapo nikazoea ugali moja kwa moja
Hiyo harufu hua naiita kigunia
 
nilifika mapema kabla ya form five wote.
nikaelekezwa na mwalimu wa malezi mahala pa mabweni nikaambiwa utakuta vitanda vingi tu.
cha ajabu mabweni yote yalikuwa yamejaa na bado kuna watu kama mia mbili hivi wanakuja.
nikatafuta kitanda kibovu, nikaenda nje nikakata miti nikqpanga kama chaga nikaweka godoro langu jipya maisha yakaenda.
cha ajabu baada ya miezi sita kila aliyekuja alipotelea kwenye mabweni hayohayo yaliyokuwa yamejaa.
Kwangu tu kwenye ile cube, iliyotakiwa kukaliwa na wanafunzi wanne tulikuwa zaidi ya nane.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Nicheke kwanza kidogo.

Nilifika shule wenzangu wakiwa wameanza masomo, siku moja akaniita dada mmoja anaitwa Nuru alikuwa kidato cha 3 akaniuliza mbona wewe sijawahi kukuona hapa shuleni umetoka wapi? Nikamwambia nimetokea sehemu fulani akauliza wote mmetahiriwa au mna magovi. Nilikuwa na rafiki yangu mmoja anaitwa Thobias.

Nikamwangalia yule jamaa yangu maana alikuwa ni lile kabila lenye kukwepa tohara, nikasema ndiyo wote tumetahiriwa. Akauliza tena wote mmetahiriwa? Nikanyamaza.

Akaitwa jamaa mmoja mbambe aje kufanya uhakiki mbele ya yule dada (Nuru) ambaye nae alikuwa na mwenzake wa kike. Yule njema akafika na kumkamata Thobias na kuanza uhakiki jamaa kakutwa ana mkono wa sweta. Duh zamu yangu kufika nikalala mbele kwa mbio za Bolt sitaki ukaguzi kwenye dushe langu mbele ya KE.

Baada ya hapo nikaitwa timu ya shule kidogo nikapata ahuweni yale mateso niliyakwepa kwa mwamvuli wa soka.
 
Naikumbuka siku ya kwanza kuripoti form one. Nilipokelewa na watemi wa kidato cha pili. Nilivyofika Bwenini nilipewa viatu vinavyonuka harufu ya soksi chafu, ili niviweke mdomoni kama simu, na niwajulishe wazazi kuwa nimefika salama shule. Niligoma, wakamwaga maji bweni zima ili form one wote tujifunze kudeki-Hiyo tuliifanya. Pia chakula kilikuwa kibaya na maharage yalikuwa na funza japo tulikuja kuyazoea.
 
Ulikuwa unasoma mixture mkuu??
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Nicheke kwanza kidogo.

Nilifika shule wenzangu wakiwa wameanza masomo, siku moja akaniita dada mmoja anaitwa Nuru alikuwa kidato cha 3 akaniuliza mbona wewe sijawahi kukuona hapa shuleni umetoka wapi? Nikamwambia nimetokea sehemu fulani akauliza wote mmetahiriwa au mna magovi. Nilikuwa na rafiki yangu mmoja anaitwa Thobias.

Nikamwangalia yule jamaa yangu maana alikuwa ni lile kabila lenye kukwepa tohara, nikasema ndiyo wote tumetahiriwa. Akauliza tena wote mmetahiriwa? Nikanyamaza.

Akaitwa jamaa mmoja mbambe aje kufanya uhakiki mbele ya yule dada (Nuru) ambaye nae alikuwa na mwenzake wa kike. Yule njema akafika na kumkamata Thobias na kuanza uhakiki jamaa kakutwa ana mkono wa sweta. Duh zamu yangu kufika nikalala mbele kwa mbio za Bolt sitaki ukaguzi kwenye dushe langu mbele ya KE.

Baada ya hapo nikaitwa timu ya shule kidogo nikapata ahuweni yale mateso niliyakwepa kwa mwamvuli wa soka.
 
Nakumbuka Lyamungo aisee,nimefika form one pale sema nilichelewa kidogo,nimemaliza kufanya registration, napelekwa bwenini wakatokea watu wakabeba tranka langu kama jeneza wakawa wanalia wakaongezeka wengine wanarusha na maua kabisa!

Daah karibu nigeuze aisee,sema nilikuja kulipiza na Mimi baada ya kuzoea kwa form one waliofuatia!
 
Nakumbuka Lyamungo aisee,nimefika form one pale sema nilichelewa kidogo,nimemaliza kufanya registration, napelekwa bwenini wakatokea watu wakabeba tranka langu kama jeneza wakawa wanalia wakaongezeka wengine wanarusha na maua kabisa!

Daah karibu nigeuze aisee,sema nilikua kulipiza na Mimi baada ya kuzoea!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Walienda nalo wapi?
 
Back
Top Bottom