Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Ile nimefika tu form V pale mjini Tanga, nilifika kwa kuchelewa kama wiki 3. Nakuta watu wanasolve necta ya form VI tena maswali ya complex number wakati hata topic nilikuwa siijui inahusu nini. Nilipagawa.
Haaa aa ahaa
 
Hahaha nilinunua chips za 1000 zikajazwa kwenye ungo wa kupepetea mchele. Gulio kila Jumamosi Chai ya rangi 200 chai ya maziwa 100
Napajua vizuri sana, mimi na baridi ni tofauti kabisa.
 
Hahaha nilinunua chips za 1000 zikajazwa kwenye ungo wa kupepetea mchele. Gulio kila Jumamosi Chai ya rangi 200 chai ya maziwa 100
Ha ha ha ha haaaaaaa, unaambiwa ukifika kule halafu ukaagiza chips za buku wanaokuzunguka wanabaki kutazamana halafu wanasemeshana kilugha huku wanakutazama.
 
Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni kwangu mimi ilikua ni kidato cha kwanza.

Kitu ninachokikumbuka sana katika ile siku ni lafudhi hasa za watu wa kanda ya ziwa.Nilikua naenjoy sana(na kushangaa pia) namna wasukuma walivyokua wanaongea kiswahili.
 
mh! mimi nililipoti baada ya siku kama tatu hivi likaibuka timbwili la kudai wali baada ya vijana kuchoshwa na ugali wengu, timbwili likiongozwa na makamanda wa form2, hasira zikichochewa zaidi baada ya timu ya mpira wa miguu ya shule niliyolipoti kutandikwa bao moja kwa sifuri na timu ya shule jirani na mkuu wa shule asubuhi alitutabilia kufungwa siku hiyo.

Form5 wengi tukiwa ni wagen madogo hawana huruma kwa mtu anaekaa nyumanyuma waliamuru form5 tuwe mstali wa mbele kuelekea kwa mkuu wa shule wao wako nyuma wakiimba kwa hasira TUNATAKA WALI TUNATAKA WALI.

Nyumba ya mkuu wa shule ilibomolewa vibaya na tayali ilikua usiku, mkuu alipona hali mbaya akatoa taarifa polisi ffu wakaja aisee kichopo kikaanza. form 2, 3, na six walikua wenyeji wanajua kila kona shida ikawa kwa form 1 na sisi form 5 hatujui tukimbilie wapi, ktk kimbiakimbia usiku ule baazi ya vijana walijikuta kwenye bonde ambalo juu kuna majani na matete mengi ila chini ni kina kirefu cha maji na ile giza ilikua ngum kujua dimbwi limeanzia wapi na linaishia wapi, hapo vijana kazaa wa form1 walipoteza maisha (RIP)
Baada ya usiku huo wa kadhia timbwili lilirudiwa tena asubuhi baada ya wanafunzi kujua kuwa kuna wenzetu waliopoteza maisha huko dimbwini hapo sasa ffu waliomba poo viongoz wa mkoa walikuja shule baada ya hali kua mbaya shule ilifungwa kwa muda usio julikana.
Bila shaka ni Kantalamba boys
 
Mimi nimesoma bagamoyo secondary, shule pekee ukiwa ufukwen au baharin unaogelea unakua bado upo eneo la shule, kama advance hukusoma serikalin bas ww ni kilaza
Yaani wewe mwenye akili ndio unasema hivi?
 
Ha ha ha ha haaaaaaa, unaambiwa ukifika kule halafu ukaagiza chips za buku wanaokuzunguka wanabaki kutazamana halafu wanasemeshana kilugha huku wanakutazama.
Wanaongea haraka haraka mno dah mpaka ilikua inabidi nipredict tu kua huyu atakua kamaanisha hiki na hiki
 
Siwezi sahau scandia pale kibaha nikamwambia mzee shule hii mbaya mzee hakunisikiliza sana Sana aliwasha gari akateleza ila nikahamia pangani... Msosi Siku ile ilikua ugali na supu.. Yani futa kama lote.. Ila nimiaka 8 iliyopita now nipo namalizia PhD yangu ufaransa
hahahahahaha, scandia umenikumbusha mbali sana mkuu.

Bonne journée!!
 
Nilipoingia form five pale ilboru maisha yalikua POA Sana sikuhisi utafauti Sana kwa sababu nilikua mpenzi Sana maharagwe niliona poa tu, sema hata ivo msosi was shuleni ulikua POA tu maana mchana Kama kawa ugali haragwe usiku Kila siku ubwabwa na haragwe , week end kitu Cha pilau , wazee wa kitei wanakumbuka Sana christopher cirilo , pongezi ziende kwa mzee kwayu best headmaster to me kwa kwel.
Mzee wa kitei, Ilboru chakula kilikua kizuri hasa usiku.Kwayu alikua mtu mzuri sana.
 
Aisee hii ratiba ya wali kila siku ilikuwa ilikuwa mwaka gani.? Maana enzi za kitemango wali ilikuwa unatafutwa kwa tochi, na mkifanya mchezo huo wali wenyewe mnakopwa.
Baada ya kitemango kuondoka.
 
Ulisoma Kibaha ukiwa umechelewa. Zamani Kibaha ilikuwa inaongoza kwa uzuri. Wali/nyama kilikuwa kitu cha kawaida. Magodoro tulikuwa tuyakuta shuleni. Wanafunzi tulikuwa hatuendi shuleni na magodoro.
 
Ile nimefika tu form V pale mjini Tanga, nilifika kwa kuchelewa kama wiki 3. Nakuta watu wanasolve necta ya form VI tena maswali ya complex number wakati hata topic nilikuwa siijui inahusu nini. Nilipagawa.
Hahahaha
 
Old moshi a.k.a Moshi Sec,karibu na Chuo cha Ushirika upande mwingine C.C.P,Chuo cha polisi, nilikutana na matope hatari.Udongo mwekundu unanata sana kipindi cha mvua.Matope bwenini unakwangua na jembe ndio uanze kudeki.Kuvaa gamboot kila mahali ,mpaka kwenda kuoga bafuni unavaa gamboot na taulo kiunoni ,kandambili mkononi.Ukifika bafuni unavua gamboot unavaa kandambili.ukimaliza unarudi tena kwenye gamboot.Chakula cha kugombania O levels wanafujo sana .Ugali na maharage au uji wanajaza kwenye ndoo ndogo,wengine wanakosa.Usiku hakuna walinzi kwa hiyo tunazurura tu mjini Moshi tupendavyo.Shule haikuwa na fence.Ni uamuzi wako uende prepal kusoma au kuzurura.Nilimaliza miaka miwili ya A level.
 
Back
Top Bottom