Siku ya Mashoto Duniani: Wana JF wenzangu tunaotumia mkono wa kushoto tukutane hapa

Mimi mwalimu wangu alinizuia kuandikia kushoto. Dah mpaka sasa mwandiko wangu sio mzuri. Lakini kazi zingine zote natumia kushoto.

Mimi nashukuru wazazi wangu na waalimu hawakuwahi kunikataza, ila kuliluwa na shangazi yangu nikienda kwake sishibi maana ananilazimisha kula na kulia akawa adui yangu.Lakini nilivyukuwa mkubwa kila nikienda hotelini nikila watu wote wananikodolea macho kwa kweli hapo nilimkumbuka shangazi.
 
Nami nimo mkuu....ila bao bonye la simu napiga zaidi kwa mkono wa kulia
 
Swali
Mkila mnatumia left or right?
Mkitawaza je?
 
binti yangu pia ni mashoto!
Tulimlazimisha kuandikia kulia!
hajaweza kuwa na mwandiko mzuri mpka kesho!
NIMEGUSIKA HAPA, kama mzazi!
Nami pia mkuu.....mama yake pamoja na walimu walilazimisha weeeeee! Januari ya mwaka huu wamelazimika kumpa uhuru wa kutumia mkono wake wa dhahabu. Sasa yuko grade seven kaurudia mkono wake kama kawaaaa
 
Mimi pia ni mashoto natunga mashairi nachora na pia mashoto wengi tunapindisha shingo tukitembea
 
Mie sikuwahi kutengwa sema zamani dawati moja tulikuwa tunakaa watu watano ilikuwa mbinde kugeuza daftari maana nilikuwa nakaa opposite na wenzangu
 
Jamani Hata mimi Mkalusanga natumia Mashoto pia Nilipigwa na Mwalimu kama Wewe Ulivyopigwa ila vitu Vyote natumia shoto kasoro kuandika tuu najisikia Faraja tupo Wengi
 
Kasoro kula kwa mkono (nilichapwa sana) na kupiga gitaa, siwezi kutumia kushoto kupiga guitar sijui kwanini imetokea natural.
 
Lefthanders wote tutembee vifua mbele. Tupo kwenye raiti traki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…