Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Aisee nimecheka sana yaani
Ok hiki ninachoandika ni off topic.

Kuna jamaa aliripoti shule, bishoo si mchezo. Kuna jamaa akawa anamuonea onea tu akimkuta anakula anachukua chakula, anachukua madaftari yake. Halafu anamwambia kama unaweza si upigane? Ishu ilienda kama mwezi.

Maji yakikata kuna kama kijito cha maji ndiyo hua tunayafuata, basi yule bishoo akavaa traki raba na fulana akamkuta mshkaji yupo na sisi akamwambia twende mtoni. Jamaa akajibu kwa dharau "Unataka nikakuf.ire?" mshkaji akajibu hapana nataka tukapigane, Ila tuwe wawili tu atakayerudi shule hapa ndiyo mshindi, jamaa akakubali wakaenda.

Dakika 10 nyingi tunamuona bishoo anarudi. Akatuambia kamchukueni jamaa, tumefika kule yule jamaa kila unapomgusa analia akafuatwa na gari la shule gari lenyewe wipers hazifanyi kazi na ukungu umeshakuja ikabidi mmoja akae kwenye boneti awe anafuta futa na mwendo uwe wa kobe.

Baada ya kupona akatuambia "Yaani sijaambulia hata ngumi moja, huyo jamaa hafai" kumbe yule bishoo ni mshindi wa Judo ngazi ya mkoa huko mkoani kwao. Halafu ikatokea wakawa marafiki vibaya mno.
 
Ha ha ha ha uzur nilikuwa mwenyeji wa hilo eneo naingia form V fresh tu madogo wakaja kunipokea na kunipeleka dom letu baada ya hapo maisha fresh tu jumatatu jumatano jumamos usiku siku za wali alhamis mchana siku ya nyama hapo ndio kimbembe.
Nafahamu Mkuu wewe ni m-boyz mwenzangu wa box 2


Cku ya kwanza nafika pale ilikua jioni mida ya saa 9 ivi nikafika kwenye bweni langu tukapokelewa na madogo wa o-level basi jioni tukaingia kupiga msosi (aisee msosi ulikua mbichi kabisa yaani nimekula tonge LA kwanza nikasema huu msosi mbichi miongoni mwa nilikua nao karibu nao alikuepo dogo aliyenipokea kule bwenini Dogo akanambia bro utaupenda tu subiri hela ziishe

Sasa bwana baada ya pesa niliyokua nayo kuisha baada kama ya week mbili nijikuta naumiss kabisa ugali + pola la saa nne ilikua ikifika tuu saa tatu ivi akili inaanza kuwanza pola tu akuna kingine
 
Naikumbuka sana siku hii.

Kantalamba secondary ilikuwa hatari sana.
mh! mimi nililipoti baada ya siku kama tatu hivi likaibuka timbwili la kudai wali baada ya vijana kuchoshwa na ugali wengu, timbwili likiongozwa na makamanda wa form2, hasira zikichochewa zaidi baada ya timu ya mpira wa miguu ya shule niliyolipoti kutandikwa bao moja kwa sifuri na timu ya shule jirani na mkuu wa shule asubuhi alitutabilia kufungwa siku hiyo.

Form5 wengi tukiwa ni wagen madogo hawana huruma kwa mtu anaekaa nyumanyuma waliamuru form5 tuwe mstali wa mbele kuelekea kwa mkuu wa shule wao wako nyuma wakiimba kwa hasira TUNATAKA WALI TUNATAKA WALI.

Nyumba ya mkuu wa shule ilibomolewa vibaya na tayali ilikua usiku, mkuu alipona hali mbaya akatoa taarifa polisi ffu wakaja aisee kichopo kikaanza. form 2, 3, na six walikua wenyeji wanajua kila kona shida ikawa kwa form 1 na sisi form 5 hatujui tukimbilie wapi, ktk kimbiakimbia usiku ule baazi ya vijana walijikuta kwenye bonde ambalo juu kuna majani na matete mengi ila chini ni kina kirefu cha maji na ile giza ilikua ngum kujua dimbwi limeanzia wapi na linaishia wapi, hapo vijana kazaa wa form1 walipoteza maisha (RIP)
Baada ya usiku huo wa kadhia timbwili lilirudiwa tena asubuhi baada ya wanafunzi kujua kuwa kuna wenzetu waliopoteza maisha huko dimbwini hapo sasa ffu waliomba poo viongoz wa mkoa walikuja shule baada ya hali kua mbaya shule ilifungwa kwa muda usio julikana.
 
Ilikuwa form V, baada ya orientation, tunes za kujuana. Wengi tulishapewa majina ya rafiki wa rafiki ambae anakuja shule ile.
Dining siku ya kwanza mdada mmoja alimwaga magarage kisa alimkuta mende ndani ya bakuli. Kwakuwa bado tulikuwa na makula kula kuna waliomtengenezea orange squash na marie biscuits.
Baada ya miezi miwili pale shule, mdada alikuwa hodari wa kutoa mende kwa kijiko na kuendelea na menu.
Ile shule niliyoenda sikupata shida sana. Maana tayari walikuwepo ma schoolmate wangu wa o'level. Halafu pamoja na kwamba ilikuwa shule ya serikali lakini wanafunzi wake wanaishi kikondoo sana hadi wanaboa.
 
Nakumbuka Lyamungo aisee,nimefika form one pale sema nilichelewa kidogo,nimemaliza kufanya registration, napelekwa bwenini wakatokea watu wakabeba tranka langu kama jeneza wakawa wanalia wakaongezeka wengine wanarusha na maua kabisa!

Daah karibu nigeuze aisee,sema nilikuja kulipiza na Mimi baada ya kuzoea kwa form one waliofuatia!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nimeshindwa kujizuia kucheka
 
Najaribu kusoma comments nione hata mtu nimesoma nae shule moja sioni maana shule yetu ilikuwa mojawapo kati ya shule za ajabu kuwahi kama kutokea
Shule gan umesoma mkuu?
 
Ilikuwa form V, baada ya orientation, tunes za kujuana. Wengi tulishapewa majina ya rafiki wa rafiki ambae anakuja shule ile.
Dining siku ya kwanza mdada mmoja alimwaga magarage kisa alimkuta mende ndani ya bakuli. Kwakuwa bado tulikuwa na makula kula kuna waliomtengenezea orange squash na marie biscuits.
Baada ya miezi miwili pale shule, mdada alikuwa hodari wa kutoa mende kwa kijiko na kuendelea na menu.
Unatukumbusha mengi, kula ugali mweusi na mchungu, maharage yaliowekwa maji na chumvi tu, and wait, yaliyotobolewa na wadudu na yamejaa funza, nyama iliochemshwa na maji na chumvi, imelepeta kinoma, wali uliochemshwa na maji na chumvi, umejaa chuya kishenzi, mara 1 kwa wiki, weekend! Uji usio na sukari wala chochote, saa nne asubuhi, ukinywa lazima usinzie class baadaye...
Ni shida..
Ila tuliweza, kwa kuboresha yote hayo kwa tanbond, sukari na chumvi...
ila vyoo vilikuwa mtihani, vimejaa na kufurika, hasa wakati wa mvua, haki ya nani wengine tulikuwa tukienda porini nyakati hizo bila kuogopa wadudu au wanyama wakali..
 
Unatukumbusha mengi, kula ugali mweusi na mchungu, maharage yaliowekwa maji na chumvi tu, and wait, yaliyotobolewa na wadudu na yamejaa funza, nyama iliochemshwa na maji na chumvi, imelepeta kinoma, wali uliochemshwa na maji na chumvi, umejaa chuya kishenzi, mara 1 kwa wiki, weekend! Uji usio na sukari wala chochote, saa nne asubuhi, ukinywa lazima usinzie class baadaye...
Ni shida..
Ila tuliweza, kwa kuboresha yote hayo kwa tanbond, sukari na chumvi...
ila vyoo vilikuwa mtihani, vimejaa na kufurika, hasa wakati wa mvua, haki ya nani wengine tulikuwa tukienda porini nyakati hizo bila kuogopa wadudu au wanyama wakali..
Usisahu kuweka maharage mango pickle na chilli source.
 
Nilifika shule usiku sana bweni lina harufu kali sijapata kuisikia vile kuna mwalimu alinipokea akaniambia asubuhi tu niende ofisini kufanya usajili.

Asubuhi mapema nikawahi ofisin kwenda kufanya usahili bwenini nikawaacha madogo kadhaa wa o level wanajiandaa kwenda madarasani.

Ofisini ile kulipa ada zao na kukamilisha usahili wakague vyeti na kukutana na wagen wengine wapya hapa na pale nikamaliza kila kitu saa nne.

Kurudi bwenini washavunja kufuli saa nyingi Dawa kubwa zile za mswaki, makatoni ya sabuni za kuogea na za unga, mafuta ya kupaka, kalamu na mazaga yote wale washamba wameiba wameniacha na counter book, nguo taulo na vitabu vichache

Roho iliniuma sana vile uzoefu wa maisha ya boarding nayajua nikahisi ni uzembe wangu jambo moja wahuni walikosa hela sikuweka kwenye sanduku la chuma.

Baada ya tukio sikureport popote nilienda kununua dawa ndogo ya mswaki, mswaki mmoja na sabuni ndogo ya kuoegea

vitu vingine vyote nikaanza kuiba kimya kimya niliiba bila huruma nilikua naiba ile mbaya mwaka mzima wezi wanatajwa hakuna anayenihisi vunja vunja makufuli wako darasani naiba vingine hata sina shida navyo natupa chooni iba iba mbaya sana.

Uchaguzi TYCS nachaguliwa kua katibu mkuu hakuna anayewaza mwizi ni mimi bwenini nakemea uwizi asubuhi jion na vunja.

Baadaye nikaamua kuacha mwenyewe. Nilisimulia marafiki kadhaa baada ya kumaliza shule miaka mingi ilivyopita. Mama alisema niwaombe msamaha. Sikuwahi kufanya hivyo.
Hahhaha dah nmecheka saaana.

Mzee baba yani uliamua automatic tuu kuwa mwizi.
Haya mambo ya ukwata na tycs....uboizin ilikuwa ndio the only loophole ya kukutana na wadada kwenye joint mass
 
Dah! Uzi huu unanirudisha nyuma miaka 8 iliyopita pale Dodoma . Nakumbuka ilikua jioni ya saa moja siku ya ijumaa mwezi wa nne tarehe 15 mwaka 2011 katika viunga vya shule ya kambi ya wapigania uhuru (Kongwa freedom fighters) . Nikiwa na brother wangu. Nilipokelewa na mwalimu wa malezi na kunipeleka bwenini. Nawashukuru sana ma brother wa form six walionipokea kwani walinikarimu vyema sana. Nilikuta washamaliza kula, ilikua kande, nakumbuka walifanya donation ili na mimi nipate riziki. Nakumbuka kuna mmoja alinipisha kwenye kitanda chake ili mimi nilale na waliniahidi kuwa kesho yake wangenitafutia kitanda. Asubuhi waliniamsha na kuniambia leo ni siku ya gulio. Hivyo kama ningependa kwenda kuongeza vitu kidogo kwa ajili ya matumizi binafsi basi niungane nao kuelekea huko sokoni. In short walinifanyia mambo mengi ya kiungwana na walinichukua nikawa naishi kwenye bweni la form six ingali mimi ni form five.
Kuhusu changamoto za chakula nadhani ni common kwa shule zote za serikali japo pale kwetu halikua kubwa kihivyo kwani ilikua ni shule mpya wakati huo. Sisi tulikua ingizo la pili. Na hata idadi ya wanafunzi ilikua ndogo.
Siku ya kwanza kwenda class , nilijikuta mnyonge ghafla kwa maana nilikua mgeni kwa kila kitu,kuanzia matumizi ya calculator mpaka how to undertake learning activities, wakati nikiwa nasubiri mwalimu aandike ubaoni, ghafla nashangaa kipindi kimeisha na watu wakiwa wamejaza kurasa wakati mimi hata title sijaandika.
Anyway maisha yalienda kasi sana na hatimae wale broh zangu wakamaliza na nikatangazwa rasmi kuwa dormitory leader. Nilijitahidi kuhakikisha vijana wa kidato cha tano wanaoingia waishi maisha ya furaha kama yale ambayo mimi niliishi. Hivyo kwa nafasi yangu ,nilijitajidi kuhakikisha maisha ndani ya dormitories kuanzia usalama wa mali na usalama wa vijana wenzangu unakua ni mkubwa.
Ila pia sitasahau siku ambapo vijana wa form five tulipofanya mpango wa mapinduzi kutaka kumuondoa headboy aliyekua form six.bahati mbaya ule mpango ulivuja na nikahusishwa moja kwa moja kuwa nilivujisha. Lakini baadae ukweli ulikuja kufahamika. Mpango ulivujishwa na head girl wa o lever ambae alikua anatoka kimapenzi na headboy wa advance na kiongozi wa chakula wa advance ambae ni form five at the same time.
Maisha yalienda kasi hatimae na mimi pia nikamaliza na kuacha vijana wengine waendeleze yale mema tuliyoyaacha.
Shout out kwa kaka zangu wote popote mlipo, mohd hilary (dsm)vintani mlowe(dodoma), toroma ruvumwa(kigoma) frank swai (moshi), issa emanuel(dsm) pareso emanuel( arusha) na wengine wengi mlionilea kwa namna moja au nyingine.
Asanteni
 
Wale wazee wa Ndanda boy shule safi siku nimeripoti tumelala vizuri saa kumi na moja naskia kiongozi mmoja anapayuka form five amkaaaaaa!!! Huku akiimba wimbo wa blood (the game ft Damian Marley) basi huu wimbo lazima niwe nao kila kwenye music devices zangu!!!
Hata mimi team Ndanda mkuu, shule safi kupitiliza ile imeshachkua tuzo za usafi kitaifa kibao, bora ukamatwe haujaingia class kuliko ukamatwe umedodge usafi

Kero ya shule ile ni kunguni waliopitiliza
 
Ahahahah.
Sijui hata nieleze nn kuhus chama langu Tosa boys Iringa.
Changamoto zilikuwepo ila kwakua maisha nilikua nayajua haikunipa shida.
Especially nikiwa ndio namalizia 6 maisha yalikua matam balaa.Unajua ukiwa na akil maisha sio magum hata kidogo.
Kwanza mshkaji wangu alikua kiongoz wa bweni linaitwa Mwenge nikawa naish chemba ya kiongoz huko ni heshima.Wanafunz mnaripot huko kupangiwa rooms za kuishi.Walim kule kuingia ilokua nadra sana so unalala kama home tu.Usafi sifanyi.full kuchaji simu na kutumia heater kuchemsha chai.Tulichepusha umeme unaoingia kwenye switch ya taa.

Jikon kuna mdau mmoja nikamuweka vizur so siku za nyama wala sina shida.Naingia kama kwangu nashuka sado limejaa minofu wakat wengine wana scramble kuoanda kipnde kimoja kwenye folen.Huyoo nazama domu kula na wana.ukishikwa shikamana.

Tukaweka utaratib wa kila mwanachemba akirud toka likizo anaweka 15,000/= mezani tulikua kama 8 hiv so tunapata fungu la kutosha.Tukamweka sawa mke wa mwalim mmoja (almaarufu kama Feudal) akawa anapewa hilo fungu maalum kwa ajil ya kutuandalia mboga nzur nzur kila mlo wa jioni.Mchana tunapmbana kivingine.Ukizingatia iringa mboga mboga za majan haikua shida basi akawa anatupikia mchicha safi na maharage yameungwa fresh sometimes na visamaki tunafuata jion kwa ajil ya kulia ugali.
Ikafika kipind chemba ikawa inapata wagen wengi sana jion ila tukaona isiwe tabu tukapiga chin.
Maisha yalikua safi.Unapiga misuli mirefu sana kama chiz mana ile chemba tuliifanya maalum kwa PCM & PCB tu.Wengine mtusamehe .Ndani meza 2 kubwa na mabench so unasoma comortably.Walim wlika adm.so tunapiga MISULI YATIMA.
ilikua tabu mwanzo ila raha mwisho
 
Najiunga f1 shule moja mkoa wa kanda maalumu, ndani ya bwaro njaa imenipiga balaa ila kuweka tonge mdomoni nilishindwa kumeza aisee ugali mbaya kichizi nikajiuliza miaka mnne ntamaliza kweli? Lkn nilivyozoea nilikuwa napemesa nguna ni balaa.

Siku hiyo nimefika daftari bado mpya hazijaandikwa kitu, f3 mmoja kaniambia dogo twende prepo tukatoka Dom hadi class yeye daftari zake zina notes Mimi karatasi zote nyeupee, yeye akanza msuli, Mimi nikawa naperuzi na kudadisi tu yaan kuanzia saa mbili usiku hadi kumi na moja alfajiri, akiona nasinzia kwenzi za hatari na kujifanya kunipa mawaidha kwamba sekondari ni kusoma sio kulala tu kama primary huko, aisee nilipiga mistari ya pambizo siku hiyo mpka nikatosha tu

Nyingine ni f v mkoa mwingine nimepangiwa bweni nikachagua bed kumbe hilo bedi ni engo ya mbabe wa shule alikuwa hajaripoti bado, nikaambiwa na madogo bro hapo hama tafuta bed lingine kuna jamaa mbabe sana atakutoa tu, sikujali nikatandika bed nikaenda uwanjani, kumbe mbabe nae karipoti mida hiyo niliyotoka kwenda uwanjani ile kurudi dom nikakuta matandiko yangu yametupwa huko nkauliza nani kafanya hiv? huyo mbabe akajibu Mimi hapa hujaambiwa hiyo ni site yangu? kumcheki jaama kapanda msuli yuko vzr moyoni nikagwaya bweni zima wananicheki ntafanya nini nikawaza fasta fasta, kabla sijaaibika "sikiliza dogo naenda lokoo nikirudi nikute matandiko yangu yako fresh kitandani tena kitanda hicho hicho la sivyo labda sijatoka mkoa wa Mara na shule ya Mara Mimi" nikaongezea kuongea kikurya ingawa sio mkurya nikasepa lokoo njian nikawa nawaza hv asiporudisha ntafanyaje maana mkono simuwezi, baada ya lokoo narudi Dom pametandikwa freshiiiii sikutaka kujua nani ametandika nikaongeza mkwala kwa sauti "yaan Leo sijui ingekuwaje afu hizi shule ambazo unakatazwa kuripoti na sime nazo za kisenge tu mbona Mara tulikuwa tunaruhusiwa yaan Leo mbane mbane" kuanzia siku hiyo nikawa naitwa mkurya na kupewa hadhi ya mbabe wa shule, ha ha ha
 
Nakumbuka ilikua najiunga fom5 kahororo, ilikua ni mara yangu ya kwanza kwa maisha ya bweni, hata DOM nlikua sjui nn mana ake. Siku ya kwanza nilikula ugali mkavu afu mchungu kinyama, system ilivokua ni kwamba ugali unawekwa kwenye madishi afu wanagawa then madishi yanarud wanaweka maharage. Asa hicho kipindi cha kusubir maharage ka nusu saa hiv nkajua ugali unapigwa mkavu, bas kinyonge nkajivuta pemben nkapiga tonge mbili nkaenda kumwaga
 
Siku ya kwanza nafika shule nikamtongoza mama mmoja alikua mpishi Wa canteen ya shule..akanikubali basi nilikula bure canteen mwaka mzima lakini nikaja kutembea na mtoto wake aliekuwa anasoma hapo kidato cha pili hapo ndipo huduma za mama zilipokata ila mtoto akawa ananihudumia zaidi ya mama mtu
Mbona kam nakufaham

Sio minaki kweli?
 
Yaani hapo ni kidato cha 1? Nyie wengine naona mlikuwa tofauti na mimi. Mimi wakati niko kidato cha 5, ndevu zimeanza kutoka sasa, niliwahi kupendwa na msichana aliyekuwa anafanya kazi tayari. Alikuwa anafanya kazi TANESCO wilayani. Basi mchezo mchezo tu aka-fall in love. Akanikaribisha nyumbani kula chakula cha mchana nikaenda na mshikaji. Tukala, akatupa pesa, halafu tukaondoka. Weekend nyingine akanikaribisha pia, nikatokea na mshikaji tena. Tukala halafu tukaondoka. Baada ya muda kupita, akanikaribisha chakula cha jioni. Safari hii akasema niende mwenyewe tu. Hapo ndio nikafunguka macho. Sikwenda na mchezo ukaishia hapo. Mtu aliyetaka kunitoa kwenye mstari wa masomo wakati huo, sikumwelewa kabisa.
Ha ha ha ha ha,ulizingua
Mabaharia hapo tungeenda na mdundo tu full kuteleza
 
Back
Top Bottom