Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Dr. Kilometa za barabara naona tupo kundi moja la watu wanaotetemeka kwenye kuongea kiingereza
 
ubunge wa afrika mashariki ndo kipimo cha wanasiasa kwenye lugha hii ya UINGEREZA
 
Yeah...offcourse yes.....you know eeeeh... this...actually....[emoji17] [emoji28]
 
Sitasahau siku nilimuomba ruhusa second master na kumwambia " my headache is paining" doh
 
Kiingereza si masikhara aisee kuna Mzee Mmoja maarufu alishawahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM, kisha Katibu Mkuu wa Chama cha Siasa M... jamaa ngeli ilikuwa haipandi akipata wageni wa kuongea nao kiingereza ama asingizie anaumwa au amsukumie Katibu Tawala ha ha ha... Chezea Lugha wewe
Hahahahahahhahahaha basi basi
 
Siku moja tupo kwenye seminar ya koz moja inaitwa rural agricultural economy maarufu kama YELLOW BOOK kwa waliosoma SUA wataelewa, basi picha moja ilikua imebandikwa ukutani ikapulizwa upepo ikadondoka chini jamaa kule mbele akiwa na maiki alisema "what is that, ooh the picture drop down without becouse" basi tulicheka sana
Hii yellow book naijua hii!!
 
Wandugu kama mjuavyo wengi wetu tumesoma shule za st. Kayumba kwa hiyo Ngeli ni ishu kwetu. Basi kwa kuunga unga hivyo hivyo nikachaguliwa Chuo (UDSM) sasa kufika huko si ndo mambo ya Seminar za DS 101 natakiwa ni-present ilikuwa balaa usiku kabla ya seminar sikulala naogopa.

Kwenye seminar yenyewe sasa jasho lilinitoka mwili mzima balaa yaani naona nyota nyota tu daah! sitaki kukumbuka. Lakini namshukuru Mungu baada ya pale nilifanya bidii y kujifunza kwa kusoma zaidi vitabu vya kiingereza na kuongea na watu wasiojua kiswahili (hasa waganda, Wazambia & Waganda).

Angalau sasa mambo si mabaya Ulimi si mzito tena kiviile!!! English aisee ni hatari jamani. SHIKAMOO KIINGEREZA
Nakumbuka chuo kuna jamaa alikuwa akiulizwa swali, kisha akaambiwa simama kuchangia lazima apumue.... Hadi siku moja Lecture akamuuliza hivi huwa unafanya makusudi au bahati mbaya? Akajibu namimi nashangaa yananikuta nikijibu kwa kingereza.
 
Mimi mara ya kwanza kuongea kiingereza nilikuwa safarini Nairobi.nikajua kila MTU Kenya anaongea English.nikiwa kwenye basi nikakaa jamaa mmoja.nikaona sehem flani wana kilimo CHA umwagiliaji nikasema " many farmers use navigation ! badala ya irrigation! jamaa akanicheki akanipotezea.ilikuwa shida mpaka nijipange dakika 10 kutoa sentensi
 
Doh! Huu uzi ni mkali...watu wanafunguka kwa kutoa experiences zao na lugha ya kiingereza.
Kuna matatizo mawili katika shule za serikali linapokuja suala la lugha:
1. Walimu wa lugha wengi wao hawaifahamu lugha kwa ufasaha. Hivyo hata ufundishaji wao siyo bora. Kunapelekea wanafunzi wengi kutojua lugha vizuri katika kuongea, kusoma na kuandika. Mara nyingi hawafundishi kwa ufasaha zile fundamentals za lugha.
2. Mazingira ya darasani kutokuwa rafiki kwa kujifunza. Kuna tabia hii ya kuchekana na kuzomeana pale mwanafunzi anapokosea. Kwa bahati mbaya, mara zingine waalimu ndiyo wa kwanza katika kuchochea uzomeaji na kuchekana.
 
Kiingereza mtihani wenyewe si mnamuona hata Mzee wetu!!! Full kuchapia! anyway Ras Simba apewe kazi pale Mjengoni.
 
Lugha uanze kuongea chuo kikuu? Ambako ni full vyama vya kikabila.
Utasikia UWASU, UWAMBE, CHAWAKAMA utajua lini?
 
Hahaha mkuu hiyo imetukuta wengi sana,haupo peke yako kwa ilo.
 
Siku moja tupo kwenye seminar ya koz moja inaitwa rural agricultural economy maarufu kama YELLOW BOOK kwa waliosoma SUA wataelewa, basi picha moja ilikua imebandikwa ukutani ikapulizwa upepo ikadondoka chini jamaa kule mbele akiwa na maiki alisema "what is that, ooh the picture drop down without becouse" basi tulicheka sana
Without because hahaha
 
duuh kwa kweli unastahili pongezi mimi mbona ningetoka NDUKI tu kwani Seminar presentation ilikuwa na marks ngapi? sidhani kama zinazidi marks 10
Hahaha kumbe mnakimbiaga wengine.
 
Nakumbuka jamaa kabla ya seminar alikariri sana , sasa wakati wa presentation akasau neno basi akakauka mpaka dakika zake zimekwisha akarudi kukaa, class nzima iliangua kicheko.. seminar leader akampa zero out of ten..... jamaa aliporudi rum akasema ''leo nimeumbuka na kwa mtindo ctapata demu tena hapa chuo.''


mwingine aliwahi sema:

why? then akajibu because kwa sababu.

Yaan mambo ya seminar acha tu.

Umenikumbusha kisa cha miaka hiyo Azania pale kila asubuhi tulikuwa na paredi tulikuwa na utaratibu wa morning talk.

Siku hiyo akaenda jamaa mmoja pale mbele kutuelezea kuhusu HIV/AIDS. Akaanza na definitions vizuri,sasa ilipofika kwenye ushauri akasema "Avoid to be...." Alirudia ili neno kama mara 5 alafu akakwamia hapo. Wanafunzi full kupiga makofi na kucheka.

Mpaka tunamaliza shule,jamaa tulikuwa tunamuita "avoid to be"

Ngeli noma.
 
skujuaga ombaomba anaitwaje kwa kingereza c siku io nikasema borrow borrow!!!watu hoi kwa kicheko alifu niliisema uku nipo serious scheck na mtu uso wa meeee!!!
 
Back
Top Bottom