Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Kuna shule inaitwa Mwakavuta (wenyeji wanaiita Mwakauta) nikavuta siku za kuripoti kwa kua nilitaka nitoke nyumbani baada ya valentine day.

Nafika siku hiyo ni jumapili siku ya wali. Nikala kidogo nikaugawa, naenda kuosha sahani ghafla ukungu umetanda kiasi hauwezi kuona hatua mbili mbele.
Nikasimama pale pale kwa zaidi ya dakika 45 ili ukungu upite nisije nikapotea nikaingia msituni. Sehemu yenye baridi kali kama haujavaa viatu au ni vyepesi vidole vya miguuni unaanza kuhisi vinachomwa chomwa na sindano. Nahisi ni dalili za kua frostbitten.

Ukungu unamalizikia vidole vikawa vinaonyesha kama damu imevilia. Tumelala bwenini nakutana na watu kutoka Chunya, Kilimanjaro, Moshi, Kigoma, Mafinga n.k. na wote wanasema baridi la pale si mchezo.

Asubuhi naamka. Njia za shule zote zina theluji, boksa niliyoiacha jana kwenye kamba imeganda kwa barafu.

Nikaanza kupima pros na cons.
-Kwanza walimu walituambia watoto wa O Level wote wana ngoma, kumbe na wale watoto waliambiwa sisi wote tuna ngoma. Ingawa wakinga siyo wabanaji lakini hilo doa litachukua muda wangu.

-Shule haina mabinti wazuri, hao waliopo wavuna mbao na wanakijiji wote mnawagombea.

-Unaweza kua na hela lakini hakuna cha kununua.

-Umbali mpaka wilayani ni 22KM na gari ni moja likipita limepita ama utembee, nilitembea aisee nilikoma, kila sehem ya mwili iliuma. Nilienda kupiga PPS hadi PPS zinatoka ndo nagundua kuna makamasi yalikua yananitoka. Sijui mpiga picha alidhani urembo.

-Rate ya kupiga puchu ikawa juu.

-Walimu wawili wa masomo yangu walikua wanakukaririsha kitu cha kitabuni hawakichambui wala nini halafu ni unasomewa sasa akiwa anasoma unagundua na yeye kuna vitu anavijua hapo. Mmoja alienda Mbeya akakaa zaidi ya mwezi huku somo limesimama.

-Chakula kibaya sijapata kujua. Kuna wadudu hua wanaranda randa kwenye balbu ukiwaua wanatoa harufu mbaya, sasa wale unawakuta kwenye maharage wapo kibao. Wali ikawa ndiyo luxury food, ugali unaula kidogo, asubuhi unanywea uji, makande, unakula kidogo asubuhi unanywea uji.
Wali ulisababisha watu wapigane, kulikua kuna paper two sasa form six wanajihisi wao ndiyo wanatakiwa kuanza, jamaa wa form five akafosi kingi ebwana washkaji wawili akaanza kumpiga.
Ila baadaye na yeye aliwatafuta mmoja mmoja na wakamheshimu.

Nilifeli kwa mengi.
Daah aisee
 
Mimi nimesoma bagamoyo secondary, shule pekee ukiwa ufukwen au baharin unaogelea unakua bado upo eneo la shule, kama advance hukusoma serikalin bas ww ni kilaza
Haha sio kweli bwana haya ni mawazo ya kitoto sana umenikumbusha sisi tulivyokuwa tunatambiana na wanafunzi wa shule ya jirani wao wanatuita mafukara eti ada yetu pocket money yao na sisi tunawaita vilaza
 
nlikuwa nimeriport form one. Baaada ya kufanya registration baada yakumaliza naelekea bwenini kuna jamaaa mmoja akaja kunipokea. Akabeba godoro. Akakunja kona sijui akaingilia wapi. Akapotea na godoro.

Baada ya kuzoea nkaja kujua lile godoro alienda kuuza mtaaan bei ya kutupwa.

Governement schools zina tabu na raha yake saana
Hahahaa nimecheka kama mazuri daah
 
nilifika mapema kabla ya form five wote.
nikaelekezwa na mwalimu wa malezi mahala pa mabweni nikaambiwa utakuta vitanda vingi tu.
cha ajabu mabweni yote yalikuwa yamejaa na bado kuna watu kama mia mbili hivi wanakuja.
nikatafuta kitanda kibovu, nikaenda nje nikakata miti nikqpanga kama chaga nikaweka godoro langu jipya maisha yakaenda.
cha ajabu baada ya miezi sita kila aliyekuja alipotelea kwenye mabweni hayohayo yaliyokuwa yamejaa.
Kwangu tu kwenye ile cube, iliyotakiwa kukaliwa na wanafunzi wanne tulikuwa zaidi ya nane.
Daah nyie mlivyofika chuo hamkupata tabu maana mlishazoea kuishi kama digidigi
 
Niliingia boarding form five:
Maisha ya boarding nilishayajua coz nikiwa o level weekend naenda kulala mashuleni kwa washkaji zangu!! So sikuwa na ugeni na misosi wala tabia.

Nilipokelewa na watemi wa form three, sura yangu tu wakajua huyu mwenyewe! Ilibidi wawe wananilia timing 🤣🤣🤣[emoji2]

Nilianza na intro! Usiku mnene nimelala kitandani ndoo na mazaga mengine nimeweka pembeni ya kitanda! Madogo wanatest zari kuniibia wanavizia wakijua nimelala, wanashtuka nawaambia oyaaah! Rudisha ndoo!

Kesho yake ikawa story shule nzima jamaa halali! Ukigusa ndoo yake au chochote anakutoa mbio! Ikawa ni mchezo na hakuna siku nilifeli, walichemka!

Wakanibananisha bwenini siku moja usiku sina hili wala lile! Nashtuka madogo kama kumi hivi wa form three na two wamenizunguka wanadai wananipa kipigo najitia msela sana hata kama nipo five!!

Niliruka ghafla toka kitandani nikatua kwenye mabega ya yule mbabe zaidi! Wakiwa wamehamaki mbabe wao kaanguka chini nikawahi switch ya taa nikazima kukawa giza totoro!! Nilitoa mkanda niliwadunda isivyo kawaida kuniona hawanioni wanashtukia vichapo mbaya zaidi mlango walifunga wenyewe kufungua hawawezi!! Walikula kichapo heavy sana!

Baada ya vilio kuzidi mle bwenini walinzi wakaja kuvunja mlango! Kuna niliokuwa nimewapasua na bakoli ya mkanda ikabidi wakatibiwe! Kesho yake waalimu hawanielewi na hawaamini kichapo nilichotoa, nikaambiwa rudi home kalete mzazi!!

Nilipoondoka sikurudi tena, na shule nikajihamisha mwenyewe kwenda shule yenye hostel badala ya boarding, dingi alikuja kujua baadae sana shule ninayosoma tena mkoa mwingine! akanyoosha mikono!!
Hwhhwh kwa ushujaaa huuu i hope umejiunga a lile jesh lililopewa kaz ya kupasua korosho
 
Jioni tunacheck mpira kengele ya msosi ikalia jamaa akaropoka tutakua ikifika half time basi mimi nikajua imeeleweka half time kufika kwenda DH msosi umeisha muda mrefu mwana mmoja ikabidi anibakizie asee siku fanikiwa kumfahamu yule jamaa sababu ilikua usiku,tangu siku ile huwa nina saidie MTU yeyote ambaye ninao uwezo pasipo kuangalia sura au mahusiano
 
Ile shule siisahau kwanza tokea utoto nilikua sipendi maharagwe... Nilivyofika kwenye ule mji nilikaa kwa rafiki wa familia yetu kama wiki nikawa naenda kuisoma shule.... Siku natinga shule nikakuta ni ugali maharagwe tena ya mawese yasiyoiva nikawa nashangaa mbona kila vessel ni la njano.... Tulikula mawese ile shule sisahau...

Ila kuna jamaa yangu alinifurahisha sana... Siku amefika shule jioni wakamshushia katikati ya mabweni... Watu wakaanza kupiga makelele asulubiweeeee jamaa akadaka tax akarudi alipotoka...
Hahaa daah nimecheka kwa nguvu..na hakuja tena?
 
Ok hiki ninachoandika ni off topic.

Kuna jamaa aliripoti shule, bishoo si mchezo. Kuna jamaa akawa anamuonea onea tu akimkuta anakula anachukua chakula, anachukua madaftari yake. Halafu anamwambia kama unaweza si upigane? Ishu ilienda kama mwezi.

Maji yakikata kuna kama kijito cha maji ndiyo hua tunayafuata, basi yule bishoo akavaa traki raba na fulana akamkuta mshkaji yupo na sisi akamwambia twende mtoni. Jamaa akajibu kwa dharau "Unataka nikakuf.ire?" mshkaji akajibu hapana nataka tukapigane, Ila tuwe wawili tu atakayerudi shule hapa ndiyo mshindi, jamaa akakubali wakaenda.

Dakika 10 nyingi tunamuona bishoo anarudi. Akatuambia kamchukueni jamaa, tumefika kule yule jamaa kila unapomgusa analia akafuatwa na gari la shule gari lenyewe wipers hazifanyi kazi na ukungu umeshakuja ikabidi mmoja akae kwenye boneti awe anafuta futa na mwendo uwe wa kobe.

Baada ya kupona akatuambia "Yaani sijaambulia hata ngumi moja, huyo jamaa hafai" kumbe yule bishoo ni mshindi wa Judo ngazi ya mkoa huko mkoani kwao. Halafu ikatokea wakawa marafiki vibaya mno.
hii nimeipenda
 
[emoji23][emoji23][emoji23]uzi mtamu sana..nakumbuka form 5 nafika shule flani hivi shida zilikua nyingi kama maji na msosi nkachukulia changamoto,
why nimeanza na kicheko,
Mapenzi ya ujanani nilmpenda toto la kichaga lipo form 6 akazungusha wee baadae akatik,
ishu ni kua alkua na urafiki na head girl ambae alikua mnoko hata walimu wana afadhali,head girl alkua mbabe ad anakunja ngumi,
Something funny,
day moja my girlfriend uyo wa kichaga akaumwa akaenda kwao,head girl mbabe akanipa adhabu 2kakate kuni nje kidogo ya shule,
head boy akaambiwa asimamie adhabu ya wengine waliokua wanapalilia mashamba,tulipokua wenywe head girl mbabe akawa mdogo hadi leo siamini, akamkandia gf wangu wa kchaga ni mhuni na malaya sana,to cut story short akanipekeka ad getto flani la hko maana yy alkua mwnyeji,
, tukabanjua ile amri ileee ya tunda na baadae 2karudi school fresh.
As days go on gf alrudi ila yeye,marafiki zangu ad walimu walkua na wasiwasi na mimi maana head girl mbabe alkua akiniona full mapozi,sauti atalegeza na hata niwe na kosa gani hanifanyi kitu,ule utomboy flani ukaanza kusepa .. fast forward'
We lived happily ever after[emoji23]
 
Back
Top Bottom