Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

NDABO nimepita hapo advance 2009-2011
 
Hahaa daah nimecheka kwa nguvu..na hakuja tena?
Alirudi kesho yake akafikia ofsini kwa walimu ndio wakamleta mabwenini... Shule za wavulana zina vituko sana..
Yani ilikua ukiingia chooni lazma uingie na chupi au uchi na ukitoka unakaa chini ya mti kama dakika tano la sivyo ukiingia na nguo harufu ya choo utaibeba nusu saa....
 
Mleta mada sijui umewaza nini.

Siku naingia shule kanda ya Pwani nimetoka zangu huko kanda ya ziwa, mambo yote naona hovyo tu, lafudhi yangu haiendani na mtu yeyote mjini, kila ninayezungumza nae ananiuliza umetokea sehem .... eeeh

Wanafunzi wa kidato cha sita walinipokea wakanisaidia kubeba tranka, tukafika ofisini nikakuta jopo kubwa la walimu wanafanya registration, wakaniuliza jina nikataja, wakatafuta fomu zangu wakaziona wakajiridhisha nikatoa barua ya joining instruction.

Nikapangiwa bweni, nikaelekezwa nikazama fresh.

Kimbebe ilikua ni chakula cha jioni ile, ugali una unga unga kibao, maharage machache mchuzi ndio mwingi, unaweza kumwaga mchuzi ukabaki na maharage yako ukayahesabu moja moja. Nikala fresh ila kiungulia kilinisumbua sana.

Maji ya kuoga ni shida, ya kunywa ndio kabisa.
Life likaanza walimu wapo ila hawafundishi kila mtu ana mishe zake tu, kitabu kigumu mimi sikuwahi kusoma tuition ya pre form five kule shule nakuta watu wamekata topics karibu wamemaliza syllabus ya form five, siku ya kwanza tu naona wenzangu wanaenda prepo kujisomea, wanabeba Scientific calculators, mimi hata calculator sina wala sijui kuitumia, sina materials zozote nina madaftari yangu mapya 3 quires mengi tu, hata sijui niandike nini, yaani advertise tu masela wanarudi bwenini saa tano saa sita mi nishalala, mwili wote una nata majasho kwakua maji ya kuoga hakuna.

Suala la msosi ni ishu, chai ya rangi inapikwa nyeusiii majani kibao, maji ya chumvi alafu sukari hawaweki na wakiweka ni kwa mbali sana kitafunwa ujitegemee, ukinywa kama vile unakunywa orals.

Mwalimu wangu wa darasa alikua na roho mbaya kinyama, kosa dogo anaweza kukushupalia ukafukuzwa shule.

Hii shule ndio mtoto wa Rais Magufuli alichemka tumeripoti nae siku moja, asubuhi uzalendo ukamshinda akapiga simu akafatwa na Land Cruiser V8.
 
Mtoto wa Magu Jesca?
 
Soma title ya uzi mtoa mada amespecify shule za serikali
 


Watu wa mkoa si sawa na wanaume wa Dar.....kipimo ndiyo hiki mkuu.
 
Hata sijui yuko wapi maana baada ya kuondoka sikuwahi kumsikia tena wala kumuona kwenye tv hata mtandaoni sina uhakika kama anaingia.
Inaelekea familia ya Magu inaishi kama iko jeshini
Haha kuwa na baba kama yule ni shida jamani bora awe mlima korosho huko unaweza hata kumpiga chenga ya mwili. Hujawahi kufikiria kuwa huenda ali RIP? (God forbid)
 
Soma title ya uzi mtoa mada amespecify shule za serikali
Secondari nilisoma shule ya serikali wakati huo Private zilikuwa kiduchu. Naongelea late sixties and early seventies. Halafu sisi tulikuwa watoto wa wakulima maskini tusingeweza kumudu hizo shule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…