SIKU YA VIJANA: Rais Samia na Elimu na Ujuzi kwa vijana

SIKU YA VIJANA: Rais Samia na Elimu na Ujuzi kwa vijana

kevylameck

Member
Joined
Nov 3, 2013
Posts
18
Reaction score
19
Rais Samia Suluhu.jpg

Na Kevin Lameck

Dunia inapoadhimisha siku ya Vijana hii leo, yapo baadhi ya mambo yaliyofanywa na kutekelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye kuwakwamua dhidi ya changamoto mbalimbali zinazowakwaza Vijana.

Changamoto kubwa inayotajwa nchini Tanzania miongoni mwa Vijana wake ni pamoja na suala la Elimu na Ujuzi miongoni mwa vijana.

Katika kushughulikia suala hili jitihada mbalimbali zimechukuliwa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha suala hilo linapata ufumbuzi wa haraka.

Tayari serikali inatoa elimu bila malipo kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita, Serikali pia imeongeza idadi ya shule za sekondari pamoja na mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi.

Zaidi ya Bilioni 500 zimekuwa zikitolewa na serikali ya Rais samia ambazo huwanufaisha wanafunzi wa vyuo vikuu takribani 160,000.

Kuhusu Ujuzi,Hatua mbalimbali zimechukuliwa na Serikali ya Rais Samia ikiwamo kujenga vyuo vya Ufundi kwenye wilaya ya Mikoa.

Bajeti ya Serikali ya Mwaka Huu, Rais Samia ameidhinisha Milioni 100 kutoka serikalini ili kwenda kujenga vyuo hivyo kwenye wilaya 36 pekee ambazo zilikuwa zimesalia bila kuwa na vyuo vya ufundi.

Serikali pia imeanzisha vituo mahiri vya mafunzo kwa taasisi ya elimu ili kuzalisha vijana wenye hwezo unaohitajika, ambapo kiasi cha Dola za Marekani Milioni 75 zinatumika.

Vituo hivyo ni taasisi ya teknolojia Dar Es salaam itakayobobea kwenye TEHAMA na Taasisi ya Teknolojia cha Jijini Mwanza kitakachobobea kwenye ngozi, Chuo cha Taifa cha usafirishaji kitabobea kwenye taaluma ya anga wakati chuo cha Arusha ufundi kitabobea kwenye nishati jadifu.

Serikali pia imeboresha kituo cha jemolojia Tanzania kilichopo Arusha ambacho kinatoa mafunzo ya ngazi ya cheti na diploma katika fani ya madini na usonara, utambuzi wa madini ya vito, ukataji na ung'arishaji na utengenezaji mapambo na urembo.

Serikali pia inaimarisha chuo cha Sanaa Bagamoyo.

Serikali ya Rais Samia pia inajenga sport Arena na vituo vya michezo (academy) katika mikoa mbalimbali ili kukuza ujuzi na vipaji katika michezo.

Serikali ya Rais Samia pia imetekeleza programu ya kitaifa ya kujuza ujuzi ambapo mpaka mwaka jana mwishoni, Vijana 65,598 wamewezeshwa kupata ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa.

Vijana hao wamejengewa uwezo kwenye sekta ya utalii na ukarimu (Tourism and hospitality),ujenzi, tehama,kilimo biashara,ushonaji nguo na viwanda.

Kubwa la mwisho, Serikali ya Rais Samia pia inapitia mitaala ya elimu nchini Tanzania kama ambavyo aliahidi wakati akihutubia bunge la Tanzania.

Lengo ni kuhuisha mitaala ya elimu na kuifanya kuwa na ujuzi zaidi wa kuwasaidia wahitimu kuwa na uwezo wa kujitegemea, kujisimamia na kujiajiri wenyewe kupitia ujuzi watakaoupata darasani.

Siku ya Vijana duniani huadhimishwa kila tarehe 12 agosti ili kutambua nguvu kazi ya vijana sambamba na kujadili kuhusu changamoto na madhila wanayopitia vijana kote duniani.

Kazi Iendelee......
 
Baada ya ufafanuzi na kusuta utasikia "Kaangalieni na wengine wanafanyeje huko Ili tujue tunakwendaje kwendaje sie kama taifa" hapo ndo imeisha hivyo 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom