sabosabo
JF-Expert Member
- Dec 16, 2012
- 2,050
- 5,066
Wanakupeleka hadi bwenini,kuna mzazi hadi alienda kulalamika kwa Mkuu wa shule baada ya kuona mwanae anafanyiwa hivyo[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Walienda nalo wapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanakupeleka hadi bwenini,kuna mzazi hadi alienda kulalamika kwa Mkuu wa shule baada ya kuona mwanae anafanyiwa hivyo[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Walienda nalo wapi?
Wanakupeleka hadi bwenini,kuna mzazi hadi alienda kulalamika kwa Mkuu wa shule baada ya kuona mwanae anafanyiwa hivyo
Mmmhhhh we jmaa kwa kamba me skuwezi aiseeeOk hiki ninachoandika ni off topic.
Kuna jamaa aliripoti shule, bishoo si mchezo. Kuna jamaa akawa anamuonea onea tu akimkuta anakula anachukua chakula, anachukua madaftari yake. Halafu anamwambia kama unaweza si upigane? Ishu ilienda kama mwezi.
Maji yakikata kuna kama kijito cha maji ndiyo hua tunayafuata, basi yule bishoo akavaa traki raba na fulana akamkuta mshkaji yupo na sisi akamwambia twende mtoni. Jamaa akajibu kwa dharau "Unataka nikakuf.ire?" mshkaji akajibu hapana nataka tukapigane, Ila tuwe wawili tu atakayerudi shule hapa ndiyo mshindi, jamaa akakubali wakaenda.
Dakika 10 nyingi tunamuona bishoo anarudi. Akatuambia kamchukueni jamaa, tumefika kule yule jamaa kila unapomgusa analia akafuatwa na gari la shule gari lenyewe wipers hazifanyi kazi na ukungu umeshakuja ikabidi mmoja akae kwenye boneti awe anafuta futa na mwendo uwe wa kobe.
Baada ya kupona akatuambia "Yaani sijaambulia hata ngumi moja, huyo jamaa hafai" kumbe yule bishoo ni mshindi wa Judo ngazi ya mkoa huko mkoani kwao. Halafu ikatokea wakawa marafiki vibaya mno.
Hapana mkuu, enzi za headmaster mazengo, we ulikua primary badoKwa mzee luandala
Mkuu huu uzi ni kwa ajil ya sisi tuliofaulu na kusoma shule za serikali, makongo ndo mdudu ganNimesoma Makongo swala la mlo lilikuwa fresh sana kilichokuwa kinaboa adhabu tu ukizingua unakabidhiwa kwa wajeda unakula mbata na kazingumu
Nilifaulu mwaka ambao wengi walifeli mkuuhahahahaha! utakuta u miungoni mwa walio faulu baada ya serikali kurudia kusahisha baada ya kufeli sanaaa
Acha dharau mkuu
kama umesoma adv. miaka ya 2011 kuja juu ww ni kilaza.Nilifaulu mwaka ambao wengi walifeli mkuu
Hahahaha thanks for sharing[emoji23]Ilikuwa form V, baada ya orientation, tunes za kujuana. Wengi tulishapewa majina ya rafiki wa rafiki ambae anakuja shule ile.
Dining siku ya kwanza mdada mmoja akimwaga magarage kisa alimkuta mende ndani ya bakuli. Kwakuwa bado tulikuwa na makula kula kuna waliomtengenezea orange squash na marie biscuits.
Baada ya miezi miwili pale shule, mdada alikuwa hodari wa kutoa mende kwa kijiko na kuendelea na menu.
Huo mwaka nilikua nishamaliza chuokama umesoma adv. miaka ya 2011 kuja juu ww ni kilaza.
MAKETESTAN BULL ON GWAH 😀😀😀😀😀Kuna shule inaitwa Mwakavuta (wenyeji wanaiita Mwakauta) nikavuta siku za kuripoti kwa kua nilitaka nitoke nyumbani baada ya valentine day.
Nafika siku hiyo ni jumapili siku ya wali. Nikala kidogo nikaugawa, naenda kuosha sahani ghafla ukungu umetanda kiasi hauwezi kuona hatua mbili mbele.
Nikasimama pale pale kwa zaidi ya dakika 45 ili ukungu upite nisije nikapotea nikaingia msituni. Sehemu yenye baridi kali kama haujavaa viatu au ni vyepesi vidole vya miguuni unaanza kuhisi vinachomwa chomwa na sindano. Nahisi ni dalili za kua frostbitten.
Ukungu unamalizikia vidole vikawa vinaonyesha kama damu imevilia. Tumelala bwenini nakutana na watu kutoka Chunya, Kilimanjaro, Moshi, Kigoma, Mafinga n.k. na wote wanasema baridi la pale si mchezo.
Asubuhi naamka. Njia za shule zote zina theluji, boksa niliyoiacha jana kwenye kamba imeganda kwa barafu.
Nikaanza kupima pros na cons.
-Kwanza walimu walituambia watoto wa O Level wote wana ngoma, kumbe na wale watoto waliambiwa sisi wote tuna ngoma. Ingawa wakinga siyo wabanaji lakini hilo doa litachukua muda wangu.
-Shule haina mabinti wazuri, hao waliopo wavuna mbao na wanakijiji wote mnawagombea.
-Unaweza kua na hela lakini hakuna cha kununua.
-Umbali mpaka wilayani ni 22KM na gari ni moja likipita limepita ama utembee, nilitembea aisee nilikoma, kila sehem ya mwili iliuma. Nilienda kupiga PPS hadi PPS zinatoka ndo nagundua kuna makamasi yalikua yananitoka. Sijui mpiga picha alidhani urembo.
-Rate ya kupiga puchu ikawa juu.
-Walimu wawili wa masomo yangu walikua wanakukaririsha kitu cha kitabuni hawakichambui wala nini halafu ni unasomewa sasa akiwa anasoma unagundua na yeye kuna vitu anavijua hapo. Mmoja alienda Mbeya akakaa zaidi ya mwezi huku somo limesimama.
-Chakula kibaya sijapata kujua. Kuna wadudu hua wanaranda randa kwenye balbu ukiwaua wanatoa harufu mbaya, sasa wale unawakuta kwenye maharage wapo kibao. Wali ikawa ndiyo luxury food, ugali unaula kidogo, asubuhi unanywea uji, makande, unakula kidogo asubuhi unanywea uji.
Wali ulisababisha watu wapigane, kulikua kuna paper two sasa form six wanajihisi wao ndiyo wanatakiwa kuanza, jamaa wa form five akafosi kingi ebwana washkaji wawili akaanza kumpiga.
Ila baadaye na yeye aliwatafuta mmoja mmoja na wakamheshimu.
Nilifeli kwa mengi.