Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Kuna hii kitu yetu inaitwa siku ya wanawake, kuna hii kitu inaitwa super woman na kuna hii kitu tumeanzisha inasema mwanamke ni kichwa cha familia.
Wanawake kuna sehemu tumetumbukizwa shimoni na wapigania haki za wanawake na bila kujijua tumejaa viburi na sasa tunajitokeza hadharani kudai sisi kwa asilimia kubwa ndio tunalisha familia.
Wanawake wengi wenye mentality kwamba wanalisha familia ndoa zao zimeyumba na watoto wapo taabani kimalezi kwa sababu tu walezi wamepishana.
Dini zipo na zinaeleza vyema lipi jukumu la mwanamke ila kwa kasi tuliyonayo imetufanya twende kinyume kabisa na maandiko, tukipata nguvu kidogo tu ya uteuzi au kupata kamtaji kwetu tayari ni agenda yakuwaumiza wanaume. Wanaume wakituchoka wakaondoka hapo ndipo tunajua sisi kamwe hatuwezi kuwa kichwa cha familia.
Tukubali tukatae tunapaswa kuishi na wanaume kama vichwa vya familia na sisi ni mkia. Tukijitutumua na hadithi za super woman tutaishia kutumiwa na makundi ya wanaume huku tukiwa tunakwama kwenye malezi. Tuwaheshimu waume zetu regardless ya vyeo vyetu na madaraka au fedha zetu.
I'm not thinking of superwoman rather gifted woman.