Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Mzee inamaana hujui Mchango wa Kanisa au hupendi kutambua Mchango huo kwenye harakati za kupigania Uhuru?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Evil...Sawa Mzee Mohamed nimekuelewa
Uzalendo...Mzee.
Naona ajabu tena kubwa kila kukicha wataja tu wanaharakati wa Kiislamu kwenye kupigania Uhuru wetu. Yaani ni kama vile Uhuru uliokuwa unatafutwa ulikuwa wa kusimamisha Dola ya Kiislamu
Hahahahahaha..kwa jinsi ulivyoandika na vile napajua hapo basi nimevuta taswira ya eneo lote hilo ..je hii nyumba ndio ile inatazama geti la Jengo la ccm mkoa ? Iliko hotel ya wasomali ..baada ya wasomali ofc za gazeti sikumbuki jinaAngalia hapo juu picha ya Bi. Mwamtoro bint Chuma mama yake Sheikh Haidar Mwinyimvua.
Picha hii inamwonyesha Bi. Mwamtoro bint Chuma akipiga kura Uchaguzi Mkuu wa 1970.
Bila ya shaka yoyote kura yake ilikwenda kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Haiwezi kuwa vinginevyo.
Bi. Mwamtoro alikuwa mmoja wa akina mama waliokuwa mstari wa mbele katika TANU.
Bibi huyu aliishi zaidi ya miaka 100 na alifariki tarehe 11 May 1981.
Nyumba yake ilikuwa Mtaa wa Kariakoo na New Street No. 69 nyuma ya ofisi ya TAA miaka ya 1930 na nyuma ya TANU katika miaka ya 1950.
Hii nyumba hivi sasa iko nyuma ya ofisi ndogo ya CCM, Lumumba Avenue.
Nyumba hii yenye historia kubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika bado ipo katika mikono ya familia ya Mzee Haidar Mwinyimvua.
Nyumba mbili hizi, Ofisi ya TANU na nyumba ya Bi. Mwamtoro ilikuwa zilikuwa katika miaka ile zkitenganishwa na ua wa makuti.
Siku ya mkutano wa ndani wa TANU Nyerere akija kuzungumza na wanachama wa TANU haya makuti yalikuwa yanaondolewa hivyo kuunganisha nyua hizi mbili kuwa ua mmoja.
Wanawake wakikaa nyuma na wanaume wakiwa mbele.
Huu ndiyo ulikuwa uwanja wao akina Bi. Titi Mohamed, Bi. Hawa bint Maftah, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Chiku bint Said Kisusa kwa kuwataja wachache.
Wakimaliza mkutano wanawake walikuwa wanaingia kwenye nyumba ya mtoto wa Bi.
Mwamtoro, Haidar Mwinyimvua.
Nyumba hii mlango wake ulikuwa Mtaa wa Udoe ukitumiwa makhsusi na wanawake kwa kuingia na kutoka kuepuka kupishana na wanaume.
Wakati wa uhai wake marehemu Rashid Mfaume Kawawa aliwaambia ndugu zake Sheikh Haidar Mwinyimvua kuwa nyumba yao hii imebeba kumbukumbu nyingi za harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na endapo watataka kuiuza basi wakifikirie chama kwanza kabla ya mnunuzi mwingine.
Wazo zuri sanaUkisikia msemo "kujitolea hali na mali" basi hawa ndio mfano mkubwa kwa jitihada zao katika kudai uhuru.
Ingefaa hizi sehemu muhimu katika historia zinge bandiikiwa vibao vidogo (plaque) kueleza kwa muhtasari tukio la kihistoria lililo tokea kwenye nyumba hiyo.
Hivi vibao vinatumika sana nchi nyingi kuelezea matukio ya kihistoria katoka jengo hata kama kwa sasa linamilikiwa na mtu mwingine.
Tre...Hahahahahaha..kwa jinsi ulivyoandika na vile napajua hapo basi nimevuta taswira ya eneo lote hilo ..je hii nyumba ndio ile inatazama geti la Jengo la ccm mkoa ? Iliko hotel ya wasomali ..baada ya wasomali ofc za gazeti sikumbuki jina