Siku ya Safari za Anga za Juu Duniani: Kuchunguza ulimwengu ni ndoto ya wanadamu wote

Siku ya Safari za Anga za Juu Duniani: Kuchunguza ulimwengu ni ndoto ya wanadamu wote

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111374271214.png


Leo Aprili 12 ni Siku ya Safari za Anga za Juu Duniani au kwa jina lingine ni Siku ya Kimataifa ya Binadamu Kwenda Angani. Kutoka "mazungumzo kati ya mbingu na dunia" na wanaanga wanaotekeleza majukumu kwenye anga za juu, kujibu barua za wanasayansi wazee walioshiriki katika operesheni ya kurusha satilaiti ya kwanza ya China iitwayo "Dongfanghong No. 1", hadi kukutana kwa ukarimu na wanaanga mara nyingi. Kama mamia ya mamilioni ya Wachina, Rais Xi Jinping wa China ana hisia nzito moyoni mwake kuhusu safari za anga za juu. Amesisitiza kuwa, kuendeleza shughuli za anga na kujenga nchi yenye nguvu kwenye sekta ya anga za juu ni harakati ya watu wa China isiyo na kikomo ya kutimiza ndoto hiyo ya anga.

Wakati huo huo, Xi Jinping anaangalia ulimwengu moyoni yaani "kukuza sekta ya anga ili kuwanufaisha wanadamu wote". Alisema, "sekta ya anga ni shughuli ya wanadamu wote, na kuchunguza ulimwengu mkubwa ni ndoto ya pamoja ya wanadamu wote." Tukichukulia mfano ushirikiano kati ya China na Afrika katika mfumo wa uongozaji wa satilaiti wa Beidou kimataifa, ujenzi wa mfumo huo ulikamilika mwaka 2020, na kuifanya China kuwa nchi ya tatu duniani kumiliki mfumo wa kimataifa wa uongozaji wa satelaiti kwa kujitegemea.

Kutoka kilimo cha kisasa hadi upimaji wa ardhi na uchoraji ramani, kutoka ujenzi wa kidijitali hadi ufuatiliaji wa hali ya hewa, mfumo wa uongozaji wa Beidou na bidhaa zinazohusika zinatumika katika nchi nyingi zaidi za Afrika, na kuchangia upunguzaji umaskini na maendeleo barani Afrika.

Kama rais Xi Jinping alivyosema alipokutana na wafanyakazi wa sayansi ya anga ya juu wa China, "Endelea na juhudi za kukuza maendeleo ya sekta ya anga ya dunia, na kuchangia zaidi hekima ya China, ufumbuzi wa China, na nguvu ya China kwa wanadamu kutumia kwa amani anga ya juu na ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja."
 
Back
Top Bottom