Siku ya kwanza kupika ilikuwaje? Ulichopika kiliiva?

Kama mimi tu mkuu. Ila mimi nachojitahidi ni kuchagua sufuria dogo ama kubwa kulingana na ukubwa wa ugali naoutaka.

Kwahiyo hilo nalisolve kiivo ila kama ingekua sufuria size moja apo ningekua nachemka daily.
 
Wali ulikuwa na mawe ya kutosha
 
wee naona tusubiri after 2 -3 yrs, maana uta kuja kupika matapu tapuπŸ˜ƒπŸ€£
 
Nilianza kupika nikiwa mdogo, na ndo mtoto pekee pale home aliyejua kupika akiwa mdogo.

Nimeanza kujifunza kupika ugali, nikiwa awali, nlikua kwa shangazi,

Mie ni mtundu na mfukunyuku wa kujua mapishi mbali mbali, hivyo kwenye kuandaa masapta sapta niko [emoji91][emoji91][emoji91]
 
Nakumbuka wife alipojifungua mtoto wa kwanza,kwa siku za mwanzo kazi nyingi ikiwemo ya upishi nilikuwa nafanya mwenyewe,sasa siku hiyo nikasema acha leo nikanunue samaki wale wakubwa nije nipike,nikaenda sokoni nikajipatia kitoweo changu nikarudi nyumbani kupika,nikamwandaa vizuri,nikaandaa na viungo pia vitunguu hoho nyanya limao na tangawizi,nilipomaliza kuweka viungo vyote na samaki jikoni nikasema acha nikaoge maana nilikuwa nahisi joto kutokana na kukaa jikoni muda mrefu,nikasema acha nijaze maji ili asije akaungua,nikaenda kuoga,nilipomaliza nikarudi,nikasema acha nifunue chungu huenda samaki wangu atakuwa ameshaiva Lahaula!!! Kuangalia nakuta samaki alishafufuka na kula vitunguu vyote yupo ananitazama tu,kumbe kile kitendo cha kujaza maji lilikuwa ni kosa kubwa sana.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…