Siku ya kwanza kupika ilikuwaje? Ulichopika kiliiva?

Siku ya kwanza kupika ilikuwaje? Ulichopika kiliiva?

Nilipiga sato kwenye chungu nikaweka chini na majani ya mgomba nikimuiga bibi yangu kuongeza udambwiudamwi. Kilichotokea nilikuta samaki ameungua kawa mweusi kama 2pac wa ghana.

Ilikuwa mara ya kwanza kuachwa home peke yangu kwa kushtukiza.
Daaah! Hayo yalikua mauaji ya samaki sio mapishi😂😂😂😂
 
Mimi nilikuwa napka wali kawaida boko nlipoanza ishi peke yangu.
Kuna mwanajeshi mwanaume alikuwa jiran alinifundisha kupika wali hadi leo nna muda nimepka ila mtu yeyote akionja wali niliopika huwa anasalute. Kati ya kitu najua kupka ni wali unachambuka balaa na ni kwa jiko la gesi au umeme nje ya hapo siwezi.
Shea maujuzi hayo Mkuu
 
'Mecheka sanaaa.
Kwenye pishi la ugali kwa mara ya kwanza wengi sana hukosea.
Mie nakumbuka nikiwa drs la nne dada alinilazimisha kupika ugali wa watu zaidi ya 10 kwenye jiko la mkaa.

Nikabana mbanio kwa kutumia mapaja, moto ni mkali , aisee sitasahau. Ugali ulikuwa na mabongebonge ya kutosha japo uliiva😀
 
Kuna siku nilikuwa home alone si nikapika njegere nikajua Kama maharage tia maji mengi nikayaacha yachemkie nakuja kufunua nakuta uji wa njegere nikayaunga ivoivo kibishi

Muda wa kula nikawa napaka njegere juu ya wali Kama vile blue band jinsi inavyopakwa kwenye mkate😁
 
Huyo alikuonea kwakweli, ugali wa watu 10+ si mchezo
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Huyo alikuonea kwakweli, ugali wa watu 10+ si mchezo
Hapo wengi walikuwa ni wadogo, watu wazima walikuwa kama wawili. So, haukuwa mkubwa kiihivyo! Sema nilikuwa sijawahi kupika ugali hata wa mtu mmoja.
Huyo dada alinifundisha kazi nyingi sana katika umri mdogo. Kukanda unga wa maandazi 2kg, kupika sambusa nk. Alinikomaza hadi leo sitetereki
 
Back
Top Bottom