Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Aisee nimecheka sana yaani
 
Ha ha ha ha uzur nilikuwa mwenyeji wa hilo eneo naingia form V fresh tu madogo wakaja kunipokea na kunipeleka dom letu baada ya hapo maisha fresh tu jumatatu jumatano jumamos usiku siku za wali alhamis mchana siku ya nyama hapo ndio kimbembe.
Nafahamu Mkuu wewe ni m-boyz mwenzangu wa box 2


Cku ya kwanza nafika pale ilikua jioni mida ya saa 9 ivi nikafika kwenye bweni langu tukapokelewa na madogo wa o-level basi jioni tukaingia kupiga msosi (aisee msosi ulikua mbichi kabisa yaani nimekula tonge LA kwanza nikasema huu msosi mbichi miongoni mwa nilikua nao karibu nao alikuepo dogo aliyenipokea kule bwenini Dogo akanambia bro utaupenda tu subiri hela ziishe

Sasa bwana baada ya pesa niliyokua nayo kuisha baada kama ya week mbili nijikuta naumiss kabisa ugali + pola la saa nne ilikua ikifika tuu saa tatu ivi akili inaanza kuwanza pola tu akuna kingine
 
Naikumbuka sana siku hii.

Kantalamba secondary ilikuwa hatari sana.
 
Ile shule niliyoenda sikupata shida sana. Maana tayari walikuwepo ma schoolmate wangu wa o'level. Halafu pamoja na kwamba ilikuwa shule ya serikali lakini wanafunzi wake wanaishi kikondoo sana hadi wanaboa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nimeshindwa kujizuia kucheka
 
Najaribu kusoma comments nione hata mtu nimesoma nae shule moja sioni maana shule yetu ilikuwa mojawapo kati ya shule za ajabu kuwahi kama kutokea
Shule gan umesoma mkuu?
 
Unatukumbusha mengi, kula ugali mweusi na mchungu, maharage yaliowekwa maji na chumvi tu, and wait, yaliyotobolewa na wadudu na yamejaa funza, nyama iliochemshwa na maji na chumvi, imelepeta kinoma, wali uliochemshwa na maji na chumvi, umejaa chuya kishenzi, mara 1 kwa wiki, weekend! Uji usio na sukari wala chochote, saa nne asubuhi, ukinywa lazima usinzie class baadaye...
Ni shida..
Ila tuliweza, kwa kuboresha yote hayo kwa tanbond, sukari na chumvi...
ila vyoo vilikuwa mtihani, vimejaa na kufurika, hasa wakati wa mvua, haki ya nani wengine tulikuwa tukienda porini nyakati hizo bila kuogopa wadudu au wanyama wakali..
 
Usisahu kuweka maharage mango pickle na chilli source.
 
Hahhaha dah nmecheka saaana.

Mzee baba yani uliamua automatic tuu kuwa mwizi.
Haya mambo ya ukwata na tycs....uboizin ilikuwa ndio the only loophole ya kukutana na wadada kwenye joint mass
 
Dah! Uzi huu unanirudisha nyuma miaka 8 iliyopita pale Dodoma . Nakumbuka ilikua jioni ya saa moja siku ya ijumaa mwezi wa nne tarehe 15 mwaka 2011 katika viunga vya shule ya kambi ya wapigania uhuru (Kongwa freedom fighters) . Nikiwa na brother wangu. Nilipokelewa na mwalimu wa malezi na kunipeleka bwenini. Nawashukuru sana ma brother wa form six walionipokea kwani walinikarimu vyema sana. Nilikuta washamaliza kula, ilikua kande, nakumbuka walifanya donation ili na mimi nipate riziki. Nakumbuka kuna mmoja alinipisha kwenye kitanda chake ili mimi nilale na waliniahidi kuwa kesho yake wangenitafutia kitanda. Asubuhi waliniamsha na kuniambia leo ni siku ya gulio. Hivyo kama ningependa kwenda kuongeza vitu kidogo kwa ajili ya matumizi binafsi basi niungane nao kuelekea huko sokoni. In short walinifanyia mambo mengi ya kiungwana na walinichukua nikawa naishi kwenye bweni la form six ingali mimi ni form five.
Kuhusu changamoto za chakula nadhani ni common kwa shule zote za serikali japo pale kwetu halikua kubwa kihivyo kwani ilikua ni shule mpya wakati huo. Sisi tulikua ingizo la pili. Na hata idadi ya wanafunzi ilikua ndogo.
Siku ya kwanza kwenda class , nilijikuta mnyonge ghafla kwa maana nilikua mgeni kwa kila kitu,kuanzia matumizi ya calculator mpaka how to undertake learning activities, wakati nikiwa nasubiri mwalimu aandike ubaoni, ghafla nashangaa kipindi kimeisha na watu wakiwa wamejaza kurasa wakati mimi hata title sijaandika.
Anyway maisha yalienda kasi sana na hatimae wale broh zangu wakamaliza na nikatangazwa rasmi kuwa dormitory leader. Nilijitahidi kuhakikisha vijana wa kidato cha tano wanaoingia waishi maisha ya furaha kama yale ambayo mimi niliishi. Hivyo kwa nafasi yangu ,nilijitajidi kuhakikisha maisha ndani ya dormitories kuanzia usalama wa mali na usalama wa vijana wenzangu unakua ni mkubwa.
Ila pia sitasahau siku ambapo vijana wa form five tulipofanya mpango wa mapinduzi kutaka kumuondoa headboy aliyekua form six.bahati mbaya ule mpango ulivuja na nikahusishwa moja kwa moja kuwa nilivujisha. Lakini baadae ukweli ulikuja kufahamika. Mpango ulivujishwa na head girl wa o lever ambae alikua anatoka kimapenzi na headboy wa advance na kiongozi wa chakula wa advance ambae ni form five at the same time.
Maisha yalienda kasi hatimae na mimi pia nikamaliza na kuacha vijana wengine waendeleze yale mema tuliyoyaacha.
Shout out kwa kaka zangu wote popote mlipo, mohd hilary (dsm)vintani mlowe(dodoma), toroma ruvumwa(kigoma) frank swai (moshi), issa emanuel(dsm) pareso emanuel( arusha) na wengine wengi mlionilea kwa namna moja au nyingine.
Asanteni
 
Hata mimi team Ndanda mkuu, shule safi kupitiliza ile imeshachkua tuzo za usafi kitaifa kibao, bora ukamatwe haujaingia class kuliko ukamatwe umedodge usafi

Kero ya shule ile ni kunguni waliopitiliza
 
Ahahahah.
Sijui hata nieleze nn kuhus chama langu Tosa boys Iringa.
Changamoto zilikuwepo ila kwakua maisha nilikua nayajua haikunipa shida.
Especially nikiwa ndio namalizia 6 maisha yalikua matam balaa.Unajua ukiwa na akil maisha sio magum hata kidogo.
Kwanza mshkaji wangu alikua kiongoz wa bweni linaitwa Mwenge nikawa naish chemba ya kiongoz huko ni heshima.Wanafunz mnaripot huko kupangiwa rooms za kuishi.Walim kule kuingia ilokua nadra sana so unalala kama home tu.Usafi sifanyi.full kuchaji simu na kutumia heater kuchemsha chai.Tulichepusha umeme unaoingia kwenye switch ya taa.

Jikon kuna mdau mmoja nikamuweka vizur so siku za nyama wala sina shida.Naingia kama kwangu nashuka sado limejaa minofu wakat wengine wana scramble kuoanda kipnde kimoja kwenye folen.Huyoo nazama domu kula na wana.ukishikwa shikamana.

Tukaweka utaratib wa kila mwanachemba akirud toka likizo anaweka 15,000/= mezani tulikua kama 8 hiv so tunapata fungu la kutosha.Tukamweka sawa mke wa mwalim mmoja (almaarufu kama Feudal) akawa anapewa hilo fungu maalum kwa ajil ya kutuandalia mboga nzur nzur kila mlo wa jioni.Mchana tunapmbana kivingine.Ukizingatia iringa mboga mboga za majan haikua shida basi akawa anatupikia mchicha safi na maharage yameungwa fresh sometimes na visamaki tunafuata jion kwa ajil ya kulia ugali.
Ikafika kipind chemba ikawa inapata wagen wengi sana jion ila tukaona isiwe tabu tukapiga chin.
Maisha yalikua safi.Unapiga misuli mirefu sana kama chiz mana ile chemba tuliifanya maalum kwa PCM & PCB tu.Wengine mtusamehe .Ndani meza 2 kubwa na mabench so unasoma comortably.Walim wlika adm.so tunapiga MISULI YATIMA.
ilikua tabu mwanzo ila raha mwisho
 
Najiunga f1 shule moja mkoa wa kanda maalumu, ndani ya bwaro njaa imenipiga balaa ila kuweka tonge mdomoni nilishindwa kumeza aisee ugali mbaya kichizi nikajiuliza miaka mnne ntamaliza kweli? Lkn nilivyozoea nilikuwa napemesa nguna ni balaa.

Siku hiyo nimefika daftari bado mpya hazijaandikwa kitu, f3 mmoja kaniambia dogo twende prepo tukatoka Dom hadi class yeye daftari zake zina notes Mimi karatasi zote nyeupee, yeye akanza msuli, Mimi nikawa naperuzi na kudadisi tu yaan kuanzia saa mbili usiku hadi kumi na moja alfajiri, akiona nasinzia kwenzi za hatari na kujifanya kunipa mawaidha kwamba sekondari ni kusoma sio kulala tu kama primary huko, aisee nilipiga mistari ya pambizo siku hiyo mpka nikatosha tu

Nyingine ni f v mkoa mwingine nimepangiwa bweni nikachagua bed kumbe hilo bedi ni engo ya mbabe wa shule alikuwa hajaripoti bado, nikaambiwa na madogo bro hapo hama tafuta bed lingine kuna jamaa mbabe sana atakutoa tu, sikujali nikatandika bed nikaenda uwanjani, kumbe mbabe nae karipoti mida hiyo niliyotoka kwenda uwanjani ile kurudi dom nikakuta matandiko yangu yametupwa huko nkauliza nani kafanya hiv? huyo mbabe akajibu Mimi hapa hujaambiwa hiyo ni site yangu? kumcheki jaama kapanda msuli yuko vzr moyoni nikagwaya bweni zima wananicheki ntafanya nini nikawaza fasta fasta, kabla sijaaibika "sikiliza dogo naenda lokoo nikirudi nikute matandiko yangu yako fresh kitandani tena kitanda hicho hicho la sivyo labda sijatoka mkoa wa Mara na shule ya Mara Mimi" nikaongezea kuongea kikurya ingawa sio mkurya nikasepa lokoo njian nikawa nawaza hv asiporudisha ntafanyaje maana mkono simuwezi, baada ya lokoo narudi Dom pametandikwa freshiiiii sikutaka kujua nani ametandika nikaongeza mkwala kwa sauti "yaan Leo sijui ingekuwaje afu hizi shule ambazo unakatazwa kuripoti na sime nazo za kisenge tu mbona Mara tulikuwa tunaruhusiwa yaan Leo mbane mbane" kuanzia siku hiyo nikawa naitwa mkurya na kupewa hadhi ya mbabe wa shule, ha ha ha
 
Nakumbuka ilikua najiunga fom5 kahororo, ilikua ni mara yangu ya kwanza kwa maisha ya bweni, hata DOM nlikua sjui nn mana ake. Siku ya kwanza nilikula ugali mkavu afu mchungu kinyama, system ilivokua ni kwamba ugali unawekwa kwenye madishi afu wanagawa then madishi yanarud wanaweka maharage. Asa hicho kipindi cha kusubir maharage ka nusu saa hiv nkajua ugali unapigwa mkavu, bas kinyonge nkajivuta pemben nkapiga tonge mbili nkaenda kumwaga
 
Mbona kam nakufaham

Sio minaki kweli?
 
Ha ha ha ha ha,ulizingua
Mabaharia hapo tungeenda na mdundo tu full kuteleza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…