Siku ya mwandiko duniani: Mwalimu wako aliyekufundisha mwandiko unamkumbuka?

Siku ya mwandiko duniani: Mwalimu wako aliyekufundisha mwandiko unamkumbuka?

Kiasili Nina muandiko mbovu, nlikuwa najitahidi Tu ili nionekane naandika vizuri, lakini once kichwa kikipata moto basi narudi kwenye Hali yangu ya muandiko wa ulalo wa bata. Nakumbuka mtihani wangu ulikuwa unasahihishwa mwanzo kabisa akili za walimu zikiwa active mana kinyume na hapo maneno mfano "Kama" ukikaa vibaya unaweza kusoma Kama "K*Uma" au "Kima....Zishukuriwe simu na vifaa vyote vya teknolojia vinavyotusaidia kuandika.
 
Mwalimu Scarion alinikataza kuandika nikiwa nimesimama. Nilikuwa naona ananionea sasa nitaandikaje nimekaa mkono utakuwa kwenye dawati.
 
Mamq Mchilasi popote ulipo kula gwala. Ila sitasahau ulinichapa sana stiki za mkono wa kishoto Ili niansikie mkono wa kulia. Big mwalimu Mwafalo the headteacher kwa kumpa somo mama Mchilasi kwamba hata mkono wa mashoto hauna shida kwa kuandikia ni maumbile tuu. Ndio ikawa pona pona yangu.
 
Nawakumbuka mwalimu mrutu na mwalimu asha saidi(R.I.P). Enzi hizo bwilingu primary chalinze..
 
Namkumbuka sana,alikuwa akiitwa Modester Matagane,segese-kahama, miaka ile!!

Sijui kama yu hai au laaah,maana ni miaka almost 40 sasa
Mimi tokea 1988 ni almost 38 yrs ila yule mama simkumbuki jina maana alihama shule akili zikiwa bado kuchaji vizuli.
ila wa darasa 2-7 nawajua kwa majina
 
Mmenikumbusha mbali sana, kuna demu secondary alinipenda kwasababu nilikua na hati (mwandiko)mzuri, nilikua na hati zaidi ya moja kila somo na hati yake, wakawa wanasema "nina hati nzuri!" Kila daftar na mwandiko wake.

Kuna wengine nao mwandiko mlikua mnaita hati?
Hati- kiswahili
ni neno linalotokana na lugha ya kiarabu neno KHATWI (likimaanisha mwandiko)
 
Mamq Mchilasi popote ulipo kula gwala. Ila sitasahau ulinichapa sana stiki za mkono wa kishoto Ili niansikie mkono wa kulia. Big mwalimu Mwafalo the headteacher kwa kumpa somo mama Mchilasi kwamba hata mkono wa mashoto hauna shida kwa kuandikia ni maumbile tuu. Ndio ikawa pona pona yangu.
huyo mwalimu alikuwa mwehu kutikujua kuwa kuna watu wanatumia mkono wa kushoto kuandika
 
Mmenikumbusha mbali sana, kuna demu secondary alinipenda kwasababu nilikua na hati (mwandiko)mzuri, nilikua na hati zaidi ya moja kila somo na hati yake, wakawa wanasema "nina hati nzuri!" Kila daftar na mwandiko wake.

Kuna wengine nao mwandiko mlikua mnaita hati?
Safi, hebu andika tuone maandiko wana JF
 
Back
Top Bottom