dadapesa
JF-Expert Member
- Jun 16, 2020
- 366
- 659
Wali na dagaa kwangu hapana, hayo ni matumizi mabaya ya Mchele, kitu ubwabwa maharageNakumbuka mimi niliivisha vizuri tu wali wangu na dagaa kwenye jiko la mafuta. Nilikua nimepanga chumba kimoja na nyua ya chumba nilichokua nakaa kulikua na vyumba vingine vya wapangaji tumepeana migongo. Kwa hiyo madilisha ya vyumba vyetu yanatazamana.
Kutokana na joto la Dar, tukiacha madirisha wazi usiku, kila mmoja anaweza kuona ndani kwa mwenzie kama taa itakua imewashwa.
Sasa bana kwasababu siku hiyo ndio nilikua nimehamia hapo, niliamua kupika mapema, nikabenanisha sufuri ya wali na mboga kwenye jiko hilo la mafuta, nikapumzika kitandani.
Usingizi ulinipitia, kuja kushtuka nikasikia chumba cha jirani jamaa ameimport anachakata papuchi. Mechi ilikua kama wamepaniana vile.
Basi kwa sababu jamaa alikua amewasha taa na mimi nimezima, nikaamka mdogo mdogo kuelekea dirishani kuchungulia. Nikapiga teke jiko, nikamwaga mboga yote chini na sefuria ya wali ikajifunika chini.
Mchakataji akasitisha shughuli ghafla na kuzima taa. [emoji24][emoji24] Nikarudi mdogomdogo kitandani nikalala mpaka asubuhi.