King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Respect.heshima yako mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Respect.heshima yako mkuu
Poapoa umepita kipindi ya miaka kitambo au dot comNimepita pale mkuu..
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Aisee ulitishaaNilifika shule usiku sana bweni lina harufu kali sijapata kuisikia vile kuna mwalimu alinipokea akaniambia asubuhi tu niende ofisini kufanya usajili.
Asubuhi mapema nikawahi ofisin kwenda kufanya usahili bwenini nikawaacha madogo kadhaa wa o level wanajiandaa kwenda madarasani.
Ofisini ile kulipa ada zao na kukamilisha usahili wakague vyeti na kukutana na wagen wengine wapya hapa na pale nikamaliza kila kitu saa nne.
Kurudi bwenini washavunja kufuli saa nyingi Dawa kubwa zile za mswaki, makatoni ya sabuni za kuogea na za unga, mafuta ya kupaka, kalamu na mazaga yote wale washamba wameiba wameniacha na counter book, nguo taulo na vitabu vichache
Roho iliniuma sana vile uzoefu wa maisha ya boarding nayajua nikahisi ni uzembe wangu jambo moja wahuni walikosa hela sikuweka kwenye sanduku la chuma.
Baada ya tukio sikureport popote nilienda kununua dawa ndogo ya mswaki, mswaki mmoja na sabuni ndogo ya kuoegea
vitu vingine vyote nikaanza kuiba kimya kimya niliiba bila huruma nilikua naiba ile mbaya mwaka mzima wezi wanatajwa hakuna anayenihisi vunja vunja makufuli wako darasani naiba vingine hata sina shida navyo natupa chooni iba iba mbaya sana.
Uchaguzi TYCS nachaguliwa kua katibu mkuu hakuna anayewaza mwizi ni mimi bwenini nakemea uwizi asubuhi jion na vunja.
Baadaye nikaamua kuacha mwenyewe. Nilisimulia marafiki kadhaa baada ya kumaliza shule miaka mingi ilivyopita. Mama alisema niwaombe msamaha. Sikuwahi kufanya hivyo.
Ulisoma Kibaha ukiwa umechelewa. Zamani Kibaha ilikuwa inaongoza kwa uzuri. Wali/nyama kilikuwa kitu cha kawaida. Magodoro tulikuwa tuyakuta shuleni. Wanafunzi tulikuwa hatuendi shuleni na magodoro.Siwezi sahau scandia pale kibaha nikamwambia mzee shule hii mbaya mzee hakunisikiliza sana Sana aliwasha gari akateleza ila nikahamia pangani... Msosi Siku ile ilikua ugali na supu.. Yani futa kama lote.. Ila nimiaka 8 iliyopita now nipo namalizia PhD yangu ufaransa
Ulisoma Kibaha ukiwa umechelewa. Zamani Kibaha ilikuwa inaongoza kwa uzuri. Wali/nyama kilikuwa kitu cha kawaida. Magodoro tulikuwa tuyakuta shuleni. Wanafunzi tulikuwa hatuendi shuleni na magodoro.
Mambo yamebadilika. Kibaha tukipewa maziwa na mayai. Anayesema yajayo yanafurahisha, muongo tu.Mpaka nafika magodoro tulikua tunapewa ila ujinga ni huo ugali
[emoji23][emoji23][emoji23]hahahahaha! utakuta u miungoni mwa walio faulu baada ya serikali kurudia kusahisha baada ya kufeli sanaaa
Acha dharau mkuu
Siliza wimbo wa Jide,natamani kuwa kama mtoto..............................siku ya kwanza nimefika shule kesho yake ikawa shamba(nilihamia kutoka day nikapelekwa bording) nimefika shamba nimepangiwa mistari nane ya mahindi ya kupalilia tangu nizaliwe sijawai kulima nililia hatari akaja dada mmoja wa mwanza akaniambia atanisaidia kulima alilima fasta kufumba na kufumbua amemaliza nikamnunulia mkate akanywa na chai enzi zile mikate ya skoz,mpaka namaliza pale sikuwai kulima wala kupalilia mimi naenda shamba kupiga story natafuta wale wa kijijini nampa mkate analima kipande changu chote.
dada angu aliyenilea alikua anafanya kazi supermarket tranka langu lilika na vilonzo hatari mambo matamumatamu na kila mwisho wa mwezi anakuja kunitembelea.
kuku ,bata wa walimu tushaiba sana tu usiku tunaenda jikoni tunachemsha tunakunywa supu na nyama tulikua watundu sana ,kuna siku sasa tuliiba mbuzi wa mwalimu dhaaa sitasahau tulimchinja wenyewe,chuna wenyewe,tulikula usiku kucha ile siku,daaah shule ilikua raha sana nilikua kibonge nilirudi nyumbani mwembamba ugali ,uji ,vilinishinda kabisa nikawa nashindia mkate na juice.
changamoto za maisha natamani nirudi vile,nilikua sina stress yyt ile ninachowaza nikadibue maji ya nani nikaoge ,maisha yalikua mazuri siwazi yyt yule sina anayenitegemea daaah,sahizi nikiwaza ada ya shule january natamani nigeuke malaika nipae mbali na majukumu .
hahaha, hiyo itakua kijijiHahahaha kuna boya alikunywa pola bangala 3 kudadeq alikojoa mchana yan kwa godolo
mwaka gani umemalizaWent to old moshi pia
Meru pia
Aisee hata mimi umenikumbusha Lyamungo,kitu cha maharage unachanganya na parachichi!ilikua inasaidia sana aisee!Nimekumbuka ugali na maparachichi umbwe secondary...nimejifunza maisha sana kusoma 1-6 govt schools...
kama wewe ni Me,hiyo shule itakuwa Songea Boys aka Box 2Siku ya kwanza nafika kidato cha 5 nikapokewa na watoto wa olevel wakanifikisha kwe bweni nililopangiwa sababu hiyo shule ilikua unapangwa kabla hata hujareport, nimefika tu nikatoa malapa nikaoge nabadili nguo kugeuka hamna malapa wala ndoo vyote vimeibiwa[emoji3] [emoji3] nilichukia shule mpaka nikaomba uhamisho
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Aisee ilikuwa balaa...hukumpa mimba mkuu???Form two kama sikosei Tulikuwa tuna mtindo wa kuiba sukari siku moja Dada Mkuu akanibamba wenzangu wakakimbia.
Dada Mkuu akaniambia nakupa adhabu chagua nikupeleke kwa Walimu ufukuzwe shule? au uniache nifanye mimi navyotaka?
Nikamuambia asiseme kwa mwalimu basi akanisogelea alafu akanishika shika dushe [emoji1787]
Akaniambia ole wangu nimuambie mtu. Toka siku hiyo kila akijisikia ananibana kwenye kona anafanya mambo yake na mie nikawa naunga mkono juhudi [emoji1787]
Akawa Demu wangu hadi alivyomaliza shule.
Ki ukweli madem wa shule walikuwa wananizimia sana sijui ilikuwa kwa sababu ya ushombe shombe [emoji1787]
Baada ya yeye kusepa niliwafyagia sana.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Aisee ilikuwa balaa...hukumpa mimba mkuu???
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Aisee itakuwa alikuwa anawaadithia baadhi ya marafiki zakee na kama ulikuwa unamsukumia motoo wenyewee ndo balaa...Sikumpa mkuu nadhani hatakuwa alikuwa anajua masiku yake maana alikuwa juu yangu Kidarasa.
Maana yeye mwenyewe ndo alikuwa ananishurutisha kwa kifupi nilikuwa kama mateka ingawa nilikuwa naenjoy baadae.
Ingawa ulifeli ila wacha nikupe likeKuna shule inaitwa Mwakavuta (wenyeji wanaiita Mwakauta) nikavuta siku za kuripoti kwa kua nilitaka nitoke nyumbani baada ya valentine day.
Nafika siku hiyo ni jumapili siku ya wali. Nikala kidogo nikaugawa, naenda kuosha sahani ghafla ukungu umetanda kiasi hauwezi kuona hatua mbili mbele.
Nikasimama pale pale kwa zaidi ya dakika 45 ili ukungu upite nisije nikapotea nikaingia msituni. Sehemu yenye baridi kali kama haujavaa viatu au ni vyepesi vidole vya miguuni unaanza kuhisi vinachomwa chomwa na sindano. Nahisi ni dalili za kua frostbitten.
Ukungu unamalizikia vidole vikawa vinaonyesha kama damu imevilia. Tumelala bwenini nakutana na watu kutoka Chunya, Kilimanjaro, Moshi, Kigoma, Mafinga n.k. na wote wanasema baridi la pale si mchezo.
Asubuhi naamka. Njia za shule zote zina theluji, boksa niliyoiacha jana kwenye kamba imeganda kwa barafu.
Nikaanza kupima pros na cons.
-Kwanza walimu walituambia watoto wa O Level wote wana ngoma, kumbe na wale watoto waliambiwa sisi wote tuna ngoma. Ingawa wakinga siyo wabanaji lakini hilo doa litachukua muda wangu.
-Shule haina mabinti wazuri, hao waliopo wavuna mbao na wanakijiji wote mnawagombea.
-Unaweza kua na hela lakini hakuna cha kununua.
-Umbali mpaka wilayani ni 22KM na gari ni moja likipita limepita ama utembee, nilitembea aisee nilikoma, kila sehem ya mwili iliuma. Nilienda kupiga PPS hadi PPS zinatoka ndo nagundua kuna makamasi yalikua yananitoka. Sijui mpiga picha alidhani urembo.
-Rate ya kupiga puchu ikawa juu.
-Walimu wawili wa masomo yangu walikua wanakukaririsha kitu cha kitabuni hawakichambui wala nini halafu ni unasomewa sasa akiwa anasoma unagundua na yeye kuna vitu anavijua hapo. Mmoja alienda Mbeya akakaa zaidi ya mwezi huku somo limesimama.
-Chakula kibaya sijapata kujua. Kuna wadudu hua wanaranda randa kwenye balbu ukiwaua wanatoa harufu mbaya, sasa wale unawakuta kwenye maharage wapo kibao. Wali ikawa ndiyo luxury food, ugali unaula kidogo, asubuhi unanywea uji, makande, unakula kidogo asubuhi unanywea uji.
Wali ulisababisha watu wapigane, kulikua kuna paper two sasa form six wanajihisi wao ndiyo wanatakiwa kuanza, jamaa wa form five akafosi kingi ebwana washkaji wawili akaanza kumpiga.
Ila baadaye na yeye aliwatafuta mmoja mmoja na wakamheshimu.
Nilifeli kwa mengi.