Ndiyo mkuu mimi ni mashoto tena wa ukweli ukweli haswaa!
barafu kaelezea mengi na yote ni kweli tupu kwamba yaanakisi uhalisia wa matendo yetu na uwezo tulio barikiwa.
Binafsi siku zote naishi na kufanya mambo yangu kwa kujiamini na kwa ujasili mkubwa.
Siyumbishwi wala kutishwa na jambo lolote hata kama liwe gumu vipi.
Maisha yangu yote nimekuwa sio mtu wa kumtegemea binaadam yeyote.
Nakumbuka nilipo hitimu chuo, nilikaa mtaani miezi5 nikapata ajira kwenye taasisi kubwa ya kimataifa bila kushikwa mkono na mtu.
Nilidumu kwenye ajira ile kwa muda mfupi sana nikajiona siko upande sahihi, nikapiga chini mzigo na kuangalia hamsini zangu nje ya ulingo wa mkoloni.
Leo mwaka wa nane nipo kitaa sina stress sihofii chochote nasonga kivyangu.