Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Dr. Kilometa za barabara naona tupo kundi moja la watu wanaotetemeka kwenye kuongea kiingereza
 
ubunge wa afrika mashariki ndo kipimo cha wanasiasa kwenye lugha hii ya UINGEREZA
 
Yeah...offcourse yes.....you know eeeeh... this...actually....[emoji17] [emoji28]
 
Sitasahau siku nilimuomba ruhusa second master na kumwambia " my headache is paining" doh
 
Hahahahahahhahahaha basi basi
 
Hii yellow book naijua hii!!
 
Nakumbuka chuo kuna jamaa alikuwa akiulizwa swali, kisha akaambiwa simama kuchangia lazima apumue.... Hadi siku moja Lecture akamuuliza hivi huwa unafanya makusudi au bahati mbaya? Akajibu namimi nashangaa yananikuta nikijibu kwa kingereza.
 
Mimi mara ya kwanza kuongea kiingereza nilikuwa safarini Nairobi.nikajua kila MTU Kenya anaongea English.nikiwa kwenye basi nikakaa jamaa mmoja.nikaona sehem flani wana kilimo CHA umwagiliaji nikasema " many farmers use navigation ! badala ya irrigation! jamaa akanicheki akanipotezea.ilikuwa shida mpaka nijipange dakika 10 kutoa sentensi
 
Doh! Huu uzi ni mkali...watu wanafunguka kwa kutoa experiences zao na lugha ya kiingereza.
Kuna matatizo mawili katika shule za serikali linapokuja suala la lugha:
1. Walimu wa lugha wengi wao hawaifahamu lugha kwa ufasaha. Hivyo hata ufundishaji wao siyo bora. Kunapelekea wanafunzi wengi kutojua lugha vizuri katika kuongea, kusoma na kuandika. Mara nyingi hawafundishi kwa ufasaha zile fundamentals za lugha.
2. Mazingira ya darasani kutokuwa rafiki kwa kujifunza. Kuna tabia hii ya kuchekana na kuzomeana pale mwanafunzi anapokosea. Kwa bahati mbaya, mara zingine waalimu ndiyo wa kwanza katika kuchochea uzomeaji na kuchekana.
 
Kiingereza mtihani wenyewe si mnamuona hata Mzee wetu!!! Full kuchapia! anyway Ras Simba apewe kazi pale Mjengoni.
 
Lugha uanze kuongea chuo kikuu? Ambako ni full vyama vya kikabila.
Utasikia UWASU, UWAMBE, CHAWAKAMA utajua lini?
 
Hahaha mkuu hiyo imetukuta wengi sana,haupo peke yako kwa ilo.
 
Without because hahaha
 
duuh kwa kweli unastahili pongezi mimi mbona ningetoka NDUKI tu kwani Seminar presentation ilikuwa na marks ngapi? sidhani kama zinazidi marks 10
Hahaha kumbe mnakimbiaga wengine.
 

Umenikumbusha kisa cha miaka hiyo Azania pale kila asubuhi tulikuwa na paredi tulikuwa na utaratibu wa morning talk.

Siku hiyo akaenda jamaa mmoja pale mbele kutuelezea kuhusu HIV/AIDS. Akaanza na definitions vizuri,sasa ilipofika kwenye ushauri akasema "Avoid to be...." Alirudia ili neno kama mara 5 alafu akakwamia hapo. Wanafunzi full kupiga makofi na kucheka.

Mpaka tunamaliza shule,jamaa tulikuwa tunamuita "avoid to be"

Ngeli noma.
 
skujuaga ombaomba anaitwaje kwa kingereza c siku io nikasema borrow borrow!!!watu hoi kwa kicheko alifu niliisema uku nipo serious scheck na mtu uso wa meeee!!!
 
nyanya chungu kwa kiingereza, mwenye kujua tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…