Mwandiko mbaya huwa naamini mpaka leo nilisababishiwa na mwalimu Magadula nikiwa darasa la kwanza mwezi January shule ya msingi Nyakabungo mwanza,yule bibi aliyekuwa anakaribia kustaafu ni kama alinilaani😭 kisa chenyewe kilikuwa hivi:- nakumbuka ilikuwa siku chache baada ya kuandikishwa na Mzee wangu darasa la kwanza shuleni hapo,siku hiyo nipo darasani na mwalimu anaendelea kuuliza maswali ya hesabu maana alikuwa anafundisha hesabu muda huo,aliandika ubaoni namba 0-10 na alikuwa anachagua mwanafunzi yoyote anaenda mbele Kisha aoneshe namba anayotajiwa na mwalimu Kisha mwanafunzi anaigusa Kwa rula.Kimbembe na dhahama kikaangukia kwangu nilipoambiwa nioneshe namba 7 nikasogea ubaoni Kwa kweli kutokana na utoto na woga nilijikanyaga takribani dakika moja bila kuonesha namba 7 ilipo.Ghafla bin fuvuuuu nilishtukia fimbo imetua mgongoni na hapo ndipo nilipoanza kuona nyota nyota na dunia yote imenigeuka.Huwa sipendi unyonge tangu nikiwa mtoto,nilichofanya nilijikaza kiume na kuangalia wapi ulipo mlango wa kutokea maana fimbo ziliendelea kushuka kama mvua bila kujali zinatua sehemu gani ya mwili(sijajua yule mwalimu alikuwa na msongo gani wa mawazo siku ile mpaka aniadhibu kikatili namna ile mbele ya darasa kwa kosa dogo lile!!!!) Nilifanikiwa kutoka nje ya darasa nikiwa na taharuki na maumivu Makali ila ninachokumbuka nilishusha mvua ya matusi Kwa yule mwalimu na tusi ninalokumbuka ni KUM* MAYO wewe (Mungu anisamehe kwa kweli maana sikujua hilo tusi lilitoka toka vipi tena kwa mwalimu na kwa sauti kubwa mpaka walimu ofisini na wanafunzi madarasani wakasimama kuchungulia madirishani ni nani huyo anatoa matusi mazito kati kati ya shule!!!). Kilichofuata niliangalia uelekeo wa njia iko wapi ili ninusuru roho yangu Kwa kukimbia,ila sikufika mbali niliona shule nzima inanifukuza Kila mwanafunzi mkubwa na mdogo akitamani awe wa kwanza kunikamata ili ajenge CV Kwa walimu(uchawa umeanza zamani sana😂 na ndio maana huwa sitaki kuwa chawa) kufupisha stori sikufika mbali nilikamatwa na mapande ya mababa nafikiri walikuwa Drs la Saba au la sita wale huku napigwa mitama na makofi ya kila aina yaani unapigwa mtama kabla hujaanguka chini unadakwa unapewa mtama mwingine tena,ndani ya dk 1 sare ya shule ilikuwa imechakaa,bahati nzuri Kuna mwalimu aliwahi kufika eneo la tukio la kuamuru wale wanafunzi wasinipige wanipeleke ofisini.Huko ndipo nilipata kipigo cha kufa mtu maana kila mwalimu alinipiga fimbo mpaka aone ametosheka yeye.TANGU TUKIO LILE NILICHUKIWA NA WALIMU WOTE na nilikaa na machungu yangu sikwenda kumwambia mtu yeyote nyumbani vinginevyo Mzee angepata taarifa angenihamisha shule.Yule mwalimu magadula alistaafu mwaka huo huo na kwa kweli niliichukia shule mapema tu tangu nimeandikishwa darasa la kwanza hiyo january na ndio chanzo cha mwandiko wangu mbaya maana walimu walinisusa kwa kumtukana mwalimu mwenzao mbele ya kadamnasi